NUKUU ZA SOMO
ELIMU YA DINI YA
KIISILAMU
KIDATO CHA TATU
MADA ZOTE ZA KIDATO CHA TATU
1. DINI SAHIHI ANAYOSTAHIKI KUFUATA MWANUAADAMU.
Kulingana na umbile lake,
mwanaadamu daima hutamani kuishi kwa furaha na amani ili kufikia lengo la
kuumbwa, na hapo ndipo inambidi kuchagua dini (njia sahihi ya maisha) kati ya
Uislamu, Ukafiri, Ushirikina au Utawa itakayomtimizia malengo yake.
1.1. Sifa
au Vigezo Vya dini sahihi
Dini sahihi ni ile inayomuwezesha mwanaadamu kuishi kwa furaha na amani
ya kweli hapa Duniani na Akhera, na ni lazima iwe na sifa zifuatazo;
(a)
Dini sahihi lazima ieleze ukweli juu ya
maumbile;
Ni
lazima ieleze ukweli juu ya mwanaadamu, lengo la kuumbwa kwake, hadhi/nafasi
yake, dhima/kazi yake na maumbile yanayomzunguka na viumbe vyote vilivyo hai na
visivyo hai, na hatima ya kila kitu.
(b)
Dini sahihi ni lazima iwe na kanuni na sheria
zinazoendana na maumbile yote;
Kanuni
na sheria za dini sahihi ni lazima ziwe sambamba na kanuni za kimaumbile ili
kuepusha mgongano wowote wa kimahitajio wa kimwili na kimazingira pia.
(c)
Ni lazima itosheleze mahitajio ya mwanaadamu
ya kimwili na kiroho;
Pia
ni wajibu kwa dini sahihi kuelekeza na kutosheleza hisia za mwanaadamu pindi
anapokuwa na hali ya furaha au hali ya majonzi, namna ya kukabiliana nazo ili
kubakia katika lengo lake la kuumbwa (maisha).
(d)
Dini sahihi pia lazima iwe ni mfumo wa
maisha uliokamilika;
Dini
sahihi haina budi kuwa na utaratibu kamili wa kila kipengele na Nyanja ya
maisha ya kila siku kiuchumi, kisiasa, kiafya, kiutamaduni, kisheria, kielimu,
n.k.
(e)
Pia dini sahihi ni lazima iwe na ibada
maalum zinazombakisha mwanaadamu katika maadili na hadhi yake;
Ni
wajibu kwa dini sahihi kuwa na muongozo wa kumuinua na kumbakisha mwanaadamu
katika mwenendo mzuri wa kiroho (kiutu) unaoweza kuustawisha mwili na kuleta
mahusiano mazuri ya kiutu yasiyo na chuki, husuda, tamaa, kiburi, vurugu, n.k.
(f)
Dini sahihi haina budi kuwa ya walimwengu
wote na ya nyakati zote;
Ili
kufikia lengo la kuumbwa mwanaadamu, dini sahihi ni lazima iwe inawahusu watu
wa aina zote (wote), isiwe na jina la mtu au mahali na isiwe na mipaka ya
kijiografia, rangi za watu, mahali, nyakati, n.k.
(g)
Dini sahihi ni lazima iainishe na kusimamia
haki zote za mwanaadamu;
Ni
wajibu kwa dini sahihi kutoa na kusimamia haki, hukumu na adhabu kwa usawa na
uadilifu kwa watu wote kibinafsi na kijamii bila upendeleo na ubaguzi wowote wa
kirangi, taifa, nasaba, cheo au hadhi.
1.2. Kwa
Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ?
Au
Haja ya kuhitaji mwongozo kutoka kwa
Mwenyezi Mungu (s.w).
Mwanaadamu pamoja na ujuzi na utundu alionao, hana uwezo wa kujiundia
dini sahihi (mfumo sahihi wa maisha) utakaomfikisha na kumbakisha kwenye lengo
la kuumbwa kwake. Na hii ni kutokana na sababu zifuatazo;
(a)
Mwanaadamu anaathiriwa na matashi ya
kibinafsi;
Pamoja
na ujuzi, utambuzi na vipawa alivyopewa mwanaadamu, bado uamuzi na fikra zake
ziaathiriwa na matashi ya nafsi yake katika upendeleo, uonevu na chuki, hivyo
hawezi kuunda mfumo utakaosimamia haki na uadilifu.
(b)
Nyenzo anazotumia mwanaadamu kujielimisha ni
dhaifu;
Mwanaadamu
hujielimisha kupitia nyenzo zifuatazo;
i.
Milango ya fahamu.
Kama vile pua, masikio, ulimi, macho, ngozi, n.k, ambavyo vyote vina
udhaifu na mara nyingine hutoa taarifu zisizo na ukweli.
ii.
Akili na fikra.
Uamuzi wa mwanaadamu wa akili na fikra peke yake hauwezi kutoa
jibu/mwongozo sahihi wa maisha kwani huathiriwa na wakati, matashi, mazingira,
uelewa, upeo wa kufikiri na pia una kikomo. Rejea Qur’an(10:36,66), (25:43,45),
(6:116) na (28:60)
iii.
Sayansi na Uchunguzi;
Sayansi na majaribio haviwezi kutumika kama nyenzo kuu ya kuunda muongozo
sahihi kwani vyote hivyo vinategemea milango ya fahamu ambayo nayo ina madhaifu
mengi na kikomo pia.
iv.
Historia;
Kutumia uzoefu wa kihistoria katika kuunda muongozo sahihi wa maisha ni
dhaifu kwa sababu mwanaadamu huathiriwa na uzoefu na ujuzi wa awali na hivyo
kutokubaliana na mabadiliko yeyote yatakayojitokeza. Rejea Qur’an(2:170, 257),
(5:104) na (6:116).
1.3. Sababu
Ya Uislamu Kuwa Ndiyo Dini Sahihi Pekee.
Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kuchaguliwa na kufuatwa kama
muongozo sahihi wa maisha na watu wote kwa sababu zifuatazo;
(a)
Uislamu unaeleza ukweli juu ya maumbile na
nafasi ya mwanaadamu hapa Duniani;
Uislamu unaeleza lengo la kuumbwa mwanaadamu kuwa ni ibada na kumtumikia
Mwenyezi Mungu na kuwa msimamizi wa sheria na hukumu zake hapa ulimwenguni ili
kupata radhi zake. Qur’an(51:56) na
(2:29).
(b)
Sheria na kanuni za Uislamu zinaendana na
kanuni za kimaumbile;
Uislamu ndiyo dini pekee inaenda na kuzingatia kanuni na taratibu zote za
kimaumbile za kibailojia kifizikia na kikemia ya viumbe vyote vilivyo na visivyo
hai ikiwa ni pamoja na maumbile au mazingira yanayotuzunguka. Rejea Qur’an(3:83) na (30:30).
(c)
Uislamu ndio dini inayotosheleza matashi
yote ya mwanaadamu kimwili na kiroho;
Uislamu ni dini inayotoa muongozo namna ya mtu kumiliki hisia zake na
kuendea mambo katika hali tofauti tofauti kama vile wakati wa furaha, shida,
huzuni, misiba, n.k.Rejea Qur’an(2:155-157).
(d)
Uislamu ni njia kamili ya maisha;
Ni Uislamu pekee ndio mfumo kamili wa maisha ya kila siku ya mwanaadamu
katika fani na nyanja zote za kibinafsi na kijamii kama vile kisiasa, kiuchumi
na kiutamaduni.
(e)
Uislamu una ibada maalum za kumjenga mwanaadamu
kimaadili;
Uislamu umeweka muongozo katika kumuadilisha mwanaadamu kupitia ibada
maalum kama vile swala, funga, hija, kutoa zakat na sadaqat na zinginezo za
sunnah.
(f)
Uislamu ni dini ya walimwengu wote na wa
nyakati zote;
Uislamu umekuwa ni mwongozo wa maisha tangu binaadamu wa kwanza hadi wa
mwisho katika Nyanja zote za maisha bila kujali taifa, ukoo, rangi na hadhi ya
watu.Rejea Qur’an(42:13).
(g)
Uislamu ni dini ya kusimamia haki, uadilifu
na usawa;
Ni dini ya Uislamu ndiyo inayotoa na kusimamia kwa usawa na uadilifu
haki, hukumu na adhabu zote kwa watu wote bila ya upendeleo na ubaguzi wa
rangi, taifa, hadhi na ukoo.Rejea Qur’an(103:1-3), (9:33), (61:9) na (17:105).
1.4. Maana ya Kusimamisha Uislamu katika jamii.
Ni pale ambapo waislamu katika jamii wataweza kuendesha kila kipengele
cha maisha yao ya binafsi na jamii katika siasa, uchumi, utamaduni, n.k kwa
kufuata kikamilifu muongozo wa Qur’anna Sunnah. Rejeab Qur’an(3:83), (10:99), (32:13),
(61:8) na (64:2).
1.5. Umuhimu wa Jihad katika kusimamisha Uislamu
katika jamii.
i.
Kusimamisha Uislamu (Jihad) katika jamii ni
amri (faradh).
Kama ilivyoamrishwa swala, funga, zakat na hijja, Neno
“kutiba”
(mmelazimishwa) limetumika katika jihad kama lilivyotumika katika kufunga,
kulipa kisasi na faradh zingine pia za kutekeleza Uislamu. Rejea Qur’an(2:216), (2:183), (2:178,180) na
(22:78).
ii.
Msamaha na Pepo hupatikana kwa kufanya
juhudi (jihad) za maksudi katika kusimamisha Uislamu katika jamii.
Kutekeleza faradh kama swala, funga, zaka na hija na ibada zingine za
sunnah za binfsi, itakuwa sio sababu ya msingi ya kupata msamaha na pepo ya
Mungu, mpaka jitihada ya dhati katika kupigania Uislamu katika jamii ifanyike. Rejea Qur’an(4:74), (9:111), (61:10-13),
(2:154), (3:169-171), (3:142), (3:157), (2:214) na (9:16).
iii.
Mwenyezi Mungu (s.w) ameteremsha chuma
(silaha) kuwa nyenzo ya kusimamisha Uislamu katika jamii.
Mitume wametumwa kusimamia haki na uadilifu katika jamii kwa kutumia
miongozo ya vitabu vya Allah (s.w) na pia chuma (silaha) kimeteremshwa ili
mitume na waumini wakitumie katika kusimamia haki na uadilifu ndani ya
jamii.Rejea Qur’an(57:25).
iv.
Kusimamisha Uislamu katika jamii ndio lengo
kuu la maisha ya Waumini.
Mwenyezi Mungu (s.w) ametubainishia kuwa chochote
tutakachokipenda au tutakachokifanya nje na lengo la kusimamisha Uislamu katika
jamii hatakuwa na radhi juu yetu. Rejea Qur’an (9:23-24).
1.6. Kwa nini ni muhimu
Kusimamisha Uislamu katika jamii?
Ni muhimu Uislamu kusimama katika jamii ili matunda yafuatayo yapatikane;
i.
Waumini wataweza kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w)
ipasavyo kwa mujibu wa Qur’anna Sunnah kwa kila kipengele cha maisha ya kila
siku binafsi na jamii katika siasa, uchumi, elimu, utamaduni kama
wanavyotekeleza swala, funga, hija, n.k.
Rejea Qur’an(51:56), (2:21-22), (7:54), (9:31), (2:85), (2:208),
(2:193), (4:75-76), (9:38), (8:39), (22:40) na (47:7).
ii.
Kupatikana amani ya kweli na kuondoka hofu na mashaka
katika jamii. Hii ni baada ya waumini kuchukua hatamu ya uongozi katika jamii
kwa mujibu wa muongozo na sheria za Mwenyezi Mungu (s.w). Rejea Qur’an(57:25), (2:257) na (5:90-91).
iii.
Waumini wataweza kuamrisha mema na kukataza maovu
kikamilifu katika jamii pasina kikwazo chochote pindi watakapochukua nafasi ya
kuiongoza jamii. Rejea Qur’an(22:41) na
(3:110).
iv.
Kuikinga jamii na majanga mbali mbali. Waumini
watakapochukua nafasi za kuiongoza jamii ndio itakuwa sababu ya kutoweka maovu
ndani jamii ambayo ndio sababu ya kupatikana majanga katika jamii. Rejea Qur’an(8:25).
2. NGUZO ZA IMANI
2.1. Kumuamini Mwenyezi Mungu (S.W).
§ Madai ya Makafiri dhidi ya uwepo wa Allah
(s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.
Makafiri wa zamani na wa zama hizi wakiwemo Charles Darwin, Friedrich
Engles, n.k wanadai kuwa imani ya uwepo wa Mungu Muumba dhana tu haina dalili
yeyote. Miongoni mwa hoja (madai) zao wanazotoa ni hizi zifuatazo;
(a) Mwenyezi Mungu hayupo kwa sababu haonekani
na wala hadirikiki kwenye milango ya fahamu. Rejea Qur’an(17:90-92).
Milango ya fahamu kama vile macho
katika kumuona, pua katika kumnusa, masikio
katika kumsikia, ngozi katika kumhisi au
kumgusa pia, n.k.
Udhaifu wa hoja hii,
Milango ya fahamu ina udhaifu mwingi sana na kikomo
pia, kama vile macho au pua huweza kuona au kunusa vitu vilivyo karibu tu na
visivyokuwa na kizuizi, kuna vitu vingi vinavyotuzunguka lakini hatuvioni kama
upepo, sauti, n.k.
(b) Mwenyezi Mungu amefanywa kuwepo na wanadamu
kutokana fikra na mawazo duni na uduni wa maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Hii ni baada ya mwanaadamu kushindwa kutatua
matatizo katika mazingira yake na hivyo kuibukia kujiundia miungu.
Udhaifu wa hoja hii,
Historia inaonyesha kuwa hakuna zama mwanaadamu
aliishi bila ya ujuzi wa kukabiliana na mazingira yake, Mwanaadamu wa kwanza
kuumbwa alipewa ujuzi (elimu) ya kukabilana na mazingira yake na hatimaye
kushushiwa muongozo kamili wa maisha kutoka kwa Muumba wake. Rejea Qur’an(2:31,38).
(c) Hapana Mungu Muumba bali vitu vyote
vimetokana na mabadiliko ya kimaada.
Wanadai kuwa maumbile na viumbe vyote vinatokana na
mabadiliko kidogo kidogo ya kimaada (evolution) baada ya muda mrefu kupita
kutoka hali moja kwenda nyingine. Mfano binaadamu kutoka pweza, mjusi, sokwe na
hatimaye mtu kamili.
Udhaifu wa hoja hii,
Nadharia hii haina ushahidi wowote wa kisayansi, kiuchunguzi na utafti
bali ni dhana tu aliyoibuni Darwin ili kupotosha uhalisia na ukweli juu ya
chanzo cha maumbile. Hadi leo hii hakuna mwanasayansi yeyote anayeweza
kuthibitisha nadharia hii.
(d) Kama Mungu Muumba yupo, ni ipi nasaba
(ukoo) yake au ametokana na nini?
Makafiri wa zamani na sasa wanasingizia kutoamini kuwepo Mungu kwa kuwa
hawajui nasaba, ukoo au asili yake anatokana na nani au na nini.
Udhaifu wa hoja hii,
Kwa kutumia mantiki, Muumba wa vitu vyote ndiye chanzo na asili ya vitu
vyote.Hivyo ni lazima asiwe na nasaba, mwanzo au mwisho pia. Na asitokane na
vitu au maumbile yale. Rejea Qur’an(112:1-4).
(e) Vitu havikuumbwa bali vimetokea kwa bahati
nasibu (by chance) na vitatoweka kwa bahati nasibu pia muda wake ukifika.
Makafiri wa zamani na sasa wanadai kuwa asili ya maumbile yote yametokana
na bahati nasibu (by chance), hivyo vitatoweka kama vilivyoibuka.
Udhaifu wa dai hili,
Hakuna uwezekano wa kuwepo maumbile bila ya Muumbaji na msimamizi mwenye
ujuzi na uwezo wa hali ya juu na mtegemewa wa kila kitu, kwani kila kitu kinachoonekana kimeumbwa na
kimewekwa kwa lengo maalum.
§
Kuamini
Mwenyezi Mungu Sio Suala La Kibubusa Au Kufuata Mkumbo.
Makafiri wanadai kuwa kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) ni ububusa
na kufuata mkumbo bila ya udadisi na kutumia akili. Dai hili sio la kweli kwa
sababu zifuatazo;
Kwanza, Mwenyezi Mungu (s.w) ametuma Mitume mbali mbali kwa
wanadamu ili kuwafundisha na kutoa dalili za kuwepo kwake bila ya shaka yeyote
kwa dalili za wazi ili kumfahamu na kuweza kumuabudu ipasavyo. Rejea Qur’an(4:165).
Pili, Vipawa, ufahamu na akili alivyopewa mwanaadamu ni
kumuwezesha kumtambua Muumba wake na kuweza kumuabudu inavyostahiki. Hivyo
kutotumia akili katika kumtambua Mwenyezi Mungu kupitia ishara mbali mbali ni
kustahiki adhabu. Rejea Qur’an(3:190),
(30:21), (7:179), (8:22) na (12:105).
Tatu, Mitume wa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwafundisha wafuasi
wao juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu, hawakuwataka kuamini na kufuata bila ya
hoja na dalili za wazi bali walionyesha ishara na miujiza kuthibitisha ujumbe
wao.
Nne, Msisitizo wa Elimu katika Qur’ankuwa faradhi ya kwanza
kama nyenzo pekee ya kumuwezesha mwanaadamu kumjua na kumuabudu Mola wake na
kuweza kuyamudu mazingira yanayomzunguka na kuweza kusimamisha Ukhalifa
ardhini.
Tano, Maana ya neno “imani” ambalo lina maana ya ‘kuwa na
yakini moyoni pasina shaka’ yeyote juu ya jambo fulani kwa kuwa na ujuzi nalo
na pia kupitia dalili na ishara za kutosha za kuonyesha kuwepo kwake.
§
Dalili Za
Kuwepo Mwenyezi Mungu (S.W).
Dalili nyingi zimedhihirishwa ndani ya Qur’ankatika maeneo makuu matano
ambamo uchunguzi wa kina na kutafakari vikifanyika vilivyo mtu atayakinisha
kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) pasina shaka yeyote. Maeneo hayo ni haya
yafuatayo;
1.
Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.
2.
Nafsi (Dhati) ya mwanaadamu.
3.
Historia ya mwanaadamu.
4.
Maisha ya mitume.
5.
Mafundisho ya mitume.
1. Umbile la Mbingu na Ardhi na Vyote Vilivyomo.
Maumbile mbali mbali kama vile udongo, milima, mabonde, maji, mimea,
wanyama, jua, mwezi, nyota, n.k ambavyo ni ishara kubwa inayoonyesha uwepo wa
Mwenyezi Mungu (s.w). Ishara hizo ni hizi zifuatazo;
(a) Umbile la Mbingu na Ardhi;
Tukichunguza maumbile mbali mbali ya dunia na sayari zote jinsi yalivyoundwa
na kupangika kwa namna iliyo maalum kama vile jua, mwezi, nyota, n.k ni ishara
tosha kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w). Rejea Qur’an(41:9-12), (7:54),
(32:4-5), (70:4), (21:30), (46:33) na (79:30).
(b) Jua, Mwezi na Nyota;
Kuwepo kwa mfumo wa ajabu uliopangika wa Jua, mwezi na Nyota na kila
kimoja kina njia yake pasina kutokea mgongano au mvurugano wa aina yeyote kati
yao ni ishara kubwa za kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w). Rejea Qur’an(6:96),
(7:54), (2:29), (10:5), (14:33).
(c) Usiku, Mchana, Mwanga na Giza;
Kupatikana na kubadilishana kwa usiku na mchana, mwanga na giza ni ishara
tosha za kuthibitisha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) kwa wenye akili. Rejea Qur’an(2:164),
(3:190), (17:12) na (28:71-72).
(d) Bahari, Maziwa na Mito;
Wingi wa maji yasiyo na mfano, kutofautiana ladha yake, na kutengana kati
ya maji matamu na chumvi bila ya kizuizi chochote na pia vyombo vizito na
vikubwa kupita juu yake bila kuzama ni dalili nyingine ya kuwepo Mwenyezi Mungu
(s.w). Rejea Qur’an(25:53), (2:264), (10:22), (14:32), (16:14), (17:66),
(22:65) na (53:12).
(e) Milima na Mabonde;
Milima, majabali na mabonde ambavyo vinaifanya ardhi iwe madhubuti na
isiyumbe wakati wa mitetemeko na
mzunguko kati ya jua, mwezi na nyota ni ishara kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu
(s.w). Rejea Qur’an(21:31), (13:3),
(15:9), (16:15), (27:61), (31:10), (50:7), (77:27), (35:27), (78:7) na (88:19).
(f)
Upepo, Mawingu, Mvua, Radi na Ngurumo;
Upepo, mawingu, radi, ngurumo na mvua ni vitu vinavyofanya kazi kwa
ushirikiano wa ajabu unaopelekea mvua kunyesha sehemu inayohitajika. Vyote hivi
ni dalili tosha juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w). Rejea Qur’an(10:22), (13:17), (2:19-20),
(2:164) na (25:48).
(g)
Matunda, Mimea na Vyakula (Riziki);
Mimea na matunda mbali mbali hustawi katika aina tofauti za udongo na
kutoa mazao ambayo ni riziki (chakula) kwa viumbe hai na kila kimoja
kinategemea kingine katika kustawi kwake. Hii ni ishara kwa wenye akili. Rejea Qur’an(67:21), (11:6), (29:60),
(6:95,99) na (13:4).
(h)
Wanyama, Ndege na Wadudu;
Viumbe vyote hivi kutokana na kutembea, kuruka kwao na kupata kwao riziki
bila ya wao kujipikia na kumiliki rasilimali yeyote, bado wanaishi bila shida
yeyote. Hii ni kuonyesha kuwa ni Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye pekee
anayewaruzuku. Rejea Qur’an(16:5-7),
(16:79) na (3:190-191).
2. Nafsi (Dhati) ya Mwanaadamu.
Kutokana na nafsi ya mwanaadamu mwenyewe tukichunguza na kutafakari kwa
makini kuna ishara nyingi zinazoonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) kama
ifuatavyo;
(a) Asili, Chanzo na mwisho wa
uhai wa mwanaadamu;
Uhai, hatua alizopitia na mfumo wa maisha ya mwanaadamu, vipi na lini
alianza atamaliza kuishi, nini sababu ya kifo chake na kitatokea wapi na nani
anayedhibiti maisha yake yote ya kila siku, tunadhibitisha kuwepo kwa Mwenyezi
Mungu (s.w). Rejea Qur’an(2:28), (30:20-21),
(22:5), (75:36-40), (23:14) na (56:81-87).
(b) Mwanaadamu kutofautiana na
Wanyama;
Wanaadamu kutofautiana na wanyama kimaumbile na kimalengo, ambapo lengo la
mwanaadamu ni kuwa Khalifah, na wanyama ni kumtumikia mwanaadamu. Mwanaadamu
amepewa akili, uhuru, vipawa na utambuzi kinyume na wanyama. Rejea Qur’an(2:29-30), (15:28-29), (95:4) na
(16:78).
(c) Kuumbwa wanaume na wanawake
na kuwa na mapenzi baina yao;
Asili ya wanaadamu wote ni moja, lakini wanatofautiana kimaumbile,
kihisia na kisaikolojia. Hii ni kwa ajili ya kutegemeana, kuhurumiana na
kuvumiliana kimahitaji kati yao kimwili na kisaikolojia. Zote hizi ni ishara
tosha za kuwepo Allah (s.w).
(d) Mwanaadamu kutofautiana
lugha, rangi, kabila na taifa;
Pamoja na wanaadamu kufanana katika viungo mbali mbali vya miili yao kama
ulimi, mdomo, koromeo, n.k lakini wanazungumza lugha tofauti bila ya kufunzwa
na mtu yeyote. Hii ni kuwa utofauti wao ni kwa ajili ya kujuana tu, na hii ni
dalili tosha.Rejea Qur’an(30:22) na(49:13).
(e) Kutofautiana vipaji na
riziki na mgawanyo wake miongoni mwa wanaadamu;
Vipaji vya wanadamu vimetofautiana mmoja na mwingine kama vile udaktari,
uhandisi, ualimu, n.k. pia upatikanaji wa riziki miongoni mwao ambao hautegemei
ujanja, fani au ujuzi wa mtu bali mgao maalum ili waweze kutegemeana. Rejea Qur’an(80:24-32).
(f) Ufanyaji kazi wa viungo vya
mwili wa mwanaadamu;
Myeyusho wa chakula, mfumo wa damu na ufanyaji kazi wa figo, mapafu, n.k
ni mashine za ajabu zisizohitaji utengenezaji na usimamizi wowote wa
kibinaadamu. Hii ni ishara kubwa juu ya uwepo Mtengenezaji Mjuzi na Mwenye
Hekima. Rejea Qur’an(30:30).
(g) Usingizi, Umbo, sura na vazi la mwanaadamu;
Umbo au sura aliyonayo mwanadamu hana uwezo wa kuibadilisha na anaridhika
nayo. Tofauti na wanyama wanaadamu wana mavazi ya kujisitiri uchi na kujikinga
na baridi na pia kupata usingizi pasina yeye kutaka au kujua chanzo na mwisho
wake. Rejea Qur’an(7:26), (82:6-8),
(95:4) na (45:4).
(h)
Mwanaadamu kumkumbuka Mwenyezi Mungu (s.w) wakati wa matatizo;
Wakati wa matatizo mwanaadamu ni mwepesi sana kurejea na kumkumbuka
Mwenyezi Mungu (s.w) na kuhitajia msaada wake, hata wale wanaokana kuwepo kwake
wanakiri uwepo wake bila ujanja. Hizi zote ni ishara za kuwepo kwake. Rejea Qur’an(6:63) na (10:90).
3. Historia ya Maisha ya Mwanaadamu.
Mchakato wa maisha na historia ya mwanaadamu tangu zama za kale hadi zama
hizi umeambatana na matukio makubwa yaliyovunja na kusambaratisha falme na dola
mbali mbali zilizotikisha dunia vita na majeshi. Yafuatayo ni baadhi tu ya
matukio hayo;
(a) Kuangamizwa watu wa (kaumu
ya) Lut, Thamud, Ad na Firauni;
Pamoja na nguvu kubwa za kijeshi na ulinzi imara waliokuwa nao watu hawa,
haikuwa chochote ilipofika muda wa kuangamizwa kwao. Mwenyezi Mungu mwenye
nguvu zisizokifani aliwafutilia mbali kwa kutumia majeshi yake ya upepo, maji,
n.k. Rejea Qur’an(89:6-13), (30:9),
(20:128) na (22:45-46).
(b) Kuangamizwa
kwa jeshi la Abraha, Gavana wa Yemen;
Abraha aliandaa jeshi kubwa la askari na tembo waliofunzwa barabara kwa
ajili ya kwenda kuibomoa Al-Ka’abah (Nyumba Tukufu ya Makka), lakini
alisambaratishwa na jeshi dogo na dhaifu kabisa la ndege, na hatimaye ikawa
ndio mwisho wao. Rejea Qur’an(105:1-5).
(c) Kufutika na kutoweka
Viongozi na Wafalme maarufu Duniani;
Viongozi na wafalme wengi waliowahi kuitawala na kuitikisa dunia na
kusababisa uharibifu, mauaji, kutokana nguvu kubwa ya kijeshi waliokuwa nayo na
hata wengine kufanywa miungu. Mfano akina Hitler, Mussolini na wengineo ambao
mwisho wao walifutika duniani na kushindwa kujinusuru pamoja na majeshi
yao.Rejea Qur’an(56:81-87) na (67:20).
4. Maisha ya Mitume;
Kwa kuzingatia maisha ya mitume hasa waliobainisha nadni ya Qur’an, jinsi
walivyofikisha ujumbe kwa watu wao kinadharia na kimatendo ni ishara tosha juu
ya uwepo wa Allah (s.w). Baadhi ya mambo hayo ni haya yafuatayo;
(a) Kuwepo na kujieleza kwao
kwa watu wao kuwa wao ni mitume wa Allah (s.w);
Mitume wote walithibitisha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w), na vile vile wote
walitoa dai lilelile la kuwa wao ni mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w) ijapokuwa
walikuja nyakati na sehemu tofauti. Rejea
Qur’an(7:59-61), (7:65-67), (16:36), (40:78) na (35:24).
(b)
Mwenendo wao mwema kutoathiriwa na mazingira ya jamii;
Mitume wengi walizaliwa na kulelewa katika jamii za kijahili, kishirikina
na kuabudu masanamu, lakini na walikuwa na mienendo na tabia nzuri isiyo kuwa
na mfano katika jamii husika. Hii ni ishara kuwa yupo Mlezi na Mjuzi, naye ni
Allah (s.w). Rejea Qur’an(57:25).
(c) Miujiza kuthibitisha utume
wao;
Mitume walikuja na miujiza tofauti tofauti ya kuthibitisha utume wao kwa
watu wao. Kila mtume alikuja na miujiza kutoka kwa Allah (s.w) kama ishara ya
kufikisha ujumbe kwa watu wake iliyokuwa tofauti na uchawi, viini macho na
mazingaumbwe. Rejea Qur’an(57:25),
(28:29-32), (5:110), (15:9) na (4:82).
(d) Kuhimili na kujitoa kwao
muhanga;
Mitume walikuwa wavumilivu na wenye subira dhidi ya mateso, kupigwa,
kufungwa gerezani, kutiwa kizuizini au kuuawa na kupata madhila, lakini hawa
kukata tama na kufikisha ujumbe wao. Hii ni yupo alikuwa anawaliwaza, naye ni
Allah (s.w). Rejea Qur’an(3:21), (3:181), (4:157-158), (21:69) na (59:8).
(e) Ujasiri wa mitume mbele ya
viongozi na jamii za kishirikina;
Pamoja na vitisho na viburi vya wafalme na watawala wa kishirikina,
mitume hawakumchelea mtu yeyote katika kumfikishia ujumbe wao. Hii ni ishara
kuwa Mwenyezi Mungu ndiye waliokuwa wanamtegemea. Rejea Qur’an(19:42-46) na (21:57-67).
(f)
Ushindi wa mitume dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu (s.w);
Mitume na wafuasi wao walikuwa wachache, dhaifu na wanyonge mbele ya
maadui wa Allah (s.w) waliokuwa wengi na wenye nguvu, lakini katika mapambano
mitume na wafuasi wao ndio waliopata ushindi kwa msaada kutoka kwa Allah (s.w).
Rejea Qur’an(71:25), (7:72), (26:60-68) na (8:9-10).
(g) Mitume kutohitaji malipo
kutoka kwa watu wao;
Mitume walifanya kazi ngumu na nzito bila ya kuhitajia malipo yeyote
kutoka kwa watu wao kinyume na viongozi wengi ambao huhitajia malipo kwa jamii
zao. Mitume walikuwa na uhakika wa kupata ujira tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu
(s.w) pekee. Rejea Qur’an(26:127).
5. Mafundisho ya Mitume.
Hili ni eneo jingine linaloonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) katika
vipengele vifuatavyo;
(a) Umoja wa ujumbe wa mitume;
Mitume walitumwa sehemu na nyakati tofauti lakini ujumbe wao ulifanana,
kila mtume alifundisha Tawhiid, lengo la kuumbwa kwao, kuwahofisha na adhabu na
kuwabashiria malipo mema pia. Hii ni kuwa ujumbe wao ulitoka kwa Allah (s.w). Rejea Qur’an(7:59, 65, 73, 85, 158), (16:36)
na (19:36).
(b)
Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira;
Mitume karibu wote walitokea katika jamii za kishirikina na kijahili,
lakini kamwe hawakuwahi kuchanganya mafundisho yao na utamaduni wa kijahili
hata kama jamii nzima ilisimama dhidi yao.
Rejea Qur’an(109:1-6).
(c) Upeo wa Elimu waliokuwa nayo
Mitume;
Mitume walikuwa na upeo, fikra na hekima ya hali juu katika kutatua na
kuendea mambo kuliko mtu yeyote katika jamii zao, japokuwa hawakupitia vyuo au
taasisi zozote za elimu. Hii ni dalili kuwa ni Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye
aliyewafunza. Rejea Qur’an(34:10-12),
(27:15-19), (43:2-3) na (25:53).
§ Athari za Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w)
katika maisha ya kila siku.
Muumini wa kweli huishi katika kila kipengele cha maisha yake kwa mujibu
wa taratibu na kanuni alizoweka Mwenyezi Mungu (s.w), na hii kama ifuatavyo;
(i)
Kupata ukombozi kutokana na utumwa wa aina
zote;
Huu hupatikana baada ya mtu kuwa huru na kuishi kwa kufuata taratibu na
kanuni alizoweka Mwenyezi Mungu (s.w) pekee.
Rejea Qur’an(12:39).
(ii)
Mwanaadamu huwa mwadilifu katika utendaji wa maisha yake ya kila siku;
Muumini wa kweli hufanya mem[a na kuepuka maovu bila hata ya kusimamiwa
au kuonekana na watu, kwa kujua kuwa mjuzi pekee
ni Mwenyezi Mungu (s.w). Rejea Qur’an(50:16).
(iii) Humfanya mwanaadamu kuwa
mpole, mvumilivu na mwenye huruma;
Mwanaadamu huwa mpole hasa kwa wenye shida na matatizo na pia kuwa na
subra anapofikwa na mitihani na kujiepusha na kibri, majivuno na kujiona. Rejea Qur’an(6:165).
(iv)
Humfanya mja kuwa jasiri katika kusimamia haki, uadilifu na usawa katika
jamii;
Muumini wa kweli huwa shujaa katika kupambana na dhulma na ukandamizaji
wa aina yeyote na kupigania haki bila kumchelea mtu yeyote. Rejea Qur’an(4:74), (5:45) na (9:111).
(v) Humfanya mja kuwa na mtazamo
mpana na sahihi juu ya maisha;
Muumini wa kweli kamwe hawi na fikra na mtazamo finyu katika kuyaendea
maisha yake ya kila siku kwa kujua lengo, thamani na nafasi yake juu ya maisha ya
Akhera. Rejea Qur’an(15:9).
(vi) Humuwezesha mja kuwa mwenye kukinai na kutosheka;
Muumini wa kweli hutosheka na kuridhika na kile alichokadiriwa na
Mwenyezi Mungu (s.w) iwe kwa kupungukiwa au kuzidishiwa, yote kwake anashukuru.
2.2. Shirk.
·
Maana : Shirk
ni kinyume cha Upweke au Umoja (Tawhiid)
·
Maana ya
Kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w):
Ni kujaalia kinadharia au kiutendaji kuwa kuna miungu wengine
wanaoshirikiana na Mwenyezi Mungu (s.w) katika kuongoza na kuendesha Ulimwengu.
§ Aina za Shirk.
Kuna aina kuu nne za shirk,
1.
Shirk katika Dhati ya Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy Dhaat).
2.
Shirk katika Sifa za Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy
Sifaat).
3.
Shirk katika Mamlaka ya Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy
Ikhtiyaar).
4.
Shirk katika Hukumu za Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy
Ah-kaam).
1. Shirk
katika Dhati ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Ni kujaalia au kuvinasibisha viumbe na uungu kwa kuvipa majina rasmi kama
washirika wa Mwenyezi Mungu (s.w) na kuviendea kwa unyenyekevu na ibada maalum
kama, kuvisujudia, kuchinja na kuviomba msaada. Rejea Qur’an(25:2-3), (22:73) na (29:41).
2. Shirk katika Sifa za Mwenyezi
Mungu (s.w).
Ni kuwasifu au kuwatukuza viumbe kiwango anachostahiki kusifiwa au
kutukuzwa Allah (s.w) peke yake. Kama kuomba dua, baraka na msaada kupitia kwa
Wacha-Mungu, mfano kwa baraka za Mtume, Abdul-Qadir, Sharifu au Sheikh fulani
n.k.Rejea Qur’an(53:32), (10:62-64), (2:180), (17:110) na (40:60).
3. Shirk katika Mamlaka ya
Mwenyezi Mungu (s.w).
Ni kuwakabidhi viumbe mamlaka kamili ya Mwenyezi Mungu (s.w) na kuwatii
kwayo kama vile kuongoza, kulisha, kulea, kulinda n.k katika maisha ya kila
siku kinyume na nafasi au uwezo wao. Rejea
Qur’an(9:31) na (2:208).
4. Shirk katika Hukumu za Mwenyezi Mungu (s.w).
Ni kutunga sheria au hukumu kinyume na sheria au hukumu za Mwenyezi Mungu
(s.w) alizoziainisha katika vitabu vyake vitukufu na kuzitumia kuhukumu kwazo
katika uendeshaji wa maisha ya kila siku.
Rejea Qur’an(5:38), (24:2), (33:36), (5:44-45, 47) na (5:50).
§
Kina cha
Uovu wa Shirk.
o
Ni dhulma kubwa kuliko zote na ndio chanzo cha matatizo
yote ulimwenguni.
Rejea Qur’an(31:13) na (10:35-36).
o
Ni dhambi kubwa kuliko zote isiyosameheka ila
apende Mwenyezi Mungu (s.w) na kutubia kikweli kweli kabla ya kufa.
o
Ni dhambi inayofuta mema yote ya mtu
aliyoyafanya kabla ya kushirikisha.
Rejea Qur’an(4:48), (4:116) na (39:65).
§ Maana ya Kumuamini Mwenyezi Mungu(s.w)
katika maisha ya kila siku.
Ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kufuata barabara mwongozo wake
katika utendaji wa wetu wa kila kipengele cha maisha yetu ya kila siku kwa
kufanya moja kati ya mambo yafuatayo;
o
Kusimamisha Tawhiid (Umoja na Upweke wa Mwenyezi
Mungu) na
o
Kujiepusha na Shirk za aina zote.
§
Tawhiid.
o
Kimaana: Ni Umoja au Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w).
o
Kimatumizi: Ni fikra, mtazamo wa kimapinduzi katika
kumkomboa
mwanaadamu na aina zote za utumwa wa kibinaadamu na kuwa mtumishi huru wa Muumba wake.
§
Aina za
Tawhiid.
Kuna aina kuu tatu za Tawhiid kama zilivyoainishwa
katika aya za Qur’an.
(i) Tawhid Al-Uluuhiyyah – Upweke wa Allah (s.w) katika Uungu wake.
Nayo ni Kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) katika Uungu wake kwa kutokuwa
na mungu mwingine yeyote wa kumuelekea kwa ibada au maombi isipokuwa yeye peke
yake. Rejea Qur’an (2:163), (3:62) na (112:1-4).
(ii) Tawhiid Al-Asmaa Wassifaat – Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w) katika Majina na Sifa.
Nayo ni kutomsifu Mwenyezi Mungu (s.w) kwa sifa za viumbe au majina ya
viumbe na pia kutomsifu kiumbe yeyote kwa sifa za Mwenyezi Mungu (s.w).Rejea Qur’an(57:1-6)
na (59:22-24).
(iii)
Tawhiid Rabbuubiyya, Upweke wa Mwenyezi
Mungu (s.w) katika Ubwana,Utawala na Mamlaka Yake.
Kumpwekesha Allah (s.w) katika Ubwana na Utawala wake ni kutofuata na
sheria na taratibu za maisha kinyume na zile alizoziweka yeye kwa kumfanya
ndiye Mlezi, Mlinzi, Mwendeshaji wa kila kitu.
Rejea Qur’an(4:59), (31:14-15), (25:52), (3:149), (3:100) na (5:57).
2.2. Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu (s.w).
·
Maana: Malaika
ni viumbe walioumbwa kutokana na nuru.
·
Sifa za
Malaika:
- Ni viumbe wa kiroho wenye mabawa.
- Ni viumbe wasio na matashi
ya kimwili (kula, kunywa, kulala, n.k.)
- Hawana hiari katika
kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w).
- Ni vimbe wasio na jinsia.
- Ni viumbe walioumbwa
kutokana na Nuru.
§ Kazi za Malaika.
Zifuatazo ni baadhi tu ya kazi za
baadhi ya Malaika.
(a)
Kuleta Wahyi (ujumbe) kwa wanaadamu kutoka
kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Malaika Jibril ndiye mhusika
mkuu wa kupeleka wahyi kwa mitume na manabii.
Rejea Qur’an(81:19-20), (16:2) na (11:69-73).
(b)
Kumchunga na Kumlinda kila mtu na kuandika
amali zake nzuri na mbaya.
Kila mtu anakundi la malaika nyuma na mbele yake kumlinda na mambo yaliyo
nje na uwezo wake. Pia kuna malaika wa kulia anayeandika mema na wa kushoto
anayeandika maovu ya mtu. Rejea Qur’an(82:1-12),
(50:17-18) na (13:11).
(c)
Kuwaombea Waumini maghufira kwa Mwenyezi
Mungu (s.w).
Hawa ni malaika ambao huzunguka katika makundi ya waumini anapotajwa
ndani yake Mwenyezi Mungu (s.w) au kusomwa Qur’anTukufu. Rejea Qur’an(40:7),
(42:5) na (17:78).
(d)
Kuwasaidia waumini katika vita vya kupambana
na maadui wa Allah (s.w).
Pindi waumini wanapopigana katika kusimamisha haki, Mwenyezi Mungu (s.w)
huteremsha malaika kuwasaidia. Rejea Qur’an(3:123-126)
na (8:12).
(e)
Kuwaangamiza watu waovu waliopindukia
mipaka.
Watu waovu waliopindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu (s.w) wakaonywa muda
mrefu na wasionyeke huangamizwa na malaika maalum. Rejea Qur’an(11:81-83).
(f)
Kutoa roho za viumbe.
Malakul-Maut ndiye mhusika mkuu
na wengineo katika kutoa roho za viumbe. Rejea Qur’an(32:11).
(g)
Kuzihoji, kuzistarehesha au kuziadhibu roho
za wafu kaburini.
Malaika wanaohusika na kazi hii ni Munkar
na Nakir.
(h)
Kupuliza Parapanda siku ya Qiyama.
Mipulizo ya Parapanda katika kufisha na kufufua viumbe siku ya Qiyama
itafanywa na malaika Israfil. Rejea Qur’an(39:68).
(i)
Kuwaliwaza na kuwakaribisha watu wema
peponi.
Hili kundi jingine la malaika watakaofanya kazi hiyo siku ya Qiyama. Rejea
Qur’an(41:30-32) na (39:73).
(j)
Kuwasimanga na kuwaadhibu watu waovu motoni.
Kuna kundi la malaika watakaokuwa wanaadhibu watu waovu motoni. Mlinzi
mkuu wa milango ya moto ni Malaika Maalik. Rejea Qur’an(25:22), (74:26-30) na (43:77).
(k)
Kumtukuza na kumsifu Mwenyezi Mungu (s.w).
Kuna kundi la malaika maalum kwa kazi hii tu. Rejea Qur’an(40:7).
§ Maana ya Kuamini Malaika katika maisha ya
kila siku.
Zifuatazo
ni athari za muumini wa kweli juu ya imani ya malaika katika kila kipengele cha
maisha ya kila siku;
Kwanza, imani ya kweli juu ya Malaika humuepusha na
kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w) na viumbe wake hasa wale wasioonekana kama
Malaika, majini, n.k.
Rejea Qur’an(37:149-154), (43:16-19) na (21:26-27).
Pili, imani juu ya malaika huchochea mja kufanya ibada kwa
bidii na kujiepusha na maovu na machafu ili kupata cheo kama malaika au zaidi.
Tatu, imani juu ya malaika pia humfanya mtu kuepuka kufanya
maovu popote alipo na muda wowote kwa kujua kuwa yupo pamoja na malaik?a.
Nne, Mja anapoamini kuwa malaika huandika na kuhudhurisha
vitendo vyake kwa Mwenyezi Mungu (s.w), hufanya bidii katika kufanya mema zaidi
na kuepuka maovu kadri ya uwezo wake.
Tano, Muumini anapoamini kuwa malaika humuombea maghufira kwa
Mwenyezi Mungu (s.w), hufanya bidii katika kuzidisha mema na kuepuka maovu
kadri awezavyo ili kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu (s.w) zaidi. Rejea Qur’an(17:13-14) na (18:49).
2.3. Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w)
§
Vitabu
vya Mwenyezi Mungu vilivyotajwa ndani ya Qur’anni;
1.
Suhufi – aliteremshiwa Nabii Ibrahim (a.s) na Nabii
Musa (a.s).
2.
Taurat – aliyoteremshiwa Nabii Musa (a.s)
3.
Zaburi – aliyoteremshiwa Nabii Daud (a.s)
4.
Injili – aliyoteremshiwa Nabii Isa (a.s) na
5.
Qur’an– aliyoteremshiwa Nabii au Mtume Muhammad
(s.a.w).
6.
§ Tofauti kati ya Qur’anna Vitabu vingine vya
Mwenyezi Mungu (s.w).
|
Kitabu cha Qur’an |
Vitabu Vingine vya Mwenyezi Mungu |
|
1. Neno la Asili. Qur’animebakia
katika lugha yake ya asili ya kiarabu fasaha pamoja
nakutafsiriwa katika lugha tofauti. |
Vitabu vingine
lugha zao za asili
zilizoshushiwa zimepotea na kutojulikana. |
|
2. Lugha
zilizoshushiwa Vitabu. Lugha ya Qur’anni
hai kwani mpaka leo inatumika na kufahamika na walimwengu wengi. |
Lugha za vitabu
vilivyotangulia ni mfu, zimefutika zamani na hazijulikani na watu. Rejea Qur’an(14:4). |
|
3.
Kuhifadhiwa na Kulindwa Vitabu. Qur’animebaki
katika asili yake kama ilivyoteremsha bila kubadilishwa chochote na wanaadamu
ndani yake. Rejea Qur’an(15:9)
na (41:42) |
Vitabu vingine
vimepotea katika asili yake kwa kupunguzwa, kuongezwa na kupotoshwa asili ya
ujumbe wake na mikono ya wanaadamu.. |
|
4.
Hitoria ya Kushushwa Vitabu. Historia ya
kushushwa Qur’aninajulikana vyema mfano; namna, sehemu, muda/kipindi na
sababu ya kuteremshwa kila aya. |
Vitabu vingine
historia ya kushushwa kwao haijulikani, mfano; muda, nama, sababu au sehemu. |
§ Lengo la kushushwa Vitabu vya Mwenyezi
Mungu (s.w).
Ni kuwa mwongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu katika kufuata maamrisho
na kuacha makatazo yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) hapa ulimwenguni. Rejea Qur’an(2:38-39), (2:185) na (5:44).
§ Maana ya Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu
(s.w) katika maisha ya kila siku.
Waumini wa kweli wa vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w) ni wale wanaoendesha
kila kipengele cha maisha yao ya kila siku kwa mujibu wa mwongozo uliopo katika
vitabu hivyo.
§ Sababu za kutokubalika Vitabu vilivyotangulia
kuwa Mwongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu zama hizi.
1.
Vitabu vilivyotangulia vimeingiliwa na mikono na
matashi ya wanaadamu kiasi cha kupoteza au kupotoshwa ujumbe wake wa asili.
2.
Lugha ya vitabu vilivyotangulia imetoweka na kusahaulika
duniani kiasi kwamba hata kingelikuwapo kimojawapo katika lugha yake asili,
ujumbe wake usingelifahamika kwa watu.
3.
Vitabu vilivyotangulia vilikuwa ni mwongozo kwa watu
maalum na kwa wakati maalum tu, havikuwa mwongozo kwa walimwengu wote na
nyakati zote.
§ Sababu za Qur’ankuwa mwongozo sahihi pekee
wa maisha ya mwanaadamu.
§ Qur’anyote
ni maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake, hivyo ni mwongozo wa uhakika.
§ Ujumbe
wa Qur’anumeelekezwa kwa walimwengu wote na zama zote zilizobakia hadi siku ya
Qiyama.
§ Maana ya Kuiamini Qur’ankatika maisha ya
kila siku.
Maana halisi ya kuiamini Qur’ankama Kitabu pekee cha mwongozo sahihi wa
maisha ya mwanaadamu (muumini) ni kufanya yafuatayo;
i.
Kuwa na yakini pasina shaka yeyote kuwa Qur’anyote ni
maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake.
Rejea Qur’an(2:2).
ii.
Kuufahamu vyema ujumbe wa Qur’anna kuuheshimu
inavyostahiki kwa kujizatiti katika kujifunza kuisoma na kuijua ipasavyo. Rejea Qur’an(73:4) na (7:204-205).
iii.
Kulifahamu vyema lengo la Qur’anna kuiendea kwa lengo
lake tu.Rejea Qur’an(14:1), (2:185) na (16:64).
iv.
Kuitekeleza Qur’ankatika kukiendea kila kipengele cha
maisha yetu ya kila siku kwa mujibu wa lengo lake tu. Rejea Qur’an(5:44, 46-47).
3. MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA IBADA
3.1 Dhana ya Ibada kwa
Mtazamo wa Uislamu.
-
Ibada – Ni neno la Kiarabu linalotokana na neno ‘Abd’ lenye maana ya mtumwa au
Mtumishi.
-
Kumtimikia Allah (s.w) kikweli kweli ni kufanya kila
analoliridhia Allah (s.w).
-
Kuzingatia na kufuata amri zake zote kwa kuchunga
mipaka yake katika maisha ya kila siku.
3.2 Lengo la Ibada
Maalum.
- Ibada maalumu kama vile; swala,
funga, zaka, hija, na sunnah zake ni kumuandaa mja
kuweza kumuabudu na kumtumikia
Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo kwa kila
kipengele
cha maisha ya kila siku kibinafsi na kijamii.
-
Ibada maalumu zimekusudiwa kumuandaa mja kufikia lengo la kuumbwa kwake.
Rejea Qur’an
(51:56),
(2:30).
4. NGUZO ZA UISLAMU.
4.1. Maana ya Shahada.
Shahada mbili ndio nguzo ya kwanza ya Uislamu na ndio kiingilio cha mtu
katika Uislamu kwa kuyakinishwa moyoni, kutamkwa kinywani na kuthibitishwa kwa
vitendo.Rejea Qur’an(41:30-31), (2:8) na (33:40).
4.2. Maana ya
Kusimamisha Swala.
Ni kuswali kwa kutekeleza kikamilifu nguzo, sharti zote za swala na kuwa
na unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.
§
Nafasi na
Umuhimu wa Kusimamisha Swala katika Uislamu.
Swala imesisitizwa na ina umuhimu katika Uislamu kwa sababu zifuatazo;
i.
Kusimamisha Swala ni Amri ya Mwenyezi Mungu
(s.w).
Mwenyezi Mungu (s.w) ameamrisha waumini (waislamu) wote wasimamishe swala
zote za faradh na sunnah ipasavyo.Rejea Qur’an(29:45),(4:103) na (14:31).
ii.
Kusimamisha swala ni nguzo ya Pili ya
Uislamu.
Baada ya shahada mbili, nguzo ya pili na ya msingi mno katika Uislamu ni
kusimamisha swala.
iii.
Swala humtakasa muislamu na mambo machafu na
maovu.
Bila shaka swala ikiswaliwa vilivyo humuepusha mja na mambo machafu na
maovu.
Rejea Qur’an(29:45).
iv.
Swala ni amali ya mwanzo kabisa kuhesabiwa
siku ya Qiyama.
Swala ya muumini ikitengemaa vizuri ndio sababu ya kufaulu kwake Duniani
na Akhera pia. Rejea Qur’an(23:1-2,9),
(87:14-15) na (22:34-35).
v.
Kutosimamisha swala ni sababu ya mtu
kuingizwa motoni.
Hii ni baada ya muislamu Kupuuza swala kwa kutozingatia sharti na nguzo
zake kikamilifu na kukosa unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.Rejea Qur’an(74:42-47),
(68:42-43) na (107:4-5).
§
Lengo la
Kusimamisha Swala.
Lengo kuu la kusimamisha swala ni kumkinga mja na mambo machafu na maovu
kwa kutekeleza kikamilifu sharti, nguzo na sunnah za swala pamoja na kuwa na
khushui ndani ya swala kama ifuatavyo;
i.
Swala inamtakasa mja kwa kuzingatia na kutekeleza
sharti zake zote kikamilifu ambazo ni kuwa twahara, sitara (kujisitiri),
kuchunga wakati wa swala na kuelekea Qibla.
ii.
Swala inamtakasa
mja kwa kutekeleza kikamilifu nguzo na sunnah za swala kama kumsifu na
kumtukuza Mwenyezi Mungu (s.w), kusoma Qur’an, kutoa ahadi ya kujisalimisha kwa
Mwenyezi Mungu (s.w), kuomba dua na kutekeleza vitendo vyote vya swala.
§
Faida
(matunda) ya kusimamisha swala katika jamii.
Swala za faradhi zikisimamishwa vilivyo faida zifuatazo hupatikana katika
jamii;
i.
Usafi na
unadhifu wa mwili.
Kwani muislamu hawezi kuswali mpaka ahakikishe kuwa msafi (twahara)
kikamilifu katika nguo na mwili pia na sehemu ya kuswalia. Rejea Qur’an(7:31).
ii.
Utakaso wa
Nafsi.
Kwa kutekeleza sharti na nguzo za swala pamoja na mnyenyekevu katika
swala, hupelekea mja kuwa mtiifu ipasavyo kwa Mola wake muda wote.
iii.
Swala za
jamaa huimarisha udugu, umoja na usawa.
Kuswali katika jamaa huleta udugu, umoja na usawa wa kweli na kuepusha
mfarakano, chuki na ubaguzi miongoni mwa waislamu. Rejea Qur’an(49:10,13).
iv.
Swala za
jamaa huwafunza waislamu uongozi bora.
Swala huongozwa na imamu (kiongozi) wa waumini husika anayetokana na wao
kutokana na sifa maalumu za kuwa kiongozi.
§
Kwa nini
Wengi wanaoswali hawafikii Lengo la Swala?
Miongoni mwa sababu ya wengi kutofikia malengo ya swala zao ingawa
wanaziswali misikitini tena kwa jamaa ni;
1.
Hawajui lengo halisi la swala.
Waislamu wengi huswali kwa lengo la kufutiwa madhambi na kupata thawabu
na sio kuepukana na machafu na maovu, ambalo ndio lengo kuu la swala. Kupata
thawabu na kufutiwa madhambi ni matunda ya swala. Rejea Qur’an(29:45) na (72:23).
2.
Waislamu wengi hawana ujuzi halisi juu ya
swala.
Pamoja na waislamu wengi kutekeleza swala zao kwa jamaa lakini wengi wao
hawajui kabisa miiko, sharti na nguzo za swala ila wanafuata mkumbo tu.Rejea Qur’an(7:205),
(7:55) na (4:142).
3.
Waislamu wengi hawahifadhi swala zao.
Pamoja na kuswali kwao bado wengi hawazingatii na kutekeleza kikamilifu
sharti na nguzo za swala zao inavyotakiwa.Rejea Qur’an(107:4-5) na (23:1,8).
4.
Wengi hawaswali kwa Unyenyekevu swala zao.
Kukosa unyenyekevu (utulivu wa mwili, fikra na uzingativu) hupelekea
mwenye kuswali kutofikia lengo na matunda ya swala.RejeaQur’an(29:45),(23:1-2)
na(23:10-11).
5.
Kutosimamisha Swala za jamaa ipasavyo.
Waislamu wengi hawaswali jamaa misikitini au hawazingatia sharti za swala
ya jamaa kama kunyoosha safu ipasavyo, kugusanisha mabega, vidole, n.k. Rejea Qur’an(23:1-2).
4.3.
Kutoa Zakat.
§
Umuhimu
wa Zakat na Sadakat katika Uislamu.
i.
Zakat ni nguzo ya tatu ya Uislamu.
Baada ya shahada mbili na kusimamisha swala nguzo muhimu sana katika
uislamu ni kutoa zakat kama ilivyoainishwa katika hadithi.
ii.
Kutoa zakat na Sadaka ni amri ya Mwenyezi
Mungu (s.w).
Kutoa zaka na vile tulivyoruzukiwa katika mali na huduma au misaada mbali
mbali ni wajibu kwa waislamu wanaovimudu.Rejea Qur’an(14:31) na (2:254).
iii.
Kutoa Zakat ndio kitambulisho cha Uislamu na
Ucha-Mungu wa mtu.
Muislamu akiacha au kukataa kutoa zakat kwa makusudi ni ishara ya
kuritadi na kutoka katika Uislamu. Rejea
Qur’an(9:11) na (2:2-3).
iv.
Kutoa Zakat na sadaka ni sababu ya mtu
kufaulu Duniani na Akhera.
Miongoni mwa sifa za waumini na wacha-Mungu ni kutoa katika vile
walivyoruzukiwa na muumba wao.Rejea Qur’an(2:2-3),
(23:1-4), (22:34-45) na (2:262,274).
v.
Kutotoa Zakat na Sadaka ni sababu ya
kuangamia mtu Duniani na Akhera.
Kutotoa katika vile tulivyoruzukiwa hupelekea mtu kustahiki adhabu hapa
Duniani na Akhera pia. Rejea Qur’an(9:34-35),
(92:8-10) na (3:180).
§
Namna
lengo la zakat linavyofikiwa.
Zakat na sadaka zinalengo la kutakasa mali na nafsi ya mtoaji na mpokeaji
kama ifuatavyo;
i.
Zakat na sadaka inavyotakasa mali ya mtoaji.
Zakat hutolewa 2.5% ya mali na kuwapa wanaostahiki, hivyo kuitakasa mali
ya mtoaji kutokana na chumo la haramu na haki za watu.
ii.
Zakat na sadaka zinavyotakasa nafsi ya
mtoaji.
Utoaji mali kwa wanaostahiki huitakasa nafsi ya mtoaji kutokana na
ubakhili, kuabudu mali, kibri, n.k katika kumiliki mali na kuwa na upole,
huruma, n.k.
Rejea Qur’an(61:10-12) na (9:102-103).
iii.
Zakat na sadaka inavyotakasa nafsi ya
mpokeaji.
Utoaji wa zaka na sadaka kwa wanaostahiki huondoa chuki, husuda, uadui,
unyonge kwa wasionacho na kuleta udugu, upendo, shukurani na ushirikiano. Rejea Qur’an(9:60).
iv.
Zakat na sadakat huitakasa jamii ya
waislamu.
Utoaji wa zakat na sadaka hujenga jamii yenye udugu
wa kweli, kujenga uchumi wa halali na kuondoa chuki na uadui baina ya masikini
na matajiri. Rejea Qur’an(61:4).
§
Kwa nini
lengo la Zakat na Sadaka halifikiwi katika jamii yetu?
Pamoja na zakat na sadaka kutolewa na baadhi ya waislamu lakini malengo
yake hayafikiwi, zifuatazo ni baadhi ya sababu;
i.
Wengi watoao zakat na sadakat hawajui lengo
lake halisi.
Waislamu wengi wanatoa zaka na sadaka kwa lengo la kupata thawabu na
kufutiwa madhambi tu na sio utakaso.
ii.
Waislamu wengi hawatoi zakat kabisa.
Waislamu wengi licha ya kuwa na mali na uwezo wa kutoa zakat na sadaka
lakini hawatekelezi au kuhimiza wengine katika kutoa mali zao pia. Rejea Qur’an(2:2-3).
iii.
Wengi watoao zakat na sadakat hawatekelezi
masharti ya utoaji.
Pamoja na matajiri wachache kutoa zakat na sadaka, lakini bado hutoa kwa
ria, masimbulizi,adha na kuleta uadui na fitna katika jamii.Rejea Qur’an(2:264).
iv.
Zakat na sadaka haikusanywi na kugawanywa
kijamii.
Utoaji na ugawaji wa zakat na sadaka umekuwa unafanywa kila mtu kivyake,
bila mpango maalumu wa kukusanya na kugawa kwa wanaostahiki.
v.
Wengi watoao zakat na sadakat chumo lao ni
la haramu.
Ingawa waislamu wengi hutoa zakat na sadaka, lakini lengo na matunda yake
hayafikiwi kutokana na chumo lao kuwa haramu.
4.4.
Saumu (Funga).
§
Umuhimu
wa swaumu (Funga) katika Uislamu.
i.
Funga ya mwezi wa Ramadhani ni nguzo ya nne
katika Uislamu.
Funga ya mwezi wa Ramadhani ni faradhi kwa waislamu wote
na ni miongoni mwa nguzo za Uislamu baada ya shahada, swala na zakat.Rejea Qur’an(2:183).
ii.
Kufunga mwezi wa Ramadhani ni utambulisho wa
Uislamu wa mtu.
Mtu akiacha nguzo hii kwa makusudi ni sababu na ishara
tosha ya kutoka katika Uislamu.
iii.
Kufunga mwezi wa Ramadhani ni utambulisho wa
Ucha-Mungu wa mtu.
Funga ya Ramadhani na sunnah zingine ni kielelezo cha Ucha-Mungu
wa muislamu zikitekelezwa vilivyo. Rejea
Qur’an(2:183).
iv.
Kutofunga mwezi wa Ramadhani makusudi
hupelekea kukosa msamaha.
Muislamu asipofunga mwezi wa Ramadhani makusudi basi,
hukosa msamaha, na rehma na hustahiki adhabu za Mwenyezi Mungu (s.w).
v.
Kufunga mwezi wa Ramadhani ni amri ya
Mwenyezi Mungu (s.w).
Kufunga mwezi wa Ramadhani ni faradhi (amri) kwa
waislamu wote isipokuwa wenye udhuru. Rejea
Qur’an(2:183).
§
Lengo la
Funga linavyofikiwa.
Lengo kuu la funga ni kumuandaa mja (muislamu) kuwa mcha-Mungu (2:183).
Na lengo hili hufikiwa kama ifuatavyo;
i.
Funga humzidishia mfungaji imani na
uadilifu.
Kufunga ni ibada ya siri, anayejua ni mfungaji na
Muumba wake tu, hivyo hufunga ili apate radhi na malipo kutoka kwa Mwenyezi
Mungu peke yake.
ii.
Funga humzidishia mja nidhamu na utii kwa
Mwenyezi Mungu (s.w).
Mja akiwa amefunga huwa mtiifu kwa kufuata amri na
kuacha makatazo ya Mwenyezi Mungu na kuchunga vilivyo masharti na nguzo zote za
funga.Rejea Qur’an(2:168) na (2:172).
iii.
Funga humzoesha mja kudhibiti matashi ya
nafsi na kimwili.
Funga humuepusha mja na tabia za kinyama kama kula,
kunywa, kujamii bila sababu ya msingi, na kumjenga kiroho na kiutu ili kuwa na
hadhi yake.Rejea Qur’an(25:43-44) na (2:30-31).
iv.
Funga humuwezesha mja kuwahurumia wanaadamu
wenzake.
Funga hujenga huruma na mapenzi kwa kule mfungaji
kukaa na njaa na adha yake, hivyo hujifunza kuwahurumia wasiokuwa nacho na
wenye matatizo. (34:12-13) na (49:13).
v.
Funga humpatia mfungaji afya (siha).
Kwa mfungaji kukaa na njaa muda mrefu, huuwezesha
mwili kupumzika na kuondoa malimbilkizo ya vyakula tumboni ambayo ni sumu
kwake.
vi.
Funga huwafanya Waislamu kuwa Ummah mmoja.
Hii ni kwa sababu funga imefaradhishwa kwa waislamu
wa rika na jinsia zote, maskini na matajiri pia, wote hutekeleza amri hii bila
ubaguzi wowote. Rejea Qur’an(49:13).
§
Faida za
Funga.
- Huleta
huruma, upendo na mapenzi baina ya wanajamii.
- Huleta utii na nidhamu
kwa mfungaji kwa Mola wake na wanaadamu pia.
- Huimarisha afya ya
mfungaji.
§
Kwa nini
Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji wengi?
Pamoja na waislamu wengi kujizatiti katika kufunga mwezi wa Ramadhani na
funga zingine za sunnah, lakini wengi wao hafikii lengo la funga kwa sababu
zifuatazo;
i.
Wengi wafungao hawajui lengo la funga.
Wafungaji wengi hufunga kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi
tu na sio kuwa wacha-Mungu kama lilivyo lengo la funga. Rejea Qur’an(2:183).
ii.
Wafungaji wengi chumo lao ni la haramu.
Waislamu wengi wafungao chakula chao, futari yao na daku zao zinatokana
na chumo la haramu ambalo ni sababu ya kutopata matunda ya funga zao.
iii.
Kutofahamika lengo la maisha na uhusiano na
lengo la funga.
Waislamu wengi hutekeleza ibada maalumu kama swala, funga, n.k na kuona
kuwa ndio lengo kuu la maisha yao na kuacha nyanja zingine za maisha yao. Rejea
Qur’an(51:56).
iv.
Wengi wafungao hawazingatii miiko na sharti
za funga zao.
Waislamu wengi wafungao huishia kushinda njaa na kiu bila kupata faida ya
funga zao kwa kutojizuilia na mambo maovu, machafu, laghawi, upuuzi, n.k.
v.
Wengi wafungao hawatekelezi nguzo na sunnah
za funga ipasavyo.
Pamoja na waislamu wengi kufunga, lakini wengi wao hawaswali kabisa swala
za faradh na sunnah na kubakia kufuata mkumbo kwa kushinda na njaa.
4.5. Hijjah.
§
Umuhimu
na Nafasi ya Hijjah katika Uislamu.
i.
Hijjah ni nguzo ya tano ya Uislamu.
Baada ya shahada, swala, zakat na funga, nguzo muhimu na ya mwisho ya
Uislamu ni Hijjah. Rejea Qur’an(3:97).
ii.
Hijjah ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Kama ilivyofaradhi kwa nguzo zingine, Hijjah ni ibada ya lazima kwa
waislamu wenye uwezo wa kimali na afya.
Rejea Qur’an(3:97).
iii.
Kutoenda Hija makusudi ni kustahiki adhabu
za Mwenyezi Mungu.
Kwa kila muislamu mwenye uwezo, akipuuza kutekeleza ibada ya Hijah basi
anastahiki adhabu hapa duniani na Akhera pia.
Rejea Qur’an(3:97).
iv.
Kutekeleza ibada ya Hija hupelekea kupata
msamaha Duniani na Akhera.
Kwa kila mwenye kutekeleza ibada ya Hijjah ipasavyo, basi husamehewa
madhambi yake yaliyotangulia.
§
Lengo la
Hijjah.
Kuwa askari Mcha-Mungu aliyekuwa tayari kutumia mali na nafsi yake katika
kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kutawala maisha ya jamii. Rejea Qur’an(48:18)
na (3:96-97).
§
Matendo
ya ibada ya Hijjah na Mafunzo yatokanayo.
Kabla na wakati wa kutekeleza ibada ya Hijjah, kuna mafunzo na hatua za
kuzingatia kama ifuatavyo;
i.
Maandalizi
na Safari ya Hijjah.
Ni lazima muislamu kabla ya kwenda Hijjah afanye maandalizi ikiwa ni
pamoja na kuzidisha ucha-Mungu, kuandaa gharama, mahitaji, n.k. Rejea Qur’an(2:197)
ii.
Ihram.
Ni hali ya kuwa katika vazi rasmi na miiko kwa mwanaume mwenye Kuhiji au
kufanya Umrah.
Funzo (49:13):
- Vazi la Ihram
linatufunza usawa baina ya wanaadamu wote.
iii.
Talbiya.
Ni kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kusema yafuatayo, “Labbayka Allahumma Labbayka. Labbayka
laashariika laka labbayka. Innal-hamda Wanni’imata laka wal-mulka, laashariika
laka”
Mafunzo (22:27) na (48:18):
-
Talbiya inatufunza kumuitikia Mwenyezi Mungu (s.w)
kufuata maamrisho na kuacha makatazo yake.
- Talbiya inatufunza
umoja na usawa baina ya waislamu wote.
iv.
Tawaf.
Ni kitendo cha kuizunguka Ka’aba mara saba kuanzia jiwe jeusi kwa
mwelekeo wa kinyume na saa kwa kulibusu au kuligusa au kuashiria.
Mafunzo:
-
Kuchukua ahadi ya utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
-
Kumtaja na kumtukuza Mwenyezi Mungu (s.w) kwa wingi.
-
Inatufunza umoja, udugu na usawa baina ya wanaadamu
wote.
v.
Sai.
Ni kitendo cha kutembea mara saba baina vilima viwili, Saffaa na Marwaa,
kwa kuanzia Saffaa na kumalizia Marwaa.
Mafunzo:
-
Inatufunza utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
-
Inatufunza ushujaa na uhodari katika kupigania Uislamu.
-
Inatufunza kuwa tayari kuhangaika kwa ajili ya
kupigania Uislam
vi.
Kupiga Kambi
Mina, Mwezi 8 Dhul-Hijah.
Ni kitongoji kilichopo baina ya Mji wa Makkah na bonde la Arafah.
Mahujaji hulala hapo na kuondoka kesho yake kuelekea Arafa asubuhi.
Mafunzo:
-
Huwafunza mahujaji kuwa askari waliotayari kuacha kila
chaokwa ajili ya kupigania Uislamu.
-
Huwafunza mahujaji kuwa askari wanatiifu kwa Muumba
wao.
vii.
Kusimama
Arafah, Mwezi 9 Dhul-Hija.
Arafa ni bonde lililo baina ya vilima vitatu. Mahujaji husimama humo
tangu Swala ya Adhuhuri hadi Magharibi na kuomba dua mbali mbali.
Mafunzo:
-
Huwakumbusha mahujaji mkutano mkuu wa siku ya Kiama.
-
Hutufunza kuwa hakuna aliyebora ila amchae Mungu zaidi.
-
Kisimamo cha Arafa kinatufunza usawa baina ya
wanaadamu.
viii.
Kupiga Kambi
Mzidalfah.
Mzidalfa ni kitongoji kilicho baina ya Mina na Arafa. Mahujaji huswali
Magharib na Isha hapo na kuelekea Mina mara tu baada ya swala Alfajir.
Mafunzo:
-
Huwafunza mahujaj kuwa askari waliojiandaa kupambana na
maadui wa Mwenyezi Mungu (s.w).
-
Kuomba dua hutufunza kuwa ushindi ni kwa nusura ya
Mungu tu.
ix.
Kutupa Mawe
Mina katika Minara Mitatu, Mwezi 10, Dhul-Hija.
Ni kitendo kinachofanyika kuanzia Mwezi 10-13, Dhul-Hija kwa kutupa
vijiwe saba kila Mnara.
Mafunzo:
- Zoezi hili
huwafunza mahujaj ujasiri wa kupambana na maadui zao.
- Huwafunza
mahujaj pia mbinu na silaha katika kupigana na maadui.
x.
Kuchinja
mnyama Mwezi 10, Dhul-Hija.
Katika siku hii Hajj atanyo nywele, kuchinja mnyama, kutupa mawe kwenye
Minara mitatu na kutufu Tawaful-Ifaadha (tawafu ya nguzo).
Mafunzo:
- Zoezi hili
linawafunza mahujaj utiifu kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
- Tunajifunza
kuwa tayari kuua au kuuawa kwa ajili ya Mungu.
- Inatufunza
kuwa na subira na kujitoa muhanga katika kunusuru dini Rejea Qur’an(22:37) na (37:111).
xi.
Siku za
Tashriiq Mwezi 11-13, Dhul-Hija.
Ni kilele cha ibada ya Hija, ambapo mahujaj hupumzika kambini na
kutathmini vitendo vyote walivyovifanya.
Mafunzo:
- Huwafunza
mahujaj kumkumbuka Mungu baada ya kazi ngumu.
- Huwafunza
askari kuwa na mazingatio na yale waliojifunza kwayo.
xii.
Tawaf ya
Kuaga (Tawaful-Widaa).
Ni Tawafu ya kuaga baada ya ibada ya Hija kukamilika na kujiandaa kurejea
nyumbani kwa mahujaji.
Mafunzo:
-
Huwafunza mahujaj kuwa viongozi (makhalifa) katika
ardhi.
-
Kuwa askari waliochukua mafunzo tayari kwa
kuyatekeleza.
-
Kuchukua ahadi ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
§
Kwa nini
wengi wanaohiji hawafikii lengo la Hijah zao?
Pamoja na mkusanyiko wa mamilioni wa mahujaj katika Mji wa Makka kila
mwaka lakini matunda ya Hija hayafikiwi. Zifuatazo ni baadhi ya sababu;
i.
Kuhiji kwa chumo la haramu.
Waislamu wengu hufunga safari ya kwenda hija kwa fedha za pato la haramu
ambazo ni kikwazo cha kupata matunda ya hija zao.
ii.
Kutochunga miiko, nguzo na sharti za Hijah.
Pamoja na kufunga safari ya Hijah au Umrah, mahujaj wengi hawachungi
miiko, nguzo na masharti ya Hijah au Umrah ipasavyo. Rejea Qur’an(2:197).
iii.
Kutokuwa na elimu na ujuzi sahihi juu ya
ibada ya Hijah.
Mahujaji wengi hufunga safari ya kwenda Hija au Umrah ili hali hawana
ujuzi wowote wa ibada watakazozitekeleza ila kufuata mkumbo tu.
iv.
Kutojulikana kwa lengo halisi la Hijah au
Umrah.
Waislamu wengi hufunga safari ya Hijah au Umrah kwa lengo la kupata
thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio kuwa askari wa kupigania dini. Rejea Qur’an(51:56).
v.
Kufunga safari ya Hijah kwa Malengo mengine.
Waislamu wengi hufunga safari kwa ajili ya biashara, utalii au kutafuta
umaarufu wa kujiita majina ya Al-Hajj ambayo ni nje na lengo la Hijah.
5.0. HAKI NA UADILIFU KATIKA
UISLAMU.
5.1. Dhana ya Haki na Uadilifu katika Uislamu.
§
Maana ya
Haki kwa Mtazamo wa Uislamu.
Ni muunganiko wa sheria na maadili kwa lengo na madhumuni ya kuilea jamii
katika amani, furaha, udugu wa kweli na mahusiano mema kati ya wanaadamu.
§
Misingi
ya Haki na Uadilifu katika Uislamu.
Maisha ya furaha na amani ya kweli hupatikana kwa kusimama misingi ya
haki na Uadilifu katika jamii kama ifuatavyo;
i.
Tawhiid.
Haki na Uadilifu wa kweli hupatikana kwa kumuamini na kumpwekesha
Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo katika maamrisho na makatazo yake.
ii.
Utume.
Katika kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) ni kufuata misingi
ya miongozo ya mitume wake wote kupitia vitabu vyao.
iii.
Siku ya Mwisho.
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha yetu ni kuzingatia kuwa
kila kitendo kitahukumiwa na kulipwa kwa haki siku ya Kiyama.
§
Aina au
migawanyo mbali mbali ya Haki katika Uislamu.
1.
Haki za Allah.
2.
Haki za Nafsi.
3.
Haki za Viumbe na Mazingira.
4.
Haki za Binadamu kwa ujumla.
5.
Haki za Raia katika Dola ya Kiislamu.
6.
Haki za Maadui katika Vita (mateka).
1. Haki za Mwenyezi Mungu (s.w).
Katika Uislamu haki za Mwenyezi Mungu ziko makundi
mawili;
i.
Haki ya
Uungu.
Ni kumsifu na kumtii kwa sifa zake kama za uumbaji, umilikaji na ulezi wa
viumbe vyote na ukamilifu wake tofauti na viumbe alivyoviumba.Rejea Qur’an(45:23),
(25:68), (9:31) na (31:13).
ii.
Haki ya
Kuabudiwa.
Ni Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa na viumbe
vyake muda wote, na ndio lengo kuu la kuumbwa mwanaadamu.Rejea Qur’an(51:56),
(5:44), (11:25-26) na (29:16-17).
2. Haki za Nafsi.
Haki za nafsi imekokotezwa kuanzia binafsi, familia,
wazazi, n.k kama ifuatavyo;
(a)
Mtu Binafsi.
Haki za msingi ni chakula, makazi, malezi, elimu, mavazi, matibabu na
kufanyia kazi vipaji na neema alizonazo inavyostahiki ikiwemo;
·
Haki ya
Macho.
Ni kutazama yaliyoamrishwa na kuyaepusha na
yaliyoharamishwa.
Rejea Qur’an(17:36),
(41:20), (24:30-31) na (20:131).
·
Haki ya
Masikio.
Ni kusikiliza yaliyoamrishwa na kutosikiliza
yaliyoharamishwa pia. Rejea Qur’an(8:22) na (6:25).
·
Haki ya
Midomo na Ulimi.
Ni kula, kunywa na kuzungumza yaliyohalalishwa na sio
yaliyoharamu.
Rejea Qur’an(16:114), (17:26-29), (17:53), (41:33) na
(31:6).
·
Haki ya
Mikono na Miguu.
Ni kushika na kuendea vyote vilivyoamrishwa na kuacha
vilivyokatazwa.Rejea Qur’an(25:72) na (31:18).
(b) Haki za Familia.
Ni kusimamia malezi, elimu, uadilifu na wajibu wa kila
mmoja katika familia kwa muongozo wa Qur’anna
Sunnah ili kuleta kufikia lengo la kuumbwa. Rejea Qur’an(52:21).
(c) Haki za Watoto.
Watoto wana haki ya kupata malezi na makuzi bora
kulingana na mahitaji yao kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’anna Sunnah katika
sehemu zifuatazo;
·
Haki ya
Uhai.
Uhai wa mtoto ni haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu (s.w)
kupitia malezi na makuzi ya wazazi.
·
Haki ya
Nasaba.
Mtoto kupata
nasaba ni haki kisheria ili kuwa mwanafamilia halali. Rejea Qur’an(33:4).
·
Haki ya Makuzi
na Malezi bora.
Makuzi na malezi bora ya mtoto ni kupata haki zake za
msingi na elimu inayomuwezesha kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo. Rejea Qur’an(66:6).
(d) Haki za Wazazi.
Ni kuwahurumia, kuwaheshimu, kuwafanyia wema,
kuwahudumia na kuwalea ipasavyo. Rejea Qur’an(31:14), (17:23-24), (4:36),
(6:151), (19:14) na (19:32).
(e) Haki za Jamaa na Majirani.
Ni kutunza
uhusiano na kusaidiana pale inapohitajika kwa kuzingatia mipaka. Rejea Qur’an
(2:215).
(f) Haki za Mayatima, Wajane na Masikini.
Ni kuwahifadhi na
kuwasaidia wanapokuwa na shida na mahitaji ya kimaisha.
Rejea Qur’an(2:220),
(4:2), (4:10), (2:262) na (2:267).
(g) Haki za Udugu wa Kiimani na za Watu wengine.
Udugu wa kiimani
ni haki na bora zaidi kuliko udugu wa damu au nasaba.
Rejea Qur’an(49:10),
(49:13), (7:172-173), (4:7) na (5:8).
3. Haki za Viumbe na Mazingira.
Uislamu umeweka kipaumbele katika kuhifadhi mazingira na
kutunza viumbe hai na visivyo hai kupitia sera mbali mbali zikiwemo;
·
Haki ya Hifadhi ya Mazingira na misitu.
Rejea Qur’an(6:38),
(27:60), (16:10-13), (50:7-9), (56:63-64) na (39:62).
·
Mazingira ni amana katika kulinda uhai wetu na
wa viumbe wengine.
Rejea Qur’an(7:10)
na (16:112).
·
Sera na Mafundisho ya Mtume (s.a.w) juu ya
hifadhi ya mazingira katika kuleta ustawi wa jamii.
·
Sera ya mapinduzi ya kitabia katika kutunza na
kuhifadhi mazingira yote yanayotuzunguka.
·
Sera ya usafi na uhifadhi wa mazingira ili
kuleta ustawi wa viumbe hai.Reje Qur’an(6:141) na (25:2).
4. Haki za Binaadamu kwa Ujumla (Basic Human
Rights).
Uislamu umezingatia, kulinda na kusimamia haki za msingi
za kibinaadamu bila kujali tofauti zao. Haki hizo ni pamoja na;
·
Haki za kuishi (maisha). Rejea Qur’an(5:32), (6:151) na (17:33).
·
Haki ya Usalama wa Maisha Rejea
Qur’an(5:32).
·
Haki ya
kulinda na kuheshimu hadhi na usafi wa mwanamke. Qur’an(17:32) na (24:2).
·
Haki ya kupata mahitaji ya lazima ya maisha. Rejea Qur’an(70:24-25).
·
Haki ya
Uadilifu na Usawa katika Hukumu (Righ to justice).Rejea Qur’an(5:8), (49:13) na
(4:135).
·
Haki ya Uhuru (kila mtu kuwa huru).
Uislamu umezingatia kila mtu kuwa huru kifikra na
kutomilikiwa kama bidhaa ya baishara.
5. Haki za Raia katika Dola ya Kiislamu.
·
Haki za msingi za raia waislamu na wasiokuwa
waislamu katika Dola ya Kiislamu ni pamoja na;
·
Haki ya kuendesha maisha binafsi bila kuingiliwa
na mtu yeyote.
·
Haki na uhuru wa kutoa maoni na kuamrisha mema
na kukataza mabaya.
Rejea Qur’an(3:104),
(9:71), (9:67).
·
Haki na Uhuru katika kufuata na kuabudu dini
yeyote aipendayo mtu.
Rejea Qur’an(2:256),
(6:108), (29:46) na (16:125).
·
Haki ya Kuwashtaki Viongozi wa juu wa Dola bila
upendeleo na ubaguzi wowote.
·
Haki ya kumiliki mali au rasilimali zozote za
halali na zisizoleta madhara kwa raia na Dola
kwa
ujumla.
·
Rejea Qur’an(2:262), (2:267) na (18:32-43).
6. Haki za Maadui Katika Vita (mateka wa
Kivita).
Uislamu
unajali, kusimamia na kulinda haki ya kila mtu hata kwa maadui waliokamatwa
katika vita (mateka) walifanyiwa haki na uadilifu kama ifuatavyo;
·
Kuhurumiwa na kutofanyiwa ukatili wowote maadamu
wamedhibitiwa.
·
Kuwapa mahitaji yao ya lazima ya kibinaadamu na
kimaisha pia.
·
Kulinda uhai na usalama wa maisha yao mpaka mwisho
wa uhasama.
·
Mateka wa kivita walikuwa na haki ya kujikomboa
kwa njia zifuatazo;
o
Kulipa kiasi fulani cha pesa au mali yeyote
inayokubalika.
o
Kubadilishana na mateka Waislamu waliokamatwa na
maadui.
o
Kulipa fidia kwa kufanya jambo fulani lenye
manufaa kwa jamii ya waislamu. Rejea Qur’an(47:4).
·
Masuria na mateka wanawake walikuwa na haki ya
kulindwa na kuhifadhiwa kwa kupewa
wanaume
waliokwenda vitani na kuishi nao katika maisha ya ndoa ili kupata mahitaji yao
ya
msingi.
·
Haki ya kumiliki mali au uchumi ulio wa halali
na usio leta madhara yeyote katika Dola ya
Kiislamu.
5.2. Msimamo wa Uislamu juu ya Utumwa.
- Hali ya Utumwa kabla ya Mtume Muhammad
(s.a.w).
-
Biashara ya
utumwa ilidumu na kuenea sana enzi za ujahili takribani nchi na
mabara
mbali mbali hasa nchi za Magharibi, Uarabuni, Bara la Asia na kwingineko
Duniani.
- Watumwa
walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.
- Watumwa
walimilikiwa kwa kuuzwa na kununuliwa kama bidhaa za biashara au kwa matumizi
mengineyo pia.
- Watumwa
walikuwa wakitumika kama sehemu ya starehe na kiburudisho kwa wakubwa zao.
- Mateso,
unyama na ukatili ilikuwa desturi ya kufanyiwa watumwa na mabwana zao katika
kutimiza
matashi
yao.
- Watumwa
walikuwa hawana uhuru wa kufanya na kufuata mila, desturi au dini waitakayo na
waipendayo
wao
wenyewe bila ruhusa ya wakubwa wao.
- Watumwa walikuwa wakitumikishwa kama
wanyama au hata zaidi ya wanyama kwa kufanyishwa kazi
ngumu
zilizozidi uwezo wao.
- Kila jaribio la ubaya lilifanywa kupitia watumwa, mfano makali ya
kisu, mkuki,
mshale, n.k yalijaribiwa kwa
watumwa.
- Watumwa ndio ilikuwa nyenzo pekee ya kufanyia kazi, kubebea na
kusafirishia
mizigo mikubwa kwa masafa ya
mbali.
- Hadhi na nafasi kati ya mabwa na watumwa ilikuwa na utofauti mkubwa
mno,
kiasi kwamba bwana anaweza
kumdhalilisha mtumwa kwa namna apendavyo.
- Huduma na misaada ya kiutu kwa watumwa ilikuwa hafifu mno, kiasi
kwamba
mtumwa akiugua au kukosa uwezo
wa kuzalisha mali alikuwa hana faida tena
kwa bwana.
§ Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya
Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w).
Uislamu baada ya kuenea na kuongoza sehemu mbali mbali, ilikuwa ndio
mwanzo wa kukomesha biashara ya utumwa na kumkomboa mwanaadamu kiutu, (kiroho),
kifikra na kisaikolojia kupitia njia na sera mbali mbali kama ifuatayo:
-
Uislamu
ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya
Mwenyezi Mungu (s.w.
- Uislamu ulijenga uhusiano wa udugu na upendo baina ya watu bila
kujali hadhi, nafasi, rangi,
taifa la mtu.
- Uislamu ulisisitiza kuwa
ubora wa mtu unatokana na ucha-Mungu wake na pia mtumwa au mtu
huru anastahiki kuwa kiongozi na kutiiwa ipasavyo Rejea Qur’an(49:13) na (4:25).
- Utumwa katika Uislamu ulikuwa jambo la
kupita na sio taasisi ya kudumu inayojenga matabaka ndani ya jamii.
-Uislamu
uliweka mikakati ya kulinda haki, utu na hadhi ya watumwa kwa kuwafanyia wema
na ihsani kama wanaadamu wengine.Rejea Qur’an(4:36) na (49:13).
- Watumwa walikuwa na haki ya kuamini na
kufuata mila au dini waipendayo bila kushurutishwa. Rejea Qur’an(2:256).
- Watumwa walikuwa wanapata huduma za
kijamii kama mavazi na malazi sawa na mabwana au wanaadamu wengine.
- Mtumwa alikuwa akikosea alisamehewa
badala ya kuadhibiwa, Mtume (s.a.w) alisema mtumwa asamehewe hata mara sabini
kwa siku.
- Mtumwa alistahiki kuwa kiongozi na
kutiiwa ipasavyo maadamu ni muislamu na Mcha-Mungu. Mtume (s.a.w) amesema “msikilizeni na mtiini kiongozi hata akiwa ni
mtumwa wa kutoka uhabeshi, maadam anafuata njia ya haki”
- Uislamu unalinda hadhi ya mtumwa kwa
kutomuita “Ewe mtumwa wangu” badala
yake anaitwa “Ewe kijana wangu”.
- Watumwa walikuwa na haki ya kujikomboa
na huru kwa njia mbali mbali zikiwemo:
o
Kulipa kiasi fulani cha pesa au mali yeyote
inayokubalika.
o
Kubadilishana na mateka Waislamu waliokamatwa na
maadui.
o
Kulipa fidia kwa kufanya jambo fulani lenye
manufaa kwa jamii ya waislamu. Rejea Qur’an(47:4).
- Mtume (s.a.w) na Maswahaba waliwaachia
watumwa huru na kuwakomboa wengine kisha kuwaacha huru kama ifuatavyo:
o
Mtume (s.a.w) mwenyewe aliwaacha huru watumwa
63.
o
Bi Aisha (r.a) mkewe Mtume (s.a.w) aliwaacha
huru watumwa 67.
o
Ibn Abbas aliwaachia huru watumwa 70.
o
Abdallah bin Umar aliwaacha huru watumwa 1,000.
o
Abdul-Rahman bin Auf alinunua watumwa 30,000 na
kuwaacha huru.
Mpaka kufikia mwisho wa uongozi wa Makhalifah wa nne Waongofu, suala la
Utumwa lilibakia kuwa historia katika ulimwengu wa Kiislamu.
6.0. QUR’AN
6.1. Sura za Makkah na Madinah.
·
Mgawanyiko
wa Qur’an.
- Qur’anyote
ina jumla ya sura 114 Sura zilizoshuka Makkah ni 86 zilizoshuka kwa miaka 13
cha Utume Na za Madinah ni 28 zilizoshuka kwa miaka 10.
§ Tofauti kati ya Sura za Makkah na Madinah
|
Sura za Makkah |
Sura za Madinah |
|
1. Walengwa. Walengwa
walikuwa waumini waliosimu mwanzo wa Utume. |
Zililenga
Maadui wa Dola ya Kiislamu Madinah wakiwemo; Wanafiq, Washirikina, Wayahudi
na Wakristo. |
|
2. Ujumbe. Sehemu kubwa
ya ujumbe ni kujenga imani juu ya Mwenyezi Mungu (s.w), Malaika, Vitabu,
Mitume, Siku ya Mwisho na Qudra yake. |
Ujumbe
ulilenga ujenzi wa Dola na jamii ya Kiislamu Madinah kupitia sheria na hukumu
mbali mbali. |
|
3. Muundo wa sura. Sura nyingi ni
fupi na zina aya fupi fupi zenye lengo moja. |
Sura nyingi ni
ndefu na zina aya ndefu zenye ufafanuzi zenye lengo la utekelezaji wa sheria. |
|
4. Mbinu Zimetumia
lugha fupi ya mchomo kwa walengwa kwa kutumia viapo, historia ya watu
waliopita, kuwahofisha na kuwakatisha tamaa maadui wa Uislamu na kuwatia moyo
na kuwaliwaza waumini katika kutekeleza ujumbe wa Qur’an. |
Zimetumia
lugha ya sheria na ufafanuzi katika ujenzi wa Dola ya Kiislamu Madinah, kwa
kutumia historia ya Mitume ili kuwaliwaza waumini kupigania Dini na
kuwakatisha tamaa maadui wao wakiwemo; makafiri, washirikina, wanafiq na
Wakristo. |
6.2.
Tafsiri na Mafunzo ya Sura Zilizochaguliwa.
§ Suratul-Fiyl (105): Imeteremshwa Makkah,
Ina Aya Tano.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye
Kurehemu.
1.
Jee, huoni jinsi Mola wako alivyowafanya watu wa ndovu
(tembo)?
2.
Jee, hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?
3.
Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi.
4.
Wakawapiga kwa vijiwe vya udongo wa motoni.
5.
Akawafanya kama majani yaliyoliwa (na kutemwa).
Mafunzo kwa Ufupi.
1.
Mwenyezi Mungu (s.w) ni Muweza wa kila kitu.
2.
Viumbe vyote viko katika Milki ya Mwenyezi Mungu (s.w)
na ni Majeshi yake yaliyotayari kumtumikia ipasavyo.
3.
Nusura na Msaada wa Mwenyezi Mungu (s.w) hupatikana
muda wowote watu watakapomuamini na kumtegemea ipasavyo.
4.
Kuangamizwa kwa Abraha na jeshi lake na Jeshi
asilolijua wala kulitegemea ni dalili ya Kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).
§ Suratul-Humaza (104): Imeteremshwa Makkah,
Ina Aya Tisa.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye
Kurehemu.
1.
Adhabu kali itamthubutikia kila mwenye kuramba kisogo,
asengenyaye, msengenyaji.
2.
Ambaye amekusanya mali na kuihesabu (tu bila ya
kuitumia katika njia za kheri).
3.
Anadhania kuwa mali yake itambakisha milele.
4.
Hasha! Bila shaka atavurumishwa katika (moto unaoitwa)
Huttama.
5.
Na ni jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni
nini (huo moto unaoitwa) Huttama?
6.
(Huo ni) moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa (kwa ukali
bara bara).
7.
Ambao unapanda (mpaka) nyoyoni.
8.
Hakika watafungiwa ndani ya moto huo.
9.
Kwa manguzo marefu (ili wasiweze kutoka).
Mafunzo kwa Ufupi ya suratul
Humaza
1.
Kusengenya ni katika makosa makubwa kabisa.
2.
Ni makosa makubwa kukusanya mali bila kuitumia katika
njia za kheri.
3.
Matumizi mabaya ya ulimi na neema zingine hupelekea
kwenye maangamizi na adhabu.
4.
Matumizi mabaya
ya ulimi kama fitna, uongo, usengenyi, n.k. huleta chuki, husda na mtafaruku
katika jamii.
§ Suratul-A’sr (103): Imeteremshwa Makkah,
Ina Aya Tatu.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye
Kurehemu.
1.
Naapa kwa zama (zako Ewe Nabii Muhammad!).
2.
Kuwa wanaadamu yuko katika hasara.
3.
Isipokuwa wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri
na wakausiana (kufuata) haki na wakausiana (kushikamana) na subira.
Mafunzo kwa Ufupi.
1.
Mwenyezi Mungu huapia kitu au kiumbe chochote
kinachofahamika ili kutoa uthibitisho kwa kile anachoapia.
2.
Muumini haruhusiwi kuapa kwa kiumbe chochote isipokuwa
kwa jina la Mwenyezi Mungu peke yake.
3.
Wakati (muda) ni rasilimali muhimu sana inayotakiwa
kutumiwa kwa uangalifu mkubwa.
4.
Imani ya kweli huthibitishwa katika vitendo vizuri.
5.
Uislamu sio dini ya ubinafsi, hivyo ni lazima watu
wausiane katika kufanya wema na kufuata haki.
6.
Subra ni nyenzo muhimu sana na ya pekee katika kuweza kuusimamisha
Uislamu
§ Suratul- Takaathur (102): Imeteremshwa
Makkah, Ina Aya Nane.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye
Kurehemu.
1.
Kumekughafilisheni (katika) kutafuta wingi (wa mali na
jaha na watoto na kujifakharisha kwayo).
2.
Hata mmeingia makaburini (mmekufa kabla ya kufanya
kheri yeyote).
3.
Sivyo hivyo! Karibuni hivi mtajua (kuwa sivyo hivyo).
4.
Kisha (nasema) sivyo hivyo karibuni hivi mtajua (kuwa
sivyo hivyo).
5.
Sivyo hivyo! Lau kama mnajua ujuzi wa yakini (kuwa
sivyo hivyo msingefanya hivyo).
6.
Hakika mtauona moto wa Jahiym.
7.
Kisha (nasema) mtauona (moto) kwa yakini.
8.
Kisha kwa hakika mtaulizwa siku hiyo juu ya neema
mlizopewa (mlizitumiaje).
Mafunzo kwa Ufupi.
1.
Pupa katika kutafuta anasa za dunia ndizo hupelekea mtu
kumuasi Mwenyezi Mungu (s.w).
2.
Kuchuma mali na kuhangaikia watoto sio jambo baya, bali
lisitusahaulishe katika kumtumikia Mwenyezi Mungu (s.w).
3.
Kuwepo siku ya mwisho ni jambo lisilo na shaka ili kila
mtu akaulzwe juu ya jinsi alivyotumia neema alizopewa.
4.
Kutumia vibaya neema na vipawa tulivyonavyo hupelekea
kumuasi Mola wake na hivyo kustahiki adhabu.
5.
Neema na vipawa tulivyonavyo ni dhamana kwetu na
tutaulizwa siku ya Kiama.
6.3.
Kukusanywa na Kuhifadhiwa kwa Qur’an.
§ Qur’anina
ahadi ya kuhifadhiwa na kulindwa na Mwenyezi Mungu (s.w) tofauti na vitabu
vingine kama aya zifuatazo zinavyobainisha;
“Hakika Sisi ndio tulioteremsha mawaidha
haya (Qur’an) na hakika Sisi ndio tutakayoyalinda” (15:9).
“Hakitakifikia batili mbele yake wala
nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye Hikima ahimidiwaye” (41:42).
§
Njia na
Hatua zilizotumika katika kuihifadhi na kuilinda Qur’an.
Mtume (s.a.w) mwenyewe aliweka misingi madhubuti ya kuihifadhi na
kuhakikisha kuwa Qur’anhaipotei kupitia njia zifuatazo;
1.
Mtume (s.a.w) alihifadhishwa na kufanyishwa marejeo ya Qur’anyote
na Malaika Jibril (a.s) mara kwa mara, hasa mwezi wa Ramadhani. Rejea Qur’an(73:1-4),
(2:185).
2.
Mtume (s.a.w) aliahidiwa kuwa atasomeshwa Qur’anna
Mwenyezi Mungu (s.w) na hata sahau kamwe.
Rejea Qur’an(75:16-19) na (87:6-7).
3.
Mtume (s.a.w) aliwahifadhisha Maswahaba na Waislamu Qur’anvifuani
mwao wakati ilipokuwa inashuka.
Zaidi bin Thaabit amesema: “…..kila
nilipomaliza kuandika (Wahayi), Mtume (s.a.w) aliniamuru nisome nilichoandika
na nilikuwa ninamsomea. Kama palikuwa na
kosa alilisahihisha kisha aliwapa watu (kunakili na kuhifadhi vifuani mwao)”.
4.
Maswahaba waliihifadhi na kuisoma Qur’anmara kwa mara
hasa katika ibada za swala na zinginezo.
Rejea Qur’an(73:1-5).
5.
Mtume (s.a.w) aliwasomea waandishi wa Qur’an(wapatao
42) na kuandika kama walivyosomewa na kisha Mtume (s.a.w) aliwataka wasome ili
ahakiki walichoandika.
Uthman bin Affan (r.a) amesimulia:
“Wakati wowote Mtume wa Allah (s.a.w) alipoteremshiwa wahyi humuita mmoja wa
watu waliochaguliwa kuandika.” (Ameipokea Tirmidh)”.
6.
Mtume (s.a.w) aliwaagiza na kuwasimamia waandishi wa Qur’anwapangilie
sura na aya kama zilivyo katika msahafu akiongozwa na Malaika Jibril (a.s).
Uthman bin Affan (r.a) ameeleza:
“Ilikuwa kawaida ya Mtume wa Allah kila iliposhuka aya za sura mbali mbali (za
Qur’an) au kila aya iliposhuka alimuita mmoja wapo wa waandishi wa Qur’anna
kumwambia, “andika aya hizi katika sura kadhaa baada ya aya kadhaa.”
§ Umihimu wa kunakiliwa upya Qur’anwakati wa Uthman
bin Affan (r.a).
Khalifa Uthman bin Affan (r.a) aliteuwa waandishi 4 kunakili misahafu 7
kutoka kwenye msahafu ulioandikwa wakati wa Mtume (s.a.w) kwa sababu zifuatazo;
- Kutokana na
kupanuka Dola ya Kiislamu na kusambaa maswahaba na walimu wa Qur’anmaeneo mbali
mbali.
- Kuwa na
hitajio kubwa la kufundishwa ujumbe wa Qur’ansehemu mbali mbali hasa za ugenini.
- Watu wengi waliingia katika Uislamu
wakiwa wageni wa lugha ya Qur’an(Kiarabu) na kushindwa kuisoma na kupata ujumbe
wa Qur’an.
- Kuepusha
kutofautiana kwa matamshi ya usomaji wa Qur’anya asili katika ufikishaji wa
ujumbe wa Qur’an.
- Kuepusha
kupatikana mwanya wa maadui wa Uislamu katika upotoshaji na upoteaji wa ujumbe wa
asili wa Qur’an.
6.4. Madai na Hoja za
Makafiri dhidi ya Qur’an.
Qur’anyenyewe inajieleza
kuwa ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake,
“Hiki
ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake” (2:2).
Makafiri wa zamani na wa zama hizi wametilia shaka Qur’ankwa kutoa madai
yafuatayo;
i.
Mayahudi wameikataa Qur’ankwa lengo la kuficha haki na
batili (kuchanganya haki na batili). Qur’an(2:42), (40:74), (2:105) na (2:23).
ii.
Dai kuwa Qur’anni uzushi, uongo na visa vya watu wa
kale. Qur’an(53:13), (65:15), (6:25), (38:7) na (8:31-32).
iii.
Dai kuwa Mtume ni mwendawazimu. Qur’an(16:6), (13:47), (23:70), (68:5).
iv.
Dai kuwa Yuko anayemfundisha. Qur’an(10:103), (44:14) na (25:2).
v.
Dai kuwa Qur’anni uchawi na maneno ya shetani. Qur’an(34:43), (26:210).
vi.
Dai kuwa Mtume amerogwa. Qur’an(17:43)
vii.
Dai kuwa Qur’anni mashairi ya Muhammad. Qur’an(21:5), (52:33).
viii.
Dai kwa nini hajapewa miujiza kama aliyopewa nabii
Musa. Qur’an(28:48)
ix.
Dai kwa nini Qur’anhaikuteremshwa yote kwa wakati
mmoja.Qur’an(25:32).
x.
Kuifanyia Qur’anmzaha, chuki, kujivuna na kujiona.
Qur’an(41:52), (47:9), (86:13-14), (21:216-217), (45:9), (9:64).
xi.
Dai kuwa Muhammad si Mtume. Qur’an(13:43).
xii.
Dai kwa nini Muhammad hakuteremshiwa Malaika. Qur’an(17:95).
xiii.
Dai kuwa mtume gani anayekula na kwenda sokoni. Qur’an(55:7).
xiv.
Dai kuwa kwa nini ametumwa binadamu. Qur’an(34:43), (17:94).
xv.
Dai kuwa Mtume apande mbinguni na ateremke na Kitabu
ili wakisome. Qur’an(17:93), (74:53).
7.0.
SUNNAH NA HADITH.
7.1. Hoja juu ya Kukubalika
Hadith.
§ Hadith
ni chanzo na chem chem ya pili kuwa muongozo wa maisha ya waumini baada ya
Qur’an.
“Anachokupeni Mtume chukuweni na
anachokukatazeni nacho kiacheni.” (59:7).
“Anayemtii Mtume ameshamtii Mwenyezi Mungu.”
(4:80) Rejea pia Qur’an(52:3-4).
§ Zifuatazo ni baadhi ya hoja za wapinzani wa
Hadith.
i.
Hadith hazikufuata mpango kama ulivyo mpangilio wa Qur’anwakati
wa kushuka, kupangwa, kuhifadhiwa na kuandikwa.
Udhaifu wa dai hili;
- Kutoandikwa kwa Hadith kama
ilivyoandikwa Qur’ansio hoja na sababu ya kutokubalika Hadith.
- Mtume mwenyewe aliwakataza Maswahaba kuandika
Hadith wakati wa uhai wake.
ii.
Baada ya kufa Mtume (s.a.w), waislamu waligawanyika
makundi tofauti yanayopingana, na hata kuweza kubuni maneno na kudai kuwa ni
Hadith za Mtume (s.a.w). Je utajuaje Hadith zilizosahihi?
Udhaifu wa Hoja hii;
- Kuna Wanachuoni wenye msimamo
madhubuti waliobobea katika elimu ya Hadith na hawakujihusisha na migogoro
yeyote iliyozuka
- Vigezo vya kisayansi kama Isnad, Riwaya na Matin vilitumika katika kuchambua usahihi na udhaifu wa Hadith.
iii.
Hadith zilikusanywa na kuandikwa muda mrefu baada ya
kufa Mtume (s.a.w) na Maswahaba. Je kuna ushahidi gani unaothibitisha kuwa
maneno yaliyosemwa ni ya mtume (s.a.w)?
Udhaifu wa Hoja hii;
- Sunnah ya Mtume (s.a.w) ni
maelezo juu ya maisha yake ambayo maswahaba walirithishana baada ya kutawafu
(kufa) Mtume.
- Ukusanyaji na uandishi wa
Hadith ulifanyika kwa utaalamu wa kisayansi katika kubaini ukweli wa Hadith.
7.2. Mafunzo ya Hadith
Zilizochaguliwa.
§ Hadith ya Kwanza; Kuamrisha mema na
Kukataza Maovu.
Kutoka kwa Abi Saidil-Khudhur (r.a) amesema: Nimemsikia mjumbe wa
Mwenyezi Mungu anasema;
“Mwenye kuuona uovu
miongoni mwenu na auondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi (na aondoshe) kwa
ulimi wake iwapo hawezi (na aondoshe) kwa moyo wake (achukie) na hiyo ndiyo
imani dhaifu.” (Ameipokea Muslim).
Hatua
za kuondosha uovu:
-
Hatua ya kwanza na bora ni kuondosha kwa mikono.
-
Hatua ya pili kwa ubora ni kuondosha kwa kusema.
-
Na hatua ya mwisho na dhaifu ni kuchukia moyoni.
Mafunzo ya Hadith kwa Ufupi:
1.
Ni wajibu kuondosha maovu kwa kisaidizi chochote kile
kiwacho kulingana na mazingira.
2.
Jukumu la kuamrisha mema na kukataza maovu linaanzia
kwa mtu mmoja mmoja na ummah kwa ujumla
3.
Kutochukia uovu na kuridhika nao ni dalili ya kukosa
imani moyoni.
§ Hadith ya Pili: Sifa za Muumini wa kweli.
Kutoka kwa Ibn Umar (r.a) amesema: Kasema mjumbe wa Mwenyezi Mungu;
“Muislamu wa kweli ni yule wanaosalimika
Waislamu kutokana na (maudhi) ya ulimi wake na mkono wake. Na muumini wa kweli
ni yule wanaomuaminisha watu juu ya damu zao na mali zao.” (Muttafaqun Alayhi)
Mafunzo ya Hadith kwa Ufupi:
1.
Haifai kuwaudhi, kuwafitinisha, n.k. waislamu,
wanaadamu wengine pamoja viumbe kwa ujumla.
2.
Miongoni mwa maudhi ya ulimi ni kusengenya, kukejeli,
kufitinisha, kupigana, kudhulumu na kuitanana majina mabaya.
3.
Uislamu ni dini ya mapenzi, huruma, kusaidiana na
kushirikiana.
4.
Muumini wa kweli ni muaminifu kwa kila anachosema na
kutenda pia.
§ Hadith ya Tatu: Ukarimu na Kusaidiana.
Kutoka kwa Abi Saidil-Khudhur (r.a) kasema: ilitokezea tumo safarini
pamoja na Mtume (s.a.w); akaja mtu mmoja juu ya kipando chake, akawa anaangaza
kulia na kushoto, Mtume (s.a.w) akasema;
“Mwenye kipando cha ziada na ampe
msaada asiye na kipando, na mwenye chakula kilichozidi (matumizi yake) na ampe
msaada mwenye kukihitaji (asiyenacho)”
Akataja
aina mbali mbali za mali mpaka tukaona (tukajua) kwamba hatuna haki ya kuweka
ziada (baada ya matumizi yetu). (Ameipokea
Muslim)
Mafunzo ya Hadith kwa Ufupi:
1.
Ni wajibu wa kila muislamu aliyenacho kumtilia hima kila
anayehitaji msaada wa kibinaadamu.
2.
Ugawaji mbaya wa rasilimali na utajiri ndio sababu ya
kuwepo matabaka ndani ya jamii.
3.
Uislamu umekataza kuhodhi bidhaa muhimu kwani kinyume
cha sheria.
4.
Uislamu umetilia mkazo maisha bora kwa kila raia na
kukataza kufanya israfu.
8.0 DOLA YA KIISLAMU MADINAH
8.1.
Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah.
- Kabla ya
kufika Madinah, Mtume (s.a.w) akiwa mji wa Quba aliamuru msikiti ujengwe
uliokuwa Ukiitwa ‘Masjid Quba.’ Rejea Qur’an(9:108).
- Mtume alifika Madinah (Yathrib), Oktoba 622
A.D.
- Kwa heshima
ya Mtume (s.a.w) Madinah ikapewa jina la Madinatun-Nabii (mji wa Mtume) na
Al-Madinah Al-Munawwarah (mji ung’aao).
§ Hatua
na Mambo (Taasisi za Kisiasa) za msingi alizotumia Mtume (s.a.w) katika
kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah.
1.
Kujenga Msikiti.
- Msikiti
ulikuwa ndio Ikulu, mahakama, kituocha jeshi, ukumbi wa bunge (shura), n.k. Qur’an(3:95),
(2:150).
- Ulikuwa kituo
muhimu cha kiharakati katika kusimamisha na kuendeleza Uislamu. Rejea Qur’an(22:40),
(2:114), (72:18) na (9:19).
2.
Kujenga Ummah wa Kiislamu.
- Mtume (s.a.w)
aliwapatanisha kabila la Aus na Khazraj Madinah waliokuwa na uadui wa muda
mrefu baina yao. Qur’an(3:103).
- Mtume (s.a.w) pia
aliwaunganisha udugu imara kati ya Muhajirina wa
- Makkah na Answaar
wa Madinah na kuwa ummah mmoja. Qur’an(8:75).
- Pia
aliimarisha uchumi kwa kuunganisha ummah wa Kiislamu na kuwa kitu kimoja. Qur’an(59:8-9).
3.
Kuweka Mkataba wa Madinah (Madinah Charter).
- Mtume (s.a.w)
alijieleza katika mkataba huo kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ndiye
kiongozi mkuu wa Dola ya Kiislamu.
- Mkataba
uliainisha vipengele vya amani na wajibu wa kila kundi kati ya makabila ya
Mayahudi na Waarabu washirikina wa Madinah na Dola ya Kiislamu Madinah.
- Uliainisha nafasi,
majukumu na wajibu wa waumini katika Dola.
- Mkataba uliainisha
uhuru wa kila mtu kuabudu kwa mujibu wa imani na dini zao.
4.
Kuweka Mikataba ya amani na Makabila ya Mayahudi
na mengine yaliyokuwa pembezoni mwa Dola ya Kiislamu Madinah.
- Makabila na
koo tatu za Kiyahudi zenye nguvu zilizokuwa pembezoni mwa mji wa Madinah yalikuwa;
·
Banu Quraizah
·
Banu Qainuqa na
·
Banu Nadhir
5.
Kuunda Shura na Sekretarieti.
- Mtume (s.a.w)
aliteua washauri wake wakuu katika kuendesha Dola ambao Walikuwa Abu Bakr
(r.a), Umar bin Khattab (r.a), Uthman bin Affan (r.a), Ally bin Abu Twalib
(r.a) na Hamza bin Abdul-Muttalib
(r.a).
- Aliteua waandishi
maalumu wa kuandika na kutunza mikataba, takwimu, kumbukumbu na nyaraka zote za
Dola ya Kiislamu Madinah.
6.
Kuandaa Ummah wa Kiislamu Kijeshi na
Kiusalama.
- Mtume (s.a.w)
aliwaanda na kuwahimiza waislamu kuwa wakakamavu na hodari katika shabaha,
mieleka na kutumia silaha.
- Kila Muislam
alikuwa mpiganaji na mpelelezi dhidi ya maadui wa waislamu na Dola ya Kiislamu.
Rejea Qur’an(4:71).
- Aliunda na
kuweka vikosi vya doria na ulinzi kuzunguka mipaka ya Dola ya Kiislamu Madinah.
Qur’an(8:26).
7.
Kuimarisha Uchumi.
- Mtume (s.a.w)
aliwahimiza waislam kufanya kazi kwa bidii ili kujiimarisha Kiuchumi na
kuendeleza Dola.
- Utoaji wa
Zaka, Sadaka na mapato mengine yalihimizwa na kukusanywa Kijamii na kuboresha
huduma za jamii. Rejea Qur’an(22:41).
§
Mafunzo
yatokanayo na Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah.
Kutokana na mambo ya msingi aliyoyafanya Mtume (s.a.w) katika kuanzisha
Dola ya Kiislamu Madinah tunajifunza yafuatayo;
1.
Hatunabudi kuanzisha na kuendesha vituo vya harakati,
msikiti ukiwa ndio kitovu cha msingi.
2.
Mshikamano, kuhurumiana na kupendana kwa vitendo baina
ya waislamu ndio nyenzo pekee katika kuhuisha na kuendeleza harakati za
Kiislamu.
3.
Hatunabudi kuishi vizuri, kuwahesimu na kuwatendea
haki, wasiokuwa waislamu hasa wale wasiopiga vita waislamu na Uislamu wazi
wazi.
4.
Ni wajibu kwa kila muislamu kuwa mkakamavu, jasiri na
kujifunza mafunzo ya kijeshi na kuwa tayari kulinda na kuupigania Uislamu
katika jamii.
5.
Hatunabudi kuwajua vema maadui wa Uislamu na Waislamu,
mbinu na silaha zao na kuchukua tahadhari dhidi yao.
6.
Ni wajibu kuimarisha uchumi wetu kwani ndio nyenzo
muhimu na ya msingi katika kuendesha harakati za Kiislamu.
7.
Uongozi bora, makini na uwajibikaji wa kila mmoja
kulingana nafasi yake ndio kiungo muhimu katika kuendesha harakati za Kiislamu.
8.2. Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Madinah.
§ Mfumo wa Mapato na Uchumi katika Dola
(Serikali) ya Kiislamu Madinah.
Dola (Serikali) ya Kiislamu Madinah ilipata mapato yake
kupitia njia zifuatazo;
1. Zaka na Sadaka ndio ilikuwa njia kuu ya
kukusanya mapato ya serikali (Dola) ya Kiislamu iliyowahusu waislamu wote wenye
uwezo.
2. Jizya – Ni kodi waliokuwa wanalipa
wasiokuwa waislamu wanaume tu wenye uwezo wa kuwa askari kwa ajili ya ulinzi wa
Dola.
3. Al-Kharaj – Ni kodi waliolipa wasiokuwa
waislamu, walio na mashamba katika Dola ya Kiislamu.
4. Al-fay – Ni mapato yanayotokana na
mashamba ya Serikali (Dola) ya Kiislamu Madinah.
5. Al-Ghanimah (Ngawira) – Ni mapato
yanayotokana na mali ilitekwa katika vita, iliyolipwa 1/5
ya mali yote ilyotekwa.
6. Ushr – Ni kodi (ushuru) iliyotolewa na
waislamu wenye ardhi katika Serikali (Dola) ya Kiislamu kwa kiwango cha 10% kwa
maji ya asili (mvua) na 5% kwa maji ya kumwagilia.
7. Zaraib – Ilikuwa ni kodi zilizotozwa na
serikali (Dola) ya Kiislamu kwa muda kwa ajili ya maslahi ya nchi.
§ Msonge wa Uongozi na Siasa katika serikali (Dola)
ya Kiislamu Madinah.
Tofauti na serikali zingine, serikali ya Kiislamu ilijengwa katika
misingi mikuu mitatu; Tawhiid, Utume na Ukhalifa (nafasi ya mwanaadamu hapa
ulimwenguni). Rejea Qur’an(30:20), (3:189), (12:40), (7:54), (4:80), (4:65),
(24:55), (2:30).
Mgawanyo na msonge wa uongozi
wa Dola ya Kiislamu ulikuwa kama ifuatavyo;
- Qur’an– ilikuwa ndio Katiba kuu
(Constitution) ya kuongozea Dola iliyotafsiriwa kivitendo (Sunnah) na Mtume
(s.a.w) mwenyewe.
- Mtume (s.a.w.) – alikuwa ndio kiongozi
na amiri jeshi mkuu (commander in chief) wa Dola ya Kiislamu aliyesimamia na
kuendesha kazi zote za Dola ambapo Msikiti ulikuwa ndio Ikulu ya Dola (State
House).
- Shura (Cabinet) – Mtume (s.a.w) aliteua
washauri wake wakuu wakaribu, weledi na wazoefu (Baraza la Mawaziri) katika
shughuli zote za kuongoza Dola ambao ni Abu Bakr (r.a), Umar bin Khattab (r.a),
Uthman bin Affan (r.a), Ally bin Abu Twalib (r.a) na Hamza bin Abdul-Muttalib
(r.a) na wengineo.
- Sekretarieti (Secretarial) – Mtume
(s.a.w) aliteua jopo la waandishi na watunza kumbukumbu na nyaraka zote za
serikali.
- Wali au Gavana – Walikuwa ni wakuu wa
majimbo (mikoa) ambao waliteuliwa na Mtume (s.a.w) ili kuhakikisha sheria na
haki zinatekelezwa ipasavyo katika majimbo yao.
- Amil – Walikuwa ni wakusanyaji wa Zaka
na Sadaka walioteuliwa na Mtume (s.a.w) kila jimbo la Dola ya Kiislamu.
- Kadhi – Mtume (s.a.w) alikuwa ndiye
Jaji mkuu wa Dola ya Kiislamu na aliteua Kadhi (Jaji) kila jimbo (mkoa)
aliyesimamia haki na hukumu zote kwa mujibu wa Qur’anna Hadith.
§ Mfumo wa Ulinzi na Usalama katika Dola ya
Kiislamu Madinah.
Dola (serikali) ya Kiislamu Madinah iliposimama na kuanza kazi za
kuongoza jamii iliandamwa na maadui wa kila aina. Mtume (s.a.w) aliweka
mikakati na mbinu madhubuti za kuilinda na kuihami serikali yake ikiwa ni
pamoja na;
i.
Misafara ya Kujihami (Patrol) na Upelelezi.
Mtume (s.a.w) aliweka watu maalum kwa ajili ya kulinda mipaka ya Dola na
kupeleleza harakati za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu.Rejea Qur’an(4:71).
ii.
Kuweka Mikataba ya amani.
Mtume (s.a.w) aliweka mikataba ya amani na makabila ambayo hayakusilimu
yaliyopembezoni mwa Dola ya Kiislamu kama, Banu Dumra, Mudlaj, n.k. Rejea Qur’an(9:13-15).
iii.
Kupigana vita.
Njia hii ililazimika kutumika baada ya kuzidi uonevu, dhuluma na choko
choko za wazi dhidi ya Waislamu na Uislamu.Rejea Qur’an(2:193), (9:111) na
(9:29)
iv.
Sera ya wazi juu ya wanafiki.
Mtume (s.a.w) alichukua tahadhari na hatua dhidi ya wanafiki waliojidhihirisha
wazi kutengana na ummah wa waislamu kwa kuwatenga.Rejea Qur’an(9:73), (9:84) na
(9:80).
v.
Sera ya Uislamu juu ya amani.
Mtume (s.a.w) alitekeleza na kuelekeza mafundisho ya Uislamu juu ya
kutunza na kulinda amani kama fursa na dhamana katika kueneza Uislamu. Rejea Qur’an(8:61), (16:90), (2:84), (8:5-8).
vi.
Uhusiano wa Kiplomasia na nchi za nje.
Mtume (s.a.w) aliweka sera ya wazi juu ya uandikashaji na utekelezaji wa
mikataba mbali mbali na maadui wa Uislamu kama Aqaba, Hudaybiyah, n.k. Rejea Qur’an(5:8), (42:40-42), (60:8).
§ Madhumuni ya Dola ya Kiislamu.
1.
Kujenga maisha ya mwanaadamu yaliyo katika misingi ya (Tawhiid)
Ucha-Mungu na matendo mema.
2.
Kuondosha uovu, dhuluma,ukandamizaji,maasi,ukatili,
tabaka, unyonyaji, uonevu, n.k katika jamii. Qur’an(57:25).
3.
Kutumia mamlaka katika kusimamia na kuendeleza maadili
katika maisha ya jamii. Qur’an(22:25).
4.
Kusimamia na kulinda haki na uadilifu kwa wanaadamu
wote na viumbe wengine.
8.3. Upinzani dhidi ya Dola ya Kiislamu Madinah.
§ Maadui wakubwa wa Dola ya Kiislamu Madinah.
Kwa kipindi cha miaka 10 ya uongozi wa Mtume (s.a.w) maadui walioibuka
kupambana na Dola ya Kiislamu walikuwa;
o
Makafiri wa Kabila la Kiquraish.
o
Wanafiki.
o
Mayahudi
o
Warumi (Wakristo).
o
Makabila mengine ya Kiarabu
§ Mbinu na njia walizotumia maadui wa Uislamu
dhidi ya Waislamu na Dola ya Kiislamu Madinah.
Rejea Kitabu cha 3, EDK – Shule za Sekondari; Uk. 250 -
352.
o
Makafiri
wa Kiquraish.
- Walivamia mji wa
Madinah na kupora mifugo na kuipeleka Makkah.
- Walimwandikia
barua kwa kiongozi wa wanafiki Abdullah bin Ubayyi kumtaka wamfukuze Mtume
(s.a.w) kutoka mji wa Madinah.
- Kuwatishia
vita makabila yaliyokuwa yakiishi kati ya Makkah na Madinah yawe dhidi ya
Uislamu na wasijekusilimu.
- Walichoma moto
mashamba ya mitende ya waislamu Madinah.
- Walimchoma mkuki
Zainabu bint Muhammad (s.a.w) wakati akielekea Madinah.
o
Wanafiki.
- Walikuwa wanatoa
nyudhuru za uongo kuepuka jukumu la kupigana jihadi.
- Walimzulia
uzinifu mke wa Mtume (s.a.w) Aisha (r.a) kuwa amezini na sahaba Safwan (r.a) wakati
wa kurudi msafara wa Banu Mustaliq.
- Walijenga
msikiti wao kama kichaka cha kupiga vita Uislamu na kutaka kumuua Mtume
(s.a.w).
- Walishirikiana na
maadui wengine wa Uislamu ili kuupiga vita Uislamu.
- Walijitenga
wanafiki 300 katika vita vya Uhudi na kuwaacha waislamu 700 Waliopambana na
maadui wa Kiquraish 3,000 waliojizatiti kivita.
- Walichochea
ugomvi baina ya Muhajirina na Answar na kutishia kumfukuza Mtume (s.a.w)
Madinah wakiongozwa na Abdullah bin Ubayyi katika msafara wa vita vya Banu
Mustaliq.
o Mayahudi.
-
Walishirikiana na wanafiki katika kuwatia wasi wasi waislamu walipobadilishiwa Qibla
kutoka Jerusalemu na kuelekea Al-Kaaba, Makkah.
- Walitangaza kuwa Mtume (s.a.w) ni mtume wa
uongo.
- Waliifanyia Qur’anstihizai (mzaha). Rejea Qur’an(2:245), (3:181).
- Wamjaribu
Mtume (s.a.w) kwa kumuuliza maswali ya kubabaisha yasiyo na majibu ya dhahiri,
kama vile:
·
Usingizi wako ukoje.
·
Ni vitu gani Israil (Nabii Yaaqub)
alijiharamishia mwenyewe.
·
Ni malaika yupi anakuletea wahayi, n.k.
- Kuwavunja moyo na kuwadhalilisha waislamu.
- Walishirikiana
na Wanafiki kwa njama za kutaka kumuua Mtume (s.a.w) na kuuhilikisha Uislamu.
- Walivunja na
kusaliti mikataba ya amani waliowekeana na Mtume (s.a.w).
- Walichochea
fitina baina ya Answar kwa kuwakumbushia ugomvi wao wa zamani baina ya Aus na
Khazraj. Rejea Qur’an(3:100-101).
o
Warumi
(Wakristo).
- Gavana,
Shurahbil bin Amr Ghassaany wa Dola ya Kirumi alimuua mjumbe wa Mtume (s.a.w), Haarith
Bin Umair Al-Az katika mji wa Muttah.
·
Mtume (s.a.w) alituma jeshi la askari 3,000
kupambana na jeshi la Kirumi lenye askari 100,000.
·
Mtume (s.a.w) alichagua makamanda watatu, ambao
ni Zaid bin Harith (r.a), Ja’afar bin Abi Twalib (r.a) na Abdullah bin Rawahah
(r.a) na kuwaagiza kuwa akiuawa moja anayefuatia achukue nafasi na wakiuawa
wote basi wamchague miongoni mwao aongoze jeshi.
·
Makamanda wote 3 waliuawa na hatimaye
walimchagua Kamanda Khalid bin Walid (r.a) aliyeoongoza jeshi kishujaa na
kupelekea kupata ushindi.
·
Kutokana na ushujaa walioonyesha waislamu katika
vita vya Muttah, Warumi walipata woga na kulikimbia jeshi la waislamu katika
msafara wa Tabuuk.
·
Kuwashinda Warumi kulipelekea Dola ya Kiislamu
kuwa Super Power ya Ulimwengu wakati wa Mtume (s.a.w) na ndio kutimia lengo la
kuletwa kwake. Rejea Qur’an(48:28).
o
Makabila
mengine ya Waarabu.
- Mtume
(s.a.w) alilishughulikia na kulitia adabu kila kabila la Kiarabu lililojaribu
kuleta choko choko dhidi ya Dola ya Kiislamu.
- Makabila ya
Taif ya Bani Thaqif na Bani Hawazin yaliyokuwa na nguvu kijeshi, Mtume (s.a.w)
aliyasambaratisha katika vita vya Hunain akiwa na askari 12,000, baada ya Fat-h Makkah mwaka wa 8 A.H.
·
Katika vita vya Hunain, Mwenyezi Mungu (s.w)
aliwaacha Waislamu wapate fundisho kwanza, kwa kupata kipigo kutoka kwa maadui.
·
Mwenyezi Mungu (s.w), aliwaonesha waislamu kuwa,
ushindi wao haupatikani kwa wingi na ubora wa silaha zao tu, bali kwa msaada
wake.
·
Baada ya fundisho hilo, waislamu walipata ushindi
wa kishindo baada ya Mwenyezi Mungu (s.w) kushushia Malaika.
·
Waislamu walipata ushindi na kuchukua ngawira
mbali mbali zikiwemo;
-
Ngamia 24,000
-
Kondoo 40,000
-
Aqyyah (fedha taslim) 4,000/=
-
Mateka 6,000
“Bila shaka Mwenyezi Mungu
amekunusuruni katika mapigano mengi, na siku ya Hunayni (pia); ambapo wingi
wenu ulikupandisheni kichwa, lakini haukukufaeni chochote, na ardhi ikawa dhiki
juu yenu; ingawa ilikuwa yenye wasaa, kisha mkageuka mkarudi nyuma (mnakimbia).
Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume Wake na juu ya
walioamini. Na akateremsha majeshi (ya Malaika) ambayo hamkuyaona, na
akawaadhibu wale waliokufuru; na hayo ndiyo malipo ya makafiri.” (9:25-26).
§ Vita vya Badri.
- Vilikuwa
ndio vita vya kwanza vya jihad vilivyopiganwa siku ya Ijumaa mwezi 17 Ramadhani,
mwaka wa 2 A.H (624 A.D) katika bonde la Badri.
- Chanzo cha
vita ni kuwa mtume (s.a.w) alikusudia kuuzuia msafara wa Maquraish wa Makkah uliotokea
Syria (Sham) uliosheheni bidhaa zenye thamani ya dinar 50,000 kwa ajili ya
maandalizi ya kuupiga vita Uislamu na Waislamu.
- Mtume
(s.a.w) alikuwa na askari 313, ngamia 70 na farasi 2 tu na Makafiri wa
Kiquraish wakiwa askari 1000 waliojizatiti kivita, ngamia 700 na farasi 300.
- Waislamu
walipata ushindi kwa waliuawa Maqurish 70 wengi wao wakiwa vigogo wa Makkah na
waislamu 14 tu waliuawa.
Rejea Qur’an(3:123-124),
(8:9-11), (54:45), (8:65), (8:17) na (8:48).
Mafunzo
kutokana na Vita vya Badri.
1.
Ushindi wa waislamu katika vita unatoka kwa Mwenyezi
Mungu (s.w) na sio kutokana na ubora wa silaha na wingi wa askari.Rejea Qur’an(3:123-124),
(8:42-45).
2.
Tunajifunza pia namna ya kuwafanyia mateka wa kivita
ikiwa ni pamoja na;
- Kuwapatia haki na huduma zote
msingi za kimaisha, kibinaadamu na kiutu.
- Kuwalea na kuwafanyia wema na
uadilifu kama wanafamilia wengine.
- Kwa mateka wanaoweza kuleta
madhara kwa waislamu na Uislamu, ni bora
kuuawa badala ya kuachwa huru
kwa kujikomboa. Rejea Qur’an(8:67-69).
3.
Mwenyezi Mungu (s.w) aliwaadhibu makafiri na kuwanusuru
waislamu katika vita vya Badri na hawakuadhibu walipokuwa Makkah kwa sababu
walikuwa pamoja na Mtume (s.a.w) na pia walipewa muda wa kutubia. Rejea Qur’an(8:32-34) na (8:19).
4.
Tunajifunza pia, inafaa nguvu ya kivita kutumika
ikibidi katika kuzuia na kuondoa uovu, udhalimu, uonevu na choko choko za
maadui. Rejea Qur’an(8:60) na (60:8-9).
5.
Tunajifunza pia, Uislamu bila ya juhudi za kweli kufanyika
na kumwagika damu na kujitoa muhanga ipasavyo, hautasimama katika jamii.
6.
Choko choko na mbinu za maadui dhidi ya Uislamu na
waislamu ni zenye kuendelea na hazitaisha kamwe hadi siku ya Qiyama.
§ Vita vya Uhudi.
- Sababu ya
kutokea vita vya Uhudi ni Maquraish kutaka kulipiza kisasi dhidi ya waislamu
baada ya kushindwa katika vita vya Badri.
- Maquraish
waliandaa msafara wa biashara wenye thamani ya Dirham 300,000 kuelekea Iraq
kama maandalizi ya kulipiza kisasi vita vya Badri.
- Kikosi cha
waislamu kikiongozwa na Zaid bin Harith (r.a) kiliteka msafara huo na kuchukua
mali yenye thamani ya Dirham 100,000 na mateka 2.
- Vita
vilipiganwa siku ya Jumamosi, mwezi 15 Shawwal, mwaka wa 3 A.H (625 A.D) katika
milima ya Uhudi nje ya mji wa Madinah.
- Waislamu
walikuwa 700 (baada ya wanafiki 300 kurudi nyuma wakiongozwa na Abdullah bin
Ubayyi) na Maquraish wakiwa askari 3,000 waliojizatiti kivita, (700 wamevaa
mavazi ya chuma), farasi 200 na ngamia 3,000.
- Kwa
waislamu kiongozi alikuwa Mtume (s.a.w) na kwa Maquraish viliongozwa na Hindu
bint Utbah mkewe Abu Sufyan.
- Mtume
(s.a.w) aliteuwa kikosi cha watu 50 wakiongozwa na Abdullah bin Jubeir kukaa
juu ya mlima ili kulinda kikosi cha maadui kikiongozwa na Khalid bin Walid.
- Vita
vilipoanza waislam walipata ushindi lakini baadae kugeuka kipigo baada ya
waislamu 43 kuondoka mlimani na kupelekea Mtume kuvunjwa meno 2.
- Waislamu 70
waliuuawa akiwemo shujaa Hamza bin Abdi Muttalib (r.a) aliyeuliwa na mtumwa Wahshi
bin Harbi aliyeandaliwa na Hindu bint Utbah.
Mafunzo
yatokanayo na Vita vya Uhudi.
1.
Lengo la maadui wa Uislamu na waislamu kupigana ni
kuwaangamiza wao, kuharibu miji yao na mali zao pia. Hivyo ni wajibu waislamu
kuwa na tahadhari muda wote kupambana na maadui wao.
2.
Kushauriana katika kupanga mambo ni jambo la busara
sana, kama alivyoshauriana Mtume (s.a.w) juu ya sehemu ya kupiganwa vita vya
Uhudi.
Rejea Qur’an(3:159) na (3:166-167).
3.
Tunajifunza pia ni wajibu waislamu kutumia mbinu,
ujuzi, uzoefu, na jitihada za kivita pamoja na kuwa wanapata msaada wa Mwenyezi
Mungu (s.w).Rejea Qur’an(8:60).
4.
Msaada wa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa waislamu unapatikana
pale tu waislamu watakapotii amri zake na wakapigania dini vilivyo.Rejea Qur’an(3:151-152).
5.
Kuvunja na kutotii amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake
hupelekea kutofikia mafanikio hata kama watajizatiti na kufanya jitihada
ipasavyo. Rejea Qur’an(3:152), (3:165)
na (33:36).
6.
Tunajifunza pia, makosa ya watu wachache yasipuuzwe na
kufumbiwa macho bali yarekebishwe kwani athari yake itasibu jamii nzima.Rejea Qur’an(8:25).
7.
Mwenyezi Mungu (s.w) anatukumbusha kuwa pepo
haipatikani kwa kutamani, lele mama na ushabiki bali, kufanya jitihada ya
kweli. Rejea Qur’an(3:142-150), (3:156-160) na (3:169-171).
8.
Msamaha na nusura ya Mwenyezi Mungu (s.w) upo karibu
kwa waislamu pindi watakapotubia na kurejea kwake na kupambana na maadui
ipasavyo.Rejea Qur’an(3:152-154), (3:166-167) na (3:139-141).
9.
Ushindi wa waislamu katika vita unatoka kwa Mwenyezi
Mungu (s.w) na sio kutokana na ubora wa silaha na wingi wa askari. Rejea Qur’an(3:123-124), (8:42-45).
10. Choko
choko na mbinu za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu ni zenye kuendelea na
hazitaisha kamwe hadi siku ya Qiyama.
§ Vita vya Ahzab
- Maquraish
waliungana na mayahudi, wanafiki na makabila mengine ya waarabu baada ya kuona
kuwa wao peke yao hawawezi kuufuta Uislamu.
- Makafiri
wakiwa 10,000 waliojizatiti kivita mwaka wa 5 A.H. kwa ajili ya kuivamia
Madinah na waislamu wakiwa askari 3,000 tu na dhaifu kwa njaa.
- Waislamu
kupitia rain a ushauri wa Salman Al-Farsy walibuni kuchimba handaki lenye upana
yadi 5 na kina yadi 5 kuzunguka mji wa Madinah.
- Maadui
walipozingira, walishindwa kuruka handaki na wakawa wamezingira mji wa Madinah
kwa muda wa mwezi 1.
- Waislamu
walipata dhiki kubwa ya njaa siku 3 na zaidi na huku wakiendelea kuchimba
mtaro.
- Waislamu
walishinda kwa kupata nusura kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) baada ya kuletwa
mvua na upepo mkali uliowakimbiza maadui. Rejea Qur’an(33:9-15), (33:25).
Mafunzo yatokanayo na vita vya
Ahzab (Handaki).
1.
Kushauriana katika kupanga mambo ni jambo la busara
sana, kama alivyoshauriana Mtume (s.a.w) juu ya sehemu ya kupiganwa vita vya
Uhudi.
Rejea Qur’an(3:159) na (3:166-167).
2.
Tunajifunza pia ni wajibu waislamu kutumia mbinu,
ujuzi, uzoefu, na jitihada za kivita pamoja na kuwa wanapata msaada wa Mwenyezi
Mungu (s.w). Rejea Qur’an(8:60).
3.
Msamaha na nusura ya Mwenyezi Mungu (s.w) upo karibu
kwa waislamu pindi watakapotubia na kurejea kwake na kupambana na maadui
ipasavyo.
Rejea Qur’an(3:152-154), (3:166-167) na (3:139-141).
4.
Ushindi wa waislamu katika vita unatoka kwa Mwenyezi
Mungu (s.w) na sio kutokana na ubora wa silaha na wingi wa askari. Rejea Qur’an(3:123-124), (8:42-45).
5.
Choko choko na mbinu za maadui dhidi ya Uislamu na
waislamu ni zenye kuendelea na hazitaisha kamwe hadi siku ya Qiyama.
8.4.
Mkataba wa Hudaibiyah.
- Ni mkataba wa amani baina ya
waislamu na Maquraish wa Makkah, mwaka wa 6 A.H, Dhul-Qa’adah (Machi, 628 A.D) katika
kitongoji cha Hudaybiyah karibu na
Mji wa Makkah.
- Mkataba
ulitiwa saini na Mtume (s.a.w) kwa niaba ya waislamu na Suhail bin Amri
Kwa niaba ya Makafiri
wa Kiquraish.
§ Yaliyopelekea kutokea kwa Mkataba wa
Hudaybiyah.
- ilikuwa Mtume (s.a.w) kutimiza ndoto
(wahay) aliyoota mwaka 6 A.H. kuwa kuna siku atafanya ‘Umrah’.
- Mtume (s.a.w) akiwa na waislamu 1,400
walikwenda kufanya ibada ya ‘Umrah’ lakini walizuiliwa na Maquraish katika
kitongoji cha Hudaibiyah wasiingie Makkah.
- Mtume (s.a.w) alituma wajumbe 2, mmoja
baada ya mwingine ili kuwaomba Maquraish wawaruhusu waingie Makkah, lakini
walikataliwa.
- Mtume (s.a.w) alituma mjumbe wa 3,
‘Uthman bin Affan’ (r.a) aliyeshikiliwa na Maquraish kwa muda, na kuja tetesi
kuwa ameuawa.
- Mtume (s.a.w) aliwakusanya waumini
chini ya mti na kuchukua kiapo cha utii (Bai’at) juu ya kulipiza kisasi cha
‘Uthman bin Affan’ (r.a), lakini baadaye alirejea.
Rejea Qur’an(48:18).
- Maquraish kwa kuwaogopa waislamu,
walimuomba Mtume (s.a.w) kuweka mkataba wa amani na Mtume (s.a.w) alikubali, na
ukaitwa “Mkataba wa Hudaybiyah”.
Rejea Qur’an(48:1).
§ Vipengele vya Mkataba wa Hudaybiyah.
1.
Waislamu warudi Madinah bila kufanya ‘Umrah’.
2.
Waislamu wanaweza kurudi mwakani (7 A.H) kufanya
‘Umrah’ lakini wakae siku tatu.
3.
Wakija Makkah wasije na silaha ila panga zikiwa ndani
yah ala zao.
4.
Waislamu hawataenda nao Madinah waislamu wanaoishi
Makkah na wala hawatamzuia yeyote miongoni mwao anayetaka kubakia Makkah.
5.
Kama yeyote wa Makkah atatoroka kwenda kusilimu,
Waislamu hawana budi kumrudisha (wasimpokee), lakini yeyote kutoka Madinah
akitoroka kwenda Makkah kuritadi, Maquraish hawatapaswa kumrudisha Madinah
(watampokea).
6.
Makabila ya Waarabu yatakuwa huru kufanya Itifaki
(urafiki) na upande wowote ule yanaoupendelea.
7.
Pasiwe na vita kwa kipindi cha miaka 10 baina ya
waislamu na Maquraish na baina ya waitifaki (Allies) wa Waislamu na waitifaki
wa Maquraish.
8.
Hapana ruhusa ya kutengua hata sharti moja katika hizi
kabla ya miaka 10 kupita.
Mafunzo yatokanayo na Mkataba wa
Hudaybiyah.
1.
Ahadi ya Mwenyezi Mungu (s.w) siku zote ni ya kweli na
yenye kutimia, kama alivyotimiza ahadi kwa Mtume (s.a.w) alipoota kuwa siku 1
atakwenda ‘Umra’. Rejea Qur’an(48:27).
2.
Katika kusimamisha Uislamu, ni lazima pawepo na mbinu
na mipango maalumu ya muda mfupi na muda mrefu ili kufikia malengo yetu katika
nyanja yeyote ile.
Kama alivyofanya Mtume (s.a.w) katika mkataba wa Hudaibiyah:
- Kufuta ‘Bismillahir Rahmaanir Rahiim’,
- Kufuta ‘Muhammad Rasulullaah’.
- kukubali kipengele cha 4 na 5
ijapokuwa vilikuwa vinawadhalilisha waislamu.
Rejea Qur’an(48:18), (48:29) na (48:22).
3.
Waumini walipata maliwazo ya Mwenyezi Mungu (s.w) baada
ya kukata tamaa kutokana na uonevu wa baadhi ya vipengele vya Mkataba wa
Hudaibiyah. Rejea Qur’an(48:20-29) na
(48:1-8).
4.
Tunajifunza pia, ni wajibu kutekeleza mikataba
tuliyoandikiana hata ikiwa na Makafiri, kama alivyotekeleza Mtume (s.a.w)
mkataba wa Hudaybiyah. Rejea Qur’an(48:10) na (60:10-12).
5.
Ni wajibu kufikisha ujumbe wa Qur’ankwa wasio waislamu
na viongozi wao, kama alivyofanya Mtume (s.a.w) kwa kutuma mabalozi sehemu
mbali mbali.
6.
Mazingira ya amani na utulivu ni jambo la muhimu sana
katika kueneza na kuendeleza ujumbe wa Uislamu, hivyo mapatano ni bora zaidi
kuliko kupigana.
7.
Waislamu tuwe wepesi katika kutumia fursa
zinazopatikana na kupelekea kufikia malengo yetu ya kuusimamisha Uislamu katika
jamii.
8.
Tuwe tayari kupoteza maslahi madogo madogo katika
kutafuta fursa, mazingira na suluhu inayopelekea kufikia lengo kuu.
9.
Tuwe na uvumilivu na subira kwa kutotegemea matunda ya
kusimamisha Uislamu kupatikana haraka na bila ya misukosuko.
10. Nusura
na ushindi kwa waislamu hupatikana baada ya waislamu kufanya juhudi ya dhati
mwisho wa uwezo wao. Rejea Qur’an(48:1).
§ Matunda (ushindi) yatokanayo na Mkataba wa
Hudaybiyah.
1.
Waislamu walipata fursa ya kulingania Uislamu na watu
wengi walisilimu wakiwemo majemedari kama, Khalid bin Walid, Suhail bin Amr na
Amr bin Al-As na wengineo.
Rejea Qur’an(48:1).
2.
Kuhamia jangwani kikosi kilichosilimu na kuwa tishio
kwa misafara ya Maquraish, Maquraish walimuomba Mtume (s.a.w) kuondoa kipengele
kilichowakataza wanaosilimu Makka kwenda Madinah kilichokuwa kero kwa waislamu.
3.
Mtume na waislamu walipata fursa ya kuutangaza Uislamu
ndani na nje ya Bara Arabu kama vile, Mashariki ya kati, Misr, Uhabeshi na
Wafalme mbali mbali.
Rejea Qur’an(3:64).
4.
Waislamu walipata fursa ya kujiimarisha kiuchumi kwa
kufanya biashara hasa za masafa ya mbali kwa amani na falme za nje ya Bara
Arab.
5.
Waislamu waliweza kujizatiti kijeshi na kuweza
kuwadhibiti maadui wa Uislamu na waislamu katika mapigano mbali mbali kama;
- Wayahudi (Warumi) katika vita vya Khaibar na Muttah mwaka wa 7
A.H.
- Ushujaa wa waislamu yalisababisha maadui kuwakimbia msafara wa
Tabuuk.
6.
Mtume (s.a.w) akiwa na waislamu 2,000 walifanikiwa
kufanya Umrah mwaka wa 7 A.H (badala ya wale 1,400 waliorudishwa 6 A.H.) na
kutimiza ndoto yake ya ushindi. Rejea Qur’an(48:27).
7.
Fat-h Makkah
– kilele cha ushindi, baada ya Maquraish na Waitifaki wao kuvunja mkataba wa
Hudaybiyah baada ya muda wa miaka 2 tu, na Mtume alitumia fursa hii kuikomboa
Makkah bila vita.
§ Fat-h Makkah (Kukombolewa Makkah).
- Mtume
(s.a.w) aliandaa askari 10,000 mwezi 10 Ramadhani, 8 A.H (Januari 1, 630 A.D)
kuelekea Makkah.
- Kukombolewa
Makkah kulipelekea kusilimu Abu Sufyan na viongozi wengine wa Makka na kuwa
kishawishi kusilimu watu na makabila mengi pia.
- Baada ya
Fat-h Makka, waislamu waliyashinda makabila ya Waarabu yenye nguvu kama; Banu
Thaqif na Banu Hawazin katika vita vya Hunain.
Rejea Qur’an(17:81).
- Dola ya
Kiislamu chini ya uongozi wa Mtume (s.a.w) ilienea Bara Arab nzima na
aliigawanya katika majimbo na kuteuwa Walii, Kadhi na Amil kama viongozi kwa
kila jimbo.
8.5. Hija ya Kuaga na Kutawafu kwa Mtume
(s.a.w).
- Ilikuwa mwaka wa 10 A.H alikwenda
kuhiji na Waislamu zaidi ya 100,000 baada ya kutimia miaka 23 ya Utume. Rejea Qur’an(5:3).
- Mtume (s.a.w) mwezi 9 Dhul-Hija, 10 A.H
akiwa Viwanja vya Arafa, alikhutubia waislamu akiwa juu ya ngamia.
- Mtume (s.a.w) alianza kuugua miezi
miwili baada ya Hija ya Kuaga na hatimaye alifariki jioni siku ya Jumatatu
mwezi 12 Rabi’al-Awwal, 11 A.H.(Juni 8, 632 A.D.) akiwa na umri wa miaka 63.
***************************************
==================================
Wabillah Tawfiiq