Main Categories
TB

Books and Notes

Vitabu vya TIE na Notes zote

PP

Past Papers

Standard One hadi Form Six

WA

WhatsApp Channel

Jiunge kwa updates

← Back Home
Tie Books & Notes List
← Back Home
Past Papers List
← Back

Business Studies Form Two Monthly Test February 2026

 BUSINESS STUDIES EXAM PDF

Join WhatsApp Channel

Form 4 Monthly Test 2026 Kagera

 AGRICULTURE F4 2026.pdf

AGRICULTURE FORM FOUR MARKING SCHEME.pdf

BASIC MATHEMATICS F4 ,JANUARY 2026.pdf

BASIC MATHEMATICS FORM FOUR ,MARKING SCHEME.pdf

bios f4 monthy exams.pdf

BIOS F4REGIONAL MARKING SCHEME.pdf

CIVICS F4 MONTHLY TEST.pdf

CIVICS F4 MS.pdf

COMMERCE F4.pdf

COMMERCE MARKING SCHEME.pdf

ENGLISH F4 MS.pdf

ENGLISH FORM FOUR JANUARY TEST.pdf

FINE ART 1 F 4 JAN, KAGERA REGION 2026.pdf

GEOGRAPHY FORM FOUR .pdf

GEOGRAPHY FORM FOUR MARKING SCHEME.pdf

Literature FIV MS.pdf

Literature FIV Examination.pdf

MTIHANI WA KISWAHILI.pdf

Join WhatsApp Channel

Biology Form Two Monthly Test 2026 Uru Minor Seminary

 DOWNLOAD PDF

Join WhatsApp Channel

Kagera Form Two Monthly Test 2026

 Agriculture F2.pdf

AGRICULTURE F2 MS.pdf

Join WhatsApp Channel

Msalala Dc Form 1 Mock Exam 2026 English

 DOWNLOAD PDF

Join WhatsApp Channel

Janeth Magufuli Girls Form Six English Language Opening Exam 2026

 PDF PAPER 1

PDF PAPER 2

Join WhatsApp Channel

History Pre Necta Open Exam 2026 Form Six

 DOWNLOAD PDF

Join WhatsApp Channel

Kwemaramba Form 6 Fitness Exam 2026

 

F6 Internal Exams-JAN-2026 (KSS) P1

F6 Internal Exams-JAN-2026 (KSS) P2
Join WhatsApp Channel

Class Four Exam 2026 Shinyanga

 


ENGLISH - STD 4.pdf

                 HISABATI - STD 4.pdf

JIOGRAFIA NA MAZINGIRA - STD 4.pdf

KISWAHILI - STD 4.pdf

Join WhatsApp Channel

Bethlehem and Mikiga School Chemistry Form Two Inter Competition Exam 2026

 DOWNLOAD PDF

Join WhatsApp Channel

Chemba Dc Darasa la Saba Pre Mock 2026

 DOWNLOAD PDF

Join WhatsApp Channel

STD 7 Mock 1 Examination 2026 Shinyanga

 

ENGLISH & SWAHILI MEDIUM

STD 7 KISWAHILI.pdf

CIVIC AND MORAL STD 7.pdf

ENGLISH.pdf

HISABATI STD 7.pdf

MAARIFA YA JAMII STD 7.pdf

MATHEMATICS STD 7.pdf

SAYANSI STD 7.pdf

SCIENCE STD 7.pdf

STD 7 SOCIAL STUDIES.pdf

URAIA NA MAADILI STD 7.pdf
Join WhatsApp Channel

Chogo Secondary Form Three Chemistry Weekly Test 2026 - Hardness of Water

 DOWNLOAD PDF

Join WhatsApp Channel

FORM 2 BIOLOGY CHAMWINO WEEKLY TEST 2026 FEBRUARY

BIOLOGY EXAM

BIOLOGY MS
Join WhatsApp Channel

Form Three Tie Books

 

Here’s a quick-access table for downloading the 2025 books:

SubjectView PDF

English Language

View PDF

Mathematics

View PDF

Physics

View PDF

Chemistry

View PDF

Biology

View PDF

Geography

View PDF

History

View PDF

Civics

View PDF

Kiswahili

View PDF

Commerce

View PDF

Book Keeping

View PDF

Agriculture

View PDF

Join WhatsApp Channel

History Form 4 Weekly Exam 2026 Chamwino Dc

 HISTORY EXAM PDF

HISTORY MS PDF

Join WhatsApp Channel

HTM FORM 2 WEWKLY TEST 2026 CHAMWINO DC

 DOWNLOAD PDF

Join WhatsApp Channel

Onical Secondary Geography Form Two Monthly Test 2026

GEOGRAPHY EXAM

GEOGRAPHY MS
Join WhatsApp Channel

Chamwino Form 4 Weekly Test February 2026 Biology

BIOLOGY EXAM

BIOLOGY MS
Join WhatsApp Channel

Physics Form Five Special Examination 2026 Dr Batilda Burian Girls School

Physics Form Five Special Examination 2026 Dr Batilda Burian Girls School

PHYSICS EXAM
Join WhatsApp Channel

NITEKELA Chemistry Form Two Weekly Examination 2026

 

CHEMISTRY EXAM

CHEMISTRY MS
Join WhatsApp Channel

Nukuu za Somo la EDK Kidato cha Nne

 SOMA HAPA

Join WhatsApp Channel

Form Two Topical Exam (Current) 2026 Manyunyu Girls

 DOWNLOAD PDF

Join WhatsApp Channel

Nukuu za Somo la EDK Kidato cha Tatu

Soma Nukuu za Somo la EDK Kidato cha Tatu kupitia App Yetu ya LusaElimu - Alika Ndugu, Marafiki na Wadau wa Elimu Kupata Notes Hizi Bure

SOMA HAPA

Join WhatsApp Channel

Nukuu za Edk Kidato cha Tatu

 

                                                                                

 


NUKUU ZA SOMO

 

ELIMU YA DINI YA KIISILAMU

 

KIDATO CHA TATU


 

MADA ZOTE ZA KIDATO CHA TATU

1.      DINI SAHIHI ANAYOSTAHIKI KUFUATA MWANUAADAMU.

Kulingana na umbile lake, mwanaadamu daima hutamani kuishi kwa furaha na amani ili kufikia lengo la kuumbwa, na hapo ndipo inambidi kuchagua dini (njia sahihi ya maisha) kati ya Uislamu, Ukafiri, Ushirikina au Utawa itakayomtimizia malengo yake.

1.1.    Sifa au Vigezo Vya dini sahihi

Dini sahihi ni ile inayomuwezesha mwanaadamu kuishi kwa furaha na amani ya kweli hapa Duniani na Akhera, na ni lazima iwe na sifa zifuatazo;

(a)   Dini sahihi lazima ieleze ukweli juu ya maumbile;

Ni lazima ieleze ukweli juu ya mwanaadamu, lengo la kuumbwa kwake, hadhi/nafasi yake, dhima/kazi yake na maumbile yanayomzunguka na viumbe vyote vilivyo hai na visivyo hai, na hatima ya kila kitu.

(b)   Dini sahihi ni lazima iwe na kanuni na sheria zinazoendana na maumbile yote;

Kanuni na sheria za dini sahihi ni lazima ziwe sambamba na kanuni za kimaumbile ili kuepusha mgongano wowote wa kimahitajio wa kimwili na kimazingira pia.

(c)   Ni lazima itosheleze mahitajio ya mwanaadamu ya kimwili na kiroho;

Pia ni wajibu kwa dini sahihi kuelekeza na kutosheleza hisia za mwanaadamu pindi anapokuwa na hali ya furaha au hali ya majonzi, namna ya kukabiliana nazo ili kubakia katika lengo lake la kuumbwa (maisha).

(d)   Dini sahihi pia lazima iwe ni mfumo wa maisha uliokamilika;

Dini sahihi haina budi kuwa na utaratibu kamili wa kila kipengele na Nyanja ya maisha ya kila siku kiuchumi, kisiasa, kiafya, kiutamaduni, kisheria, kielimu, n.k.

(e)   Pia dini sahihi ni lazima iwe na ibada maalum zinazombakisha mwanaadamu katika maadili na hadhi yake;

Ni wajibu kwa dini sahihi kuwa na muongozo wa kumuinua na kumbakisha mwanaadamu katika mwenendo mzuri wa kiroho (kiutu) unaoweza kuustawisha mwili na kuleta mahusiano mazuri ya kiutu yasiyo na chuki, husuda, tamaa, kiburi, vurugu, n.k.

(f)    Dini sahihi haina budi kuwa ya walimwengu wote na ya nyakati zote;

Ili kufikia lengo la kuumbwa mwanaadamu, dini sahihi ni lazima iwe inawahusu watu wa aina zote (wote), isiwe na jina la mtu au mahali na isiwe na mipaka ya kijiografia, rangi za watu, mahali, nyakati, n.k.

(g)   Dini sahihi ni lazima iainishe na kusimamia haki zote za mwanaadamu;

Ni wajibu kwa dini sahihi kutoa na kusimamia haki, hukumu na adhabu kwa usawa na uadilifu kwa watu wote kibinafsi na kijamii bila upendeleo na ubaguzi wowote wa kirangi, taifa, nasaba, cheo au hadhi.

 

1.2.    Kwa Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ? 

 Au

      Haja ya kuhitaji mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

Mwanaadamu pamoja na ujuzi na utundu alionao, hana uwezo wa kujiundia dini sahihi (mfumo sahihi wa maisha) utakaomfikisha na kumbakisha kwenye lengo la kuumbwa kwake. Na hii ni kutokana na sababu zifuatazo;

 

(a)   Mwanaadamu anaathiriwa na matashi ya kibinafsi;

Pamoja na ujuzi, utambuzi na vipawa alivyopewa mwanaadamu, bado uamuzi na fikra zake ziaathiriwa na matashi ya nafsi yake katika upendeleo, uonevu na chuki, hivyo hawezi kuunda mfumo utakaosimamia haki na uadilifu.

(b)   Nyenzo anazotumia mwanaadamu kujielimisha ni dhaifu;

Mwanaadamu hujielimisha kupitia nyenzo zifuatazo;

                                i.      Milango ya fahamu.

Kama vile pua, masikio, ulimi, macho, ngozi, n.k, ambavyo vyote vina udhaifu na mara nyingine hutoa taarifu zisizo na ukweli.

                              ii.      Akili na fikra.

Uamuzi wa mwanaadamu wa akili na fikra peke yake hauwezi kutoa jibu/mwongozo sahihi wa maisha kwani huathiriwa na wakati, matashi, mazingira, uelewa, upeo wa kufikiri na pia una kikomo. Rejea Qur’an(10:36,66), (25:43,45), (6:116) na (28:60)

                            iii.      Sayansi na Uchunguzi;

Sayansi na majaribio haviwezi kutumika kama nyenzo kuu ya kuunda muongozo sahihi kwani vyote hivyo vinategemea milango ya fahamu ambayo nayo ina madhaifu mengi na kikomo pia.

                            iv.      Historia;

Kutumia uzoefu wa kihistoria katika kuunda muongozo sahihi wa maisha ni dhaifu kwa sababu mwanaadamu huathiriwa na uzoefu na ujuzi wa awali na hivyo kutokubaliana na mabadiliko yeyote yatakayojitokeza. Rejea Qur’an(2:170, 257), (5:104) na (6:116).

 

1.3.    Sababu Ya Uislamu Kuwa Ndiyo Dini Sahihi Pekee.

Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kuchaguliwa na kufuatwa kama muongozo sahihi wa maisha na watu wote kwa sababu zifuatazo;

(a)   Uislamu unaeleza ukweli juu ya maumbile na nafasi ya mwanaadamu hapa Duniani;

Uislamu unaeleza lengo la kuumbwa mwanaadamu kuwa ni ibada na kumtumikia Mwenyezi Mungu na kuwa msimamizi wa sheria na hukumu zake hapa ulimwenguni ili kupata radhi zake.  Qur’an(51:56) na (2:29).

(b)   Sheria na kanuni za Uislamu zinaendana na kanuni za kimaumbile;

Uislamu ndiyo dini pekee inaenda na kuzingatia kanuni na taratibu zote za kimaumbile za kibailojia kifizikia na kikemia ya viumbe vyote vilivyo na visivyo hai ikiwa ni pamoja na maumbile au mazingira yanayotuzunguka.     Rejea Qur’an(3:83) na (30:30).

(c)   Uislamu ndio dini inayotosheleza matashi yote ya mwanaadamu kimwili na kiroho;

Uislamu ni dini inayotoa muongozo namna ya mtu kumiliki hisia zake na kuendea mambo katika hali tofauti tofauti kama vile wakati wa furaha, shida, huzuni, misiba, n.k.Rejea Qur’an(2:155-157).

(d)   Uislamu ni njia kamili ya maisha;

Ni Uislamu pekee ndio mfumo kamili wa maisha ya kila siku ya mwanaadamu katika fani na nyanja zote za kibinafsi na kijamii kama vile kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.

(e)   Uislamu una ibada maalum za kumjenga mwanaadamu kimaadili;

Uislamu umeweka muongozo katika kumuadilisha mwanaadamu kupitia ibada maalum kama vile swala, funga, hija, kutoa zakat na sadaqat na zinginezo za sunnah.

(f)    Uislamu ni dini ya walimwengu wote na wa nyakati zote;

Uislamu umekuwa ni mwongozo wa maisha tangu binaadamu wa kwanza hadi wa mwisho katika Nyanja zote za maisha bila kujali taifa, ukoo, rangi na hadhi ya watu.Rejea Qur’an(42:13).

(g)   Uislamu ni dini ya kusimamia haki, uadilifu na usawa;

Ni dini ya Uislamu ndiyo inayotoa na kusimamia kwa usawa na uadilifu haki, hukumu na adhabu zote kwa watu wote bila ya upendeleo na ubaguzi wa rangi, taifa, hadhi na ukoo.Rejea Qur’an(103:1-3), (9:33), (61:9) na (17:105).

 

1.4.   Maana ya Kusimamisha Uislamu katika jamii.

Ni pale ambapo waislamu katika jamii wataweza kuendesha kila kipengele cha maisha yao ya binafsi na jamii katika siasa, uchumi, utamaduni, n.k kwa kufuata kikamilifu muongozo wa Qur’anna Sunnah.    Rejeab Qur’an(3:83), (10:99), (32:13), (61:8) na (64:2).

 

1.5.   Umuhimu wa Jihad katika kusimamisha Uislamu katika jamii.

                          i.      Kusimamisha Uislamu (Jihad) katika jamii ni amri (faradh).

Kama ilivyoamrishwa swala, funga, zakat na hijja, Neno kutiba (mmelazimishwa) limetumika katika jihad kama lilivyotumika katika kufunga, kulipa kisasi na faradh zingine pia za kutekeleza Uislamu.  Rejea Qur’an(2:216), (2:183), (2:178,180) na (22:78).

 

                        ii.      Msamaha na Pepo hupatikana kwa kufanya juhudi (jihad) za maksudi katika kusimamisha Uislamu katika jamii.

Kutekeleza faradh kama swala, funga, zaka na hija na ibada zingine za sunnah za binfsi, itakuwa sio sababu ya msingi ya kupata msamaha na pepo ya Mungu, mpaka jitihada ya dhati katika kupigania Uislamu katika jamii ifanyike.  Rejea Qur’an(4:74), (9:111), (61:10-13), (2:154), (3:169-171), (3:142), (3:157), (2:214) na (9:16).

                                   

                      iii.      Mwenyezi Mungu (s.w) ameteremsha chuma (silaha) kuwa nyenzo ya kusimamisha Uislamu katika jamii.

Mitume wametumwa kusimamia haki na uadilifu katika jamii kwa kutumia miongozo ya vitabu vya Allah (s.w) na pia chuma (silaha) kimeteremshwa ili mitume na waumini wakitumie katika kusimamia haki na uadilifu ndani ya jamii.Rejea Qur’an(57:25).

 

                      iv.      Kusimamisha Uislamu katika jamii ndio lengo kuu la maisha ya Waumini.

Mwenyezi Mungu (s.w) ametubainishia kuwa chochote tutakachokipenda au tutakachokifanya nje na lengo la kusimamisha Uislamu katika jamii hatakuwa na radhi juu yetu. Rejea Qur’an (9:23-24).

 

1.6. Kwa nini ni muhimu Kusimamisha Uislamu katika jamii?                   

Ni muhimu Uislamu kusimama katika jamii ili matunda yafuatayo yapatikane;

                       i.            Waumini wataweza kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo kwa mujibu wa Qur’anna Sunnah kwa kila kipengele cha maisha ya kila siku binafsi na jamii katika siasa, uchumi, elimu, utamaduni kama wanavyotekeleza swala, funga, hija, n.k.  Rejea Qur’an(51:56), (2:21-22), (7:54), (9:31), (2:85), (2:208), (2:193), (4:75-76), (9:38), (8:39), (22:40) na (47:7).

                                                                 

                     ii.            Kupatikana amani ya kweli na kuondoka hofu na mashaka katika jamii. Hii ni baada ya waumini kuchukua hatamu ya uongozi katika jamii kwa mujibu wa muongozo na sheria za Mwenyezi Mungu (s.w).  Rejea Qur’an(57:25), (2:257) na (5:90-91).

 

                   iii.            Waumini wataweza kuamrisha mema na kukataza maovu kikamilifu katika jamii pasina kikwazo chochote pindi watakapochukua nafasi ya kuiongoza jamii.  Rejea Qur’an(22:41) na (3:110).

 

                   iv.            Kuikinga jamii na majanga mbali mbali. Waumini watakapochukua nafasi za kuiongoza jamii ndio itakuwa sababu ya kutoweka maovu ndani jamii ambayo ndio sababu ya kupatikana majanga katika jamii.  Rejea Qur’an(8:25).

 

2.      NGUZO ZA IMANI

2.1.   Kumuamini Mwenyezi Mungu (S.W).

§  Madai ya Makafiri dhidi ya uwepo wa Allah (s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.

Makafiri wa zamani na wa zama hizi wakiwemo Charles Darwin, Friedrich Engles, n.k wanadai kuwa imani ya uwepo wa Mungu Muumba dhana tu haina dalili yeyote. Miongoni mwa hoja (madai) zao wanazotoa ni hizi zifuatazo;

(a)    Mwenyezi Mungu hayupo kwa sababu haonekani na wala hadirikiki kwenye milango ya fahamu. Rejea Qur’an(17:90-92).

Milango ya fahamu kama vile macho katika kumuona, pua katika kumnusa,     masikio katika kumsikia, ngozi  katika kumhisi au kumgusa pia, n.k.

Udhaifu wa hoja hii,

Milango ya fahamu ina udhaifu mwingi sana na kikomo pia, kama vile macho au pua huweza kuona au kunusa vitu vilivyo karibu tu na visivyokuwa na kizuizi, kuna vitu vingi vinavyotuzunguka lakini hatuvioni kama upepo, sauti, n.k.

 

(b)   Mwenyezi Mungu amefanywa kuwepo na wanadamu kutokana fikra na mawazo duni na uduni wa maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Hii ni baada ya mwanaadamu kushindwa kutatua matatizo katika mazingira yake na hivyo kuibukia kujiundia miungu.

Udhaifu wa hoja hii,

Historia inaonyesha kuwa hakuna zama mwanaadamu aliishi bila ya ujuzi wa kukabiliana na mazingira yake, Mwanaadamu wa kwanza kuumbwa alipewa ujuzi (elimu) ya kukabilana na mazingira yake na hatimaye kushushiwa muongozo kamili wa maisha kutoka kwa Muumba wake.   Rejea Qur’an(2:31,38).

 

(c)    Hapana Mungu Muumba bali vitu vyote vimetokana na mabadiliko ya kimaada.

Wanadai kuwa maumbile na viumbe vyote vinatokana na mabadiliko kidogo kidogo ya kimaada (evolution) baada ya muda mrefu kupita kutoka hali moja kwenda nyingine. Mfano binaadamu kutoka pweza, mjusi, sokwe na hatimaye mtu kamili.

Udhaifu wa hoja hii,

Nadharia hii haina ushahidi wowote wa kisayansi, kiuchunguzi na utafti bali ni dhana tu aliyoibuni Darwin ili kupotosha uhalisia na ukweli juu ya chanzo cha maumbile. Hadi leo hii hakuna mwanasayansi yeyote anayeweza kuthibitisha nadharia hii. 

 

(d)   Kama Mungu Muumba yupo, ni ipi nasaba (ukoo) yake au ametokana na nini?

Makafiri wa zamani na sasa wanasingizia kutoamini kuwepo Mungu kwa kuwa hawajui nasaba, ukoo au asili yake anatokana na nani au na nini.

Udhaifu wa hoja hii,

Kwa kutumia mantiki, Muumba wa vitu vyote ndiye chanzo na asili ya vitu vyote.Hivyo ni lazima asiwe na nasaba, mwanzo au mwisho pia. Na asitokane na vitu au maumbile yale. Rejea Qur’an(112:1-4).

 

(e)    Vitu havikuumbwa bali vimetokea kwa bahati nasibu (by chance) na vitatoweka kwa bahati nasibu pia muda wake ukifika.

Makafiri wa zamani na sasa wanadai kuwa asili ya maumbile yote yametokana na bahati nasibu (by chance), hivyo vitatoweka kama vilivyoibuka.

Udhaifu wa dai hili,

Hakuna uwezekano wa kuwepo maumbile bila ya Muumbaji na msimamizi mwenye ujuzi na uwezo wa hali ya juu na mtegemewa wa kila kitu, kwani  kila kitu kinachoonekana kimeumbwa na kimewekwa kwa lengo maalum.

 

§  Kuamini Mwenyezi Mungu Sio Suala La Kibubusa Au Kufuata Mkumbo.

Makafiri wanadai kuwa kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) ni ububusa na kufuata mkumbo bila ya udadisi na kutumia akili. Dai hili sio la kweli kwa sababu zifuatazo;

Kwanza, Mwenyezi Mungu (s.w) ametuma Mitume mbali mbali kwa wanadamu ili kuwafundisha na kutoa dalili za kuwepo kwake bila ya shaka yeyote kwa dalili za wazi ili kumfahamu na kuweza kumuabudu ipasavyo.   Rejea Qur’an(4:165).

 

Pili, Vipawa, ufahamu na akili alivyopewa mwanaadamu ni kumuwezesha kumtambua Muumba wake na kuweza kumuabudu inavyostahiki. Hivyo kutotumia akili katika kumtambua Mwenyezi Mungu kupitia ishara mbali mbali ni kustahiki adhabu.   Rejea Qur’an(3:190), (30:21), (7:179), (8:22) na (12:105).

 

Tatu, Mitume wa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwafundisha wafuasi wao juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu, hawakuwataka kuamini na kufuata bila ya hoja na dalili za wazi bali walionyesha ishara na miujiza kuthibitisha ujumbe wao.

 

Nne, Msisitizo wa Elimu katika Qur’ankuwa faradhi ya kwanza kama nyenzo pekee ya kumuwezesha mwanaadamu kumjua na kumuabudu Mola wake na kuweza kuyamudu mazingira yanayomzunguka na kuweza kusimamisha Ukhalifa ardhini.

 

Tano, Maana ya neno “imani” ambalo lina maana ya ‘kuwa na yakini moyoni pasina shaka’ yeyote juu ya jambo fulani kwa kuwa na ujuzi nalo na pia kupitia dalili na ishara za kutosha za kuonyesha kuwepo kwake.

 

§  Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S.W).

Dalili nyingi zimedhihirishwa ndani ya Qur’ankatika maeneo makuu matano ambamo uchunguzi wa kina na kutafakari vikifanyika vilivyo mtu atayakinisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) pasina shaka yeyote. Maeneo hayo ni haya yafuatayo;

1.      Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.

2.      Nafsi (Dhati) ya mwanaadamu.

3.      Historia ya mwanaadamu.

4.      Maisha ya mitume.

5.      Mafundisho ya mitume.

 

1.      Umbile la Mbingu na Ardhi na Vyote Vilivyomo.

Maumbile mbali mbali kama vile udongo, milima, mabonde, maji, mimea, wanyama, jua, mwezi, nyota, n.k ambavyo ni ishara kubwa inayoonyesha uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w). Ishara hizo ni hizi zifuatazo;

(a) Umbile la Mbingu na Ardhi;

Tukichunguza maumbile mbali mbali ya dunia na sayari zote jinsi yalivyoundwa na kupangika kwa namna iliyo maalum kama vile jua, mwezi, nyota, n.k ni ishara tosha kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w). Rejea Qur’an(41:9-12), (7:54), (32:4-5), (70:4), (21:30), (46:33) na (79:30).

 

                  (b) Jua, Mwezi na Nyota;

Kuwepo kwa mfumo wa ajabu uliopangika wa Jua, mwezi na Nyota na kila kimoja kina njia yake pasina kutokea mgongano au mvurugano wa aina yeyote kati yao ni ishara kubwa za kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w). Rejea Qur’an(6:96), (7:54), (2:29), (10:5), (14:33).

 

                   (c) Usiku, Mchana, Mwanga na Giza;

Kupatikana na kubadilishana kwa usiku na mchana, mwanga na giza ni ishara tosha za kuthibitisha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) kwa wenye akili. Rejea Qur’an(2:164), (3:190), (17:12) na (28:71-72).

 

(d) Bahari, Maziwa na Mito;

Wingi wa maji yasiyo na mfano, kutofautiana ladha yake, na kutengana kati ya maji matamu na chumvi bila ya kizuizi chochote na pia vyombo vizito na vikubwa kupita juu yake bila kuzama ni dalili nyingine ya kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w). Rejea Qur’an(25:53), (2:264), (10:22), (14:32), (16:14), (17:66), (22:65) na (53:12).

 

(e)  Milima na Mabonde;

Milima, majabali na mabonde ambavyo vinaifanya ardhi iwe madhubuti na isiyumbe  wakati wa mitetemeko na mzunguko kati ya jua, mwezi na nyota ni ishara kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).     Rejea Qur’an(21:31), (13:3), (15:9), (16:15), (27:61), (31:10), (50:7), (77:27), (35:27), (78:7) na (88:19).

 

(f)     Upepo, Mawingu, Mvua, Radi na Ngurumo;

Upepo, mawingu, radi, ngurumo na mvua ni vitu vinavyofanya kazi kwa ushirikiano wa ajabu unaopelekea mvua kunyesha sehemu inayohitajika. Vyote hivi ni dalili tosha juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).  Rejea Qur’an(10:22), (13:17), (2:19-20), (2:164) na (25:48).

 

(g)    Matunda, Mimea na Vyakula (Riziki);

Mimea na matunda mbali mbali hustawi katika aina tofauti za udongo na kutoa mazao ambayo ni riziki (chakula) kwa viumbe hai na kila kimoja kinategemea kingine katika kustawi kwake. Hii ni ishara kwa wenye akili.  Rejea Qur’an(67:21), (11:6), (29:60), (6:95,99) na (13:4).

 

(h)   Wanyama, Ndege na Wadudu;

Viumbe vyote hivi kutokana na kutembea, kuruka kwao na kupata kwao riziki bila ya wao kujipikia na kumiliki rasilimali yeyote, bado wanaishi bila shida yeyote. Hii ni kuonyesha kuwa ni Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye pekee anayewaruzuku.   Rejea Qur’an(16:5-7), (16:79) na (3:190-191).

 

2.      Nafsi (Dhati) ya Mwanaadamu.

Kutokana na nafsi ya mwanaadamu mwenyewe tukichunguza na kutafakari kwa makini kuna ishara nyingi zinazoonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) kama ifuatavyo;

 

(a)  Asili, Chanzo na mwisho wa uhai wa mwanaadamu;

Uhai, hatua alizopitia na mfumo wa maisha ya mwanaadamu, vipi na lini alianza atamaliza kuishi, nini sababu ya kifo chake na kitatokea wapi na nani anayedhibiti maisha yake yote ya kila siku, tunadhibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w).   Rejea Qur’an(2:28), (30:20-21), (22:5), (75:36-40), (23:14) na (56:81-87).

 

                  (b)  Mwanaadamu kutofautiana na Wanyama;

Wanaadamu kutofautiana na wanyama kimaumbile na kimalengo, ambapo lengo la mwanaadamu ni kuwa Khalifah, na wanyama ni kumtumikia mwanaadamu. Mwanaadamu amepewa akili, uhuru, vipawa na utambuzi kinyume na wanyama.  Rejea Qur’an(2:29-30), (15:28-29), (95:4) na (16:78).

 

(c)  Kuumbwa wanaume na wanawake na kuwa na mapenzi baina yao;

Asili ya wanaadamu wote ni moja, lakini wanatofautiana kimaumbile, kihisia na kisaikolojia. Hii ni kwa ajili ya kutegemeana, kuhurumiana na kuvumiliana kimahitaji kati yao kimwili na kisaikolojia. Zote hizi ni ishara tosha za kuwepo Allah (s.w).

 

(d)  Mwanaadamu kutofautiana lugha, rangi, kabila na taifa;

Pamoja na wanaadamu kufanana katika viungo mbali mbali vya miili yao kama ulimi, mdomo, koromeo, n.k lakini wanazungumza lugha tofauti bila ya kufunzwa na mtu yeyote. Hii ni kuwa utofauti wao ni kwa ajili ya kujuana tu, na hii ni dalili tosha.Rejea Qur’an(30:22) na(49:13).

 

(e)  Kutofautiana vipaji na riziki na mgawanyo wake miongoni mwa wanaadamu; 

Vipaji vya wanadamu vimetofautiana mmoja na mwingine kama vile udaktari, uhandisi, ualimu, n.k. pia upatikanaji wa riziki miongoni mwao ambao hautegemei ujanja, fani au ujuzi wa mtu bali mgao maalum ili waweze kutegemeana.   Rejea Qur’an(80:24-32).

 

(f)  Ufanyaji kazi wa viungo vya mwili wa mwanaadamu;

Myeyusho wa chakula, mfumo wa damu na ufanyaji kazi wa figo, mapafu, n.k ni mashine za ajabu zisizohitaji utengenezaji na usimamizi wowote wa kibinaadamu. Hii ni ishara kubwa juu ya uwepo Mtengenezaji Mjuzi na Mwenye Hekima.  Rejea Qur’an(30:30).

 

                 (g)  Usingizi, Umbo, sura na vazi la mwanaadamu;

Umbo au sura aliyonayo mwanadamu hana uwezo wa kuibadilisha na anaridhika nayo. Tofauti na wanyama wanaadamu wana mavazi ya kujisitiri uchi na kujikinga na baridi na pia kupata usingizi pasina yeye kutaka au kujua chanzo na mwisho wake.  Rejea Qur’an(7:26), (82:6-8), (95:4) na (45:4).

 

      (h)  Mwanaadamu kumkumbuka Mwenyezi Mungu (s.w) wakati wa matatizo;

Wakati wa matatizo mwanaadamu ni mwepesi sana kurejea na kumkumbuka Mwenyezi Mungu (s.w) na kuhitajia msaada wake, hata wale wanaokana kuwepo kwake wanakiri uwepo wake bila ujanja. Hizi zote ni ishara za kuwepo kwake.  Rejea Qur’an(6:63) na (10:90).

 

3.      Historia ya Maisha ya Mwanaadamu.

Mchakato wa maisha na historia ya mwanaadamu tangu zama za kale hadi zama hizi umeambatana na matukio makubwa yaliyovunja na kusambaratisha falme na dola mbali mbali zilizotikisha dunia vita na majeshi. Yafuatayo ni baadhi tu ya matukio hayo;

 

(a)  Kuangamizwa watu wa (kaumu ya) Lut, Thamud, Ad na Firauni;

Pamoja na nguvu kubwa za kijeshi na ulinzi imara waliokuwa nao watu hawa, haikuwa chochote ilipofika muda wa kuangamizwa kwao. Mwenyezi Mungu mwenye nguvu zisizokifani aliwafutilia mbali kwa kutumia majeshi yake ya upepo, maji, n.k.  Rejea Qur’an(89:6-13), (30:9), (20:128) na (22:45-46).

 

    (b)  Kuangamizwa kwa  jeshi la Abraha, Gavana wa Yemen;

Abraha aliandaa jeshi kubwa la askari na tembo waliofunzwa barabara kwa ajili ya kwenda kuibomoa Al-Ka’abah (Nyumba Tukufu ya Makka), lakini alisambaratishwa na jeshi dogo na dhaifu kabisa la ndege, na hatimaye ikawa ndio mwisho wao.  Rejea Qur’an(105:1-5).

 

(c)  Kufutika na kutoweka Viongozi na Wafalme maarufu Duniani;

Viongozi na wafalme wengi waliowahi kuitawala na kuitikisa dunia na kusababisa uharibifu, mauaji, kutokana nguvu kubwa ya kijeshi waliokuwa nayo na hata wengine kufanywa miungu. Mfano akina Hitler, Mussolini na wengineo ambao mwisho wao walifutika duniani na kushindwa kujinusuru pamoja na majeshi yao.Rejea Qur’an(56:81-87) na (67:20).

 

4.      Maisha ya Mitume;

Kwa kuzingatia maisha ya mitume hasa waliobainisha nadni ya Qur’an, jinsi walivyofikisha ujumbe kwa watu wao kinadharia na kimatendo ni ishara tosha juu ya uwepo wa Allah (s.w). Baadhi ya mambo hayo ni haya yafuatayo;

(a)   Kuwepo na kujieleza kwao kwa watu wao kuwa wao ni mitume wa Allah (s.w);

Mitume wote walithibitisha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w), na vile vile wote walitoa dai lilelile la kuwa wao ni mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w) ijapokuwa walikuja nyakati na sehemu tofauti.   Rejea Qur’an(7:59-61), (7:65-67), (16:36), (40:78) na (35:24).

 

      (b)  Mwenendo wao mwema kutoathiriwa na mazingira ya jamii;

Mitume wengi walizaliwa na kulelewa katika jamii za kijahili, kishirikina na kuabudu masanamu, lakini na walikuwa na mienendo na tabia nzuri isiyo kuwa na mfano katika jamii husika. Hii ni ishara kuwa yupo Mlezi na Mjuzi, naye ni Allah (s.w).  Rejea Qur’an(57:25).

 

(c)  Miujiza kuthibitisha utume wao;

Mitume walikuja na miujiza tofauti tofauti ya kuthibitisha utume wao kwa watu wao. Kila mtume alikuja na miujiza kutoka kwa Allah (s.w) kama ishara ya kufikisha ujumbe kwa watu wake iliyokuwa tofauti na uchawi, viini macho na mazingaumbwe.  Rejea Qur’an(57:25), (28:29-32), (5:110), (15:9) na (4:82).

 

(d)  Kuhimili na kujitoa kwao muhanga;

Mitume walikuwa wavumilivu na wenye subira dhidi ya mateso, kupigwa, kufungwa gerezani, kutiwa kizuizini au kuuawa na kupata madhila, lakini hawa kukata tama na kufikisha ujumbe wao. Hii ni yupo alikuwa anawaliwaza, naye ni Allah (s.w). Rejea Qur’an(3:21), (3:181), (4:157-158), (21:69) na (59:8).

 

                  (e)  Ujasiri wa mitume mbele ya viongozi na jamii za kishirikina;

Pamoja na vitisho na viburi vya wafalme na watawala wa kishirikina, mitume hawakumchelea mtu yeyote katika kumfikishia ujumbe wao. Hii ni ishara kuwa Mwenyezi Mungu ndiye waliokuwa wanamtegemea.   Rejea Qur’an(19:42-46) na (21:57-67).

 

     (f)  Ushindi wa mitume dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu (s.w);

Mitume na wafuasi wao walikuwa wachache, dhaifu na wanyonge mbele ya maadui wa Allah (s.w) waliokuwa wengi na wenye nguvu, lakini katika mapambano mitume na wafuasi wao ndio waliopata ushindi kwa msaada kutoka kwa Allah (s.w). Rejea Qur’an(71:25), (7:72), (26:60-68) na (8:9-10).

 

                 (g)  Mitume kutohitaji malipo kutoka kwa watu wao;

Mitume walifanya kazi ngumu na nzito bila ya kuhitajia malipo yeyote kutoka kwa watu wao kinyume na viongozi wengi ambao huhitajia malipo kwa jamii zao. Mitume walikuwa na uhakika wa kupata ujira tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) pekee.  Rejea Qur’an(26:127).

 

5.      Mafundisho ya Mitume.

Hili ni eneo jingine linaloonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) katika vipengele vifuatavyo;

(a)  Umoja wa ujumbe wa mitume;

Mitume walitumwa sehemu na nyakati tofauti lakini ujumbe wao ulifanana, kila mtume alifundisha Tawhiid, lengo la kuumbwa kwao, kuwahofisha na adhabu na kuwabashiria malipo mema pia. Hii ni kuwa ujumbe wao ulitoka kwa Allah (s.w).  Rejea Qur’an(7:59, 65, 73, 85, 158), (16:36) na (19:36).

 

      (b)  Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira;

Mitume karibu wote walitokea katika jamii za kishirikina na kijahili, lakini kamwe hawakuwahi kuchanganya mafundisho yao na utamaduni wa kijahili hata kama jamii nzima ilisimama dhidi yao.   Rejea Qur’an(109:1-6).

 

                  (c)  Upeo wa Elimu waliokuwa nayo Mitume;

Mitume walikuwa na upeo, fikra na hekima ya hali juu katika kutatua na kuendea mambo kuliko mtu yeyote katika jamii zao, japokuwa hawakupitia vyuo au taasisi zozote za elimu. Hii ni dalili kuwa ni Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye aliyewafunza.   Rejea Qur’an(34:10-12), (27:15-19), (43:2-3) na (25:53).

 

§  Athari za Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha ya kila siku.

Muumini wa kweli huishi katika kila kipengele cha maisha yake kwa mujibu wa taratibu na kanuni alizoweka Mwenyezi Mungu (s.w), na hii kama ifuatavyo;

 

(i)      Kupata ukombozi kutokana na utumwa wa aina zote;

Huu hupatikana baada ya mtu kuwa huru na kuishi kwa kufuata taratibu na kanuni alizoweka Mwenyezi Mungu (s.w) pekee.  Rejea Qur’an(12:39).

       (ii)  Mwanaadamu huwa mwadilifu katika utendaji wa maisha yake ya kila siku;

Muumini wa kweli hufanya mem[a na kuepuka maovu bila hata ya kusimamiwa au      kuonekana na watu, kwa kujua kuwa mjuzi pekee ni Mwenyezi Mungu (s.w).  Rejea Qur’an(50:16).

 

                 (iii)  Humfanya mwanaadamu kuwa mpole, mvumilivu na mwenye huruma;

Mwanaadamu huwa mpole hasa kwa wenye shida na matatizo na pia kuwa na subra anapofikwa na mitihani na kujiepusha na kibri, majivuno na kujiona.   Rejea Qur’an(6:165).

 

     (iv)  Humfanya mja kuwa jasiri katika kusimamia haki, uadilifu na usawa katika jamii;

Muumini wa kweli huwa shujaa katika kupambana na dhulma na ukandamizaji wa aina yeyote na kupigania haki bila kumchelea mtu yeyote.   Rejea Qur’an(4:74), (5:45) na (9:111).

                 (v)  Humfanya mja kuwa na mtazamo mpana na sahihi juu ya maisha;

Muumini wa kweli kamwe hawi na fikra na mtazamo finyu katika kuyaendea maisha yake ya kila siku kwa kujua lengo, thamani na nafasi yake juu ya maisha ya Akhera. Rejea Qur’an(15:9).

                 (vi) Humuwezesha mja kuwa mwenye kukinai na kutosheka;

Muumini wa kweli hutosheka na kuridhika na kile alichokadiriwa na Mwenyezi Mungu (s.w) iwe kwa kupungukiwa au kuzidishiwa, yote kwake anashukuru.

 

2.2.   Shirk.

·         Maana : Shirk ni kinyume cha Upweke au Umoja (Tawhiid)

 

·         Maana ya Kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w):

Ni kujaalia kinadharia au kiutendaji kuwa kuna miungu wengine wanaoshirikiana na Mwenyezi Mungu (s.w) katika kuongoza na kuendesha Ulimwengu.

 

§  Aina za Shirk.

Kuna aina kuu nne za shirk,

1.      Shirk katika Dhati ya Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy Dhaat).

2.      Shirk katika Sifa za Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy Sifaat).

3.      Shirk katika Mamlaka ya Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy Ikhtiyaar).

4.      Shirk katika Hukumu za Mwenyezi Mungu – (Shirk fiy Ah-kaam).

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                            

        1. Shirk katika Dhati ya Mwenyezi Mungu (s.w).

Ni kujaalia au kuvinasibisha viumbe na uungu kwa kuvipa majina rasmi kama washirika wa Mwenyezi Mungu (s.w) na kuviendea kwa unyenyekevu na ibada maalum kama, kuvisujudia, kuchinja na kuviomba msaada.    Rejea Qur’an(25:2-3), (22:73) na (29:41).

 

                 2.  Shirk katika Sifa za Mwenyezi Mungu (s.w).

Ni kuwasifu au kuwatukuza viumbe kiwango anachostahiki kusifiwa au kutukuzwa Allah (s.w) peke yake. Kama kuomba dua, baraka na msaada kupitia kwa Wacha-Mungu, mfano kwa baraka za Mtume, Abdul-Qadir, Sharifu au Sheikh fulani n.k.Rejea Qur’an(53:32), (10:62-64), (2:180), (17:110) na (40:60).

 

                  3.  Shirk katika Mamlaka ya Mwenyezi Mungu (s.w).

Ni kuwakabidhi viumbe mamlaka kamili ya Mwenyezi Mungu (s.w) na kuwatii kwayo kama vile kuongoza, kulisha, kulea, kulinda n.k katika maisha ya kila siku kinyume na nafasi au uwezo wao.   Rejea Qur’an(9:31) na (2:208).

 

                  4. Shirk katika Hukumu za Mwenyezi Mungu (s.w).

Ni kutunga sheria au hukumu kinyume na sheria au hukumu za Mwenyezi Mungu (s.w) alizoziainisha katika vitabu vyake vitukufu na kuzitumia kuhukumu kwazo katika uendeshaji wa maisha ya kila siku.    Rejea Qur’an(5:38), (24:2), (33:36), (5:44-45, 47) na (5:50).

 

§  Kina cha Uovu wa Shirk.

o   Ni dhulma kubwa kuliko zote na ndio chanzo cha matatizo yote ulimwenguni.

Rejea Qur’an(31:13) na (10:35-36).

o   Ni dhambi kubwa kuliko zote isiyosameheka ila apende Mwenyezi Mungu (s.w) na kutubia kikweli kweli kabla ya kufa.

o   Ni dhambi inayofuta mema yote ya mtu aliyoyafanya kabla ya kushirikisha.

Rejea Qur’an(4:48), (4:116) na (39:65).

§  Maana ya Kumuamini Mwenyezi Mungu(s.w) katika maisha ya kila siku.

Ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kufuata barabara mwongozo wake katika utendaji wa wetu wa kila kipengele cha maisha yetu ya kila siku kwa kufanya moja kati ya mambo yafuatayo;

o   Kusimamisha Tawhiid (Umoja na Upweke wa Mwenyezi Mungu) na

o   Kujiepusha na Shirk za aina zote.

 

§   Tawhiid.

o   Kimaana:  Ni Umoja au Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w).

o   Kimatumizi:   Ni fikra, mtazamo wa kimapinduzi katika kumkomboa

mwanaadamu na aina zote za utumwa wa kibinaadamu na kuwa   mtumishi huru wa Muumba wake. 

 

§  Aina za Tawhiid.

Kuna aina kuu tatu za Tawhiid kama zilivyoainishwa katika aya za Qur’an.

 

(i)  Tawhid Al-Uluuhiyyah – Upweke wa Allah (s.w) katika Uungu wake.

Nayo ni Kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) katika Uungu wake kwa kutokuwa na mungu mwingine yeyote wa kumuelekea kwa ibada au maombi isipokuwa yeye peke yake. Rejea Qur’an (2:163), (3:62) na (112:1-4).

 

   (ii)  Tawhiid Al-Asmaa Wassifaat – Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w) katika Majina  na Sifa.

Nayo ni kutomsifu Mwenyezi Mungu (s.w) kwa sifa za viumbe au majina ya viumbe na pia kutomsifu kiumbe yeyote kwa sifa za Mwenyezi Mungu (s.w).Rejea Qur’an(57:1-6) na (59:22-24).

 

 (iii) Tawhiid Rabbuubiyya, Upweke wa Mwenyezi Mungu (s.w) katika Ubwana,Utawala na Mamlaka Yake. 

Kumpwekesha Allah (s.w) katika Ubwana na Utawala wake ni kutofuata na sheria na taratibu za maisha kinyume na zile alizoziweka yeye kwa kumfanya ndiye Mlezi, Mlinzi, Mwendeshaji wa kila kitu.   Rejea Qur’an(4:59), (31:14-15), (25:52), (3:149), (3:100) na (5:57).

 

2.2.      Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu (s.w).

·         Maana: Malaika ni viumbe walioumbwa kutokana na nuru.

·      Sifa za Malaika:

- Ni viumbe wa kiroho wenye mabawa.

- Ni viumbe wasio na matashi ya kimwili (kula, kunywa, kulala, n.k.)

- Hawana hiari katika kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w).

- Ni vimbe wasio na jinsia.

- Ni viumbe walioumbwa kutokana na Nuru.

§  Kazi za Malaika.

                     Zifuatazo ni baadhi tu ya kazi za baadhi ya Malaika.

(a)    Kuleta Wahyi (ujumbe) kwa wanaadamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

Malaika Jibril ndiye mhusika mkuu wa kupeleka wahyi kwa mitume na manabii.

Rejea Qur’an(81:19-20), (16:2) na (11:69-73).

(b)    Kumchunga na Kumlinda kila mtu na kuandika amali zake nzuri na mbaya.

Kila mtu anakundi la malaika nyuma na mbele yake kumlinda na mambo yaliyo nje na uwezo wake. Pia kuna malaika wa kulia anayeandika mema na wa kushoto anayeandika maovu ya mtu.    Rejea Qur’an(82:1-12), (50:17-18) na (13:11).

(c)    Kuwaombea Waumini maghufira kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

Hawa ni malaika ambao huzunguka katika makundi ya waumini anapotajwa ndani yake Mwenyezi Mungu (s.w) au kusomwa Qur’anTukufu. Rejea Qur’an(40:7), (42:5) na (17:78).

(d)    Kuwasaidia waumini katika vita vya kupambana na maadui wa Allah (s.w).

Pindi waumini wanapopigana katika kusimamisha haki, Mwenyezi Mungu (s.w) huteremsha malaika kuwasaidia.  Rejea Qur’an(3:123-126) na (8:12).

(e)    Kuwaangamiza watu waovu waliopindukia mipaka.

Watu waovu waliopindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu (s.w) wakaonywa muda mrefu na wasionyeke huangamizwa na malaika maalum.  Rejea Qur’an(11:81-83).

(f)     Kutoa roho za viumbe.

Malakul-Maut ndiye mhusika mkuu na wengineo katika kutoa roho za viumbe. Rejea Qur’an(32:11).

(g)    Kuzihoji, kuzistarehesha au kuziadhibu roho za wafu kaburini.

Malaika wanaohusika na kazi hii ni Munkar na Nakir.

(h)   Kupuliza Parapanda siku ya Qiyama.

Mipulizo ya Parapanda katika kufisha na kufufua viumbe siku ya Qiyama itafanywa na malaika Israfil.  Rejea Qur’an(39:68).

(i)      Kuwaliwaza na kuwakaribisha watu wema peponi.

Hili kundi jingine la malaika watakaofanya kazi hiyo siku ya Qiyama. Rejea Qur’an(41:30-32) na (39:73).

(j)      Kuwasimanga na kuwaadhibu watu waovu motoni.

Kuna kundi la malaika watakaokuwa wanaadhibu watu waovu motoni. Mlinzi mkuu wa milango ya moto ni Malaika Maalik.   Rejea Qur’an(25:22), (74:26-30) na (43:77).

(k)    Kumtukuza na kumsifu Mwenyezi Mungu (s.w).

Kuna kundi la malaika maalum kwa kazi hii tu.  Rejea Qur’an(40:7).

 

§  Maana ya Kuamini Malaika katika maisha ya kila siku.

              Zifuatazo ni athari za muumini wa kweli juu ya imani ya malaika katika kila kipengele cha maisha ya kila siku;

Kwanza, imani ya kweli juu ya Malaika humuepusha na kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w) na viumbe wake hasa wale wasioonekana kama Malaika, majini, n.k.

Rejea Qur’an(37:149-154), (43:16-19) na (21:26-27).

Pili, imani juu ya malaika huchochea mja kufanya ibada kwa bidii na kujiepusha na maovu na machafu ili kupata cheo kama malaika au zaidi.

Tatu, imani juu ya malaika pia humfanya mtu kuepuka kufanya maovu popote alipo na muda wowote kwa kujua kuwa yupo pamoja na malaik?a.

Nne, Mja anapoamini kuwa malaika huandika na kuhudhurisha vitendo vyake kwa Mwenyezi Mungu (s.w), hufanya bidii katika kufanya mema zaidi na kuepuka maovu kadri ya uwezo wake.

Tano, Muumini anapoamini kuwa malaika humuombea maghufira kwa Mwenyezi Mungu (s.w), hufanya bidii katika kuzidisha mema na kuepuka maovu kadri awezavyo ili kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu (s.w) zaidi.  Rejea Qur’an(17:13-14) na (18:49).

 

2.3.      Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w)

§  Vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyotajwa ndani ya Qur’anni;

1.      Suhufi – aliteremshiwa Nabii Ibrahim (a.s) na Nabii Musa (a.s).

2.      Taurat – aliyoteremshiwa Nabii Musa (a.s)

3.      Zaburi – aliyoteremshiwa Nabii Daud (a.s)

4.      Injili – aliyoteremshiwa Nabii Isa (a.s) na

5.      Qur’an– aliyoteremshiwa Nabii au Mtume Muhammad (s.a.w).

6.       

§  Tofauti kati ya Qur’anna Vitabu vingine vya Mwenyezi Mungu (s.w).

Kitabu cha Qur’an

Vitabu Vingine vya Mwenyezi Mungu

1. Neno la Asili.

Qur’animebakia katika lugha yake                    ya asili ya kiarabu fasaha pamoja nakutafsiriwa katika lugha tofauti.

 

Vitabu vingine lugha zao za asili                                                       zilizoshushiwa zimepotea na kutojulikana.

2. Lugha zilizoshushiwa Vitabu.

Lugha ya Qur’anni hai kwani mpaka leo inatumika na kufahamika na walimwengu wengi.

Lugha za vitabu vilivyotangulia ni mfu, zimefutika zamani na hazijulikani na watu.

Rejea Qur’an(14:4).

3. Kuhifadhiwa na Kulindwa Vitabu.

Qur’animebaki katika asili yake kama ilivyoteremsha bila kubadilishwa chochote na wanaadamu ndani yake.

Rejea Qur’an(15:9) na (41:42)

 

Vitabu vingine vimepotea katika asili yake kwa kupunguzwa, kuongezwa na kupotoshwa asili ya ujumbe wake na mikono ya wanaadamu..

4. Hitoria ya Kushushwa Vitabu.

Historia ya kushushwa Qur’aninajulikana vyema mfano; namna, sehemu, muda/kipindi na sababu ya kuteremshwa kila aya.

 

Vitabu vingine historia ya kushushwa kwao haijulikani, mfano; muda, nama, sababu au sehemu.

 

§  Lengo la kushushwa Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w).

Ni kuwa mwongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu katika kufuata maamrisho na kuacha makatazo yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) hapa ulimwenguni.  Rejea Qur’an(2:38-39), (2:185) na (5:44).

 

§  Maana ya Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha ya kila siku.

Waumini wa kweli wa vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w) ni wale wanaoendesha kila kipengele cha maisha yao ya kila siku kwa mujibu wa mwongozo uliopo katika vitabu hivyo.

 

§  Sababu za kutokubalika Vitabu vilivyotangulia kuwa Mwongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu zama hizi.

1.      Vitabu vilivyotangulia vimeingiliwa na mikono na matashi ya wanaadamu kiasi cha kupoteza au kupotoshwa ujumbe wake wa asili.

 

2.      Lugha ya vitabu vilivyotangulia imetoweka na kusahaulika duniani kiasi kwamba hata kingelikuwapo kimojawapo katika lugha yake asili, ujumbe wake usingelifahamika kwa watu.

 

3.      Vitabu vilivyotangulia vilikuwa ni mwongozo kwa watu maalum na kwa wakati maalum tu, havikuwa mwongozo kwa walimwengu wote na nyakati zote.

 

§  Sababu za Qur’ankuwa mwongozo sahihi pekee wa maisha ya mwanaadamu.

§  Qur’anyote ni maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake, hivyo ni mwongozo wa uhakika.

§  Ujumbe wa Qur’anumeelekezwa kwa walimwengu wote na zama zote zilizobakia hadi siku ya Qiyama.

 

§  Maana ya Kuiamini Qur’ankatika maisha ya kila siku.

Maana halisi ya kuiamini Qur’ankama Kitabu pekee cha mwongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu (muumini) ni kufanya yafuatayo;

                                            i.            Kuwa na yakini pasina shaka yeyote kuwa Qur’anyote ni maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake.    Rejea Qur’an(2:2).

 

                                          ii.            Kuufahamu vyema ujumbe wa Qur’anna kuuheshimu inavyostahiki kwa kujizatiti katika kujifunza kuisoma na kuijua ipasavyo.   Rejea Qur’an(73:4) na (7:204-205).

 

                                        iii.            Kulifahamu vyema lengo la Qur’anna kuiendea kwa lengo lake tu.Rejea Qur’an(14:1), (2:185) na (16:64).

 

                                        iv.            Kuitekeleza Qur’ankatika kukiendea kila kipengele cha maisha yetu ya kila siku kwa mujibu wa lengo lake tu.     Rejea Qur’an(5:44, 46-47).

                                               

3. MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA IBADA

            3.1 Dhana ya Ibada kwa Mtazamo wa Uislamu.

                  -    Ibada – Ni neno la Kiarabu linalotokana na neno ‘Abd’ lenye maana ya mtumwa au

                                     Mtumishi.

-          Kumtimikia Allah (s.w) kikweli kweli ni kufanya kila analoliridhia Allah (s.w).

-          Kuzingatia na kufuata amri zake zote kwa kuchunga mipaka yake katika maisha ya kila siku.

                           

            3.2 Lengo la Ibada Maalum.

                  - Ibada maalumu kama vile; swala, funga, zaka, hija, na sunnah zake ni kumuandaa mja

                     kuweza kumuabudu na kumtumikia Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo kwa kila

         kipengele cha maisha ya kila siku kibinafsi na kijamii. 

                 -  Ibada maalumu zimekusudiwa kumuandaa mja kufikia lengo la kuumbwa kwake. Rejea Qur’an                               

                    (51:56), (2:30).

 

     4.  NGUZO ZA UISLAMU.

4.1. Maana ya Shahada.

Shahada mbili ndio nguzo ya kwanza ya Uislamu na ndio kiingilio cha mtu katika Uislamu kwa kuyakinishwa moyoni, kutamkwa kinywani na kuthibitishwa kwa vitendo.Rejea Qur’an(41:30-31), (2:8) na (33:40).

 

            4.2. Maana ya Kusimamisha Swala.

Ni kuswali kwa kutekeleza kikamilifu nguzo, sharti zote za swala na kuwa na unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.

 

§  Nafasi na Umuhimu wa Kusimamisha Swala katika Uislamu.

Swala imesisitizwa na ina umuhimu katika Uislamu kwa sababu zifuatazo;

 

                                            i.            Kusimamisha Swala ni Amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).

Mwenyezi Mungu (s.w) ameamrisha waumini (waislamu) wote wasimamishe swala zote za faradh na sunnah ipasavyo.Rejea Qur’an(29:45),(4:103) na (14:31).

 

                                          ii.            Kusimamisha swala ni nguzo ya Pili ya Uislamu.

Baada ya shahada mbili, nguzo ya pili na ya msingi mno katika Uislamu ni kusimamisha swala.

 

                                        iii.            Swala humtakasa muislamu na mambo machafu na maovu.

Bila shaka swala ikiswaliwa vilivyo humuepusha mja na mambo machafu na maovu.

Rejea Qur’an(29:45).

 

                                        iv.            Swala ni amali ya mwanzo kabisa kuhesabiwa siku ya Qiyama.

Swala ya muumini ikitengemaa vizuri ndio sababu ya kufaulu kwake Duniani na Akhera pia.   Rejea Qur’an(23:1-2,9), (87:14-15) na (22:34-35).

 

                                           v.            Kutosimamisha swala ni sababu ya mtu kuingizwa motoni.

Hii ni baada ya muislamu Kupuuza swala kwa kutozingatia sharti na nguzo zake kikamilifu na kukosa unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.Rejea Qur’an(74:42-47), (68:42-43) na (107:4-5).

 

§  Lengo la Kusimamisha Swala.

Lengo kuu la kusimamisha swala ni kumkinga mja na mambo machafu na maovu kwa kutekeleza kikamilifu sharti, nguzo na sunnah za swala pamoja na kuwa na khushui ndani ya swala kama ifuatavyo;

                                               i.            Swala inamtakasa mja kwa kuzingatia na kutekeleza sharti zake zote kikamilifu ambazo ni kuwa twahara, sitara (kujisitiri), kuchunga wakati wa swala na kuelekea Qibla.

                                             ii.             Swala inamtakasa mja kwa kutekeleza kikamilifu nguzo na sunnah za swala kama kumsifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu (s.w), kusoma Qur’an, kutoa ahadi ya kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (s.w), kuomba dua na kutekeleza vitendo vyote vya swala.

 

§  Faida (matunda) ya kusimamisha swala katika jamii.

Swala za faradhi zikisimamishwa vilivyo faida zifuatazo hupatikana katika jamii;

 

                                               i.            Usafi na unadhifu wa mwili.

Kwani muislamu hawezi kuswali mpaka ahakikishe kuwa msafi (twahara) kikamilifu katika nguo na mwili pia na sehemu ya kuswalia.   Rejea Qur’an(7:31).

 

                                             ii.            Utakaso wa Nafsi.

Kwa kutekeleza sharti na nguzo za swala pamoja na mnyenyekevu katika swala, hupelekea mja kuwa mtiifu ipasavyo kwa Mola wake muda wote.

 

                                           iii.            Swala za jamaa huimarisha udugu, umoja na usawa.

Kuswali katika jamaa huleta udugu, umoja na usawa wa kweli na kuepusha mfarakano, chuki na ubaguzi miongoni mwa waislamu.    Rejea Qur’an(49:10,13).

 

                                           iv.            Swala za jamaa huwafunza waislamu uongozi bora.

Swala huongozwa na imamu (kiongozi) wa waumini husika anayetokana na wao kutokana na sifa maalumu za kuwa kiongozi.

 

§  Kwa nini Wengi wanaoswali hawafikii Lengo la Swala?

Miongoni mwa sababu ya wengi kutofikia malengo ya swala zao ingawa wanaziswali misikitini tena kwa jamaa ni;

 

1.      Hawajui lengo halisi la swala.

Waislamu wengi huswali kwa lengo la kufutiwa madhambi na kupata thawabu na sio kuepukana na machafu na maovu, ambalo ndio lengo kuu la swala. Kupata thawabu na kufutiwa madhambi ni matunda ya swala.   Rejea Qur’an(29:45) na (72:23).

 

2.      Waislamu wengi hawana ujuzi halisi juu ya swala.

Pamoja na waislamu wengi kutekeleza swala zao kwa jamaa lakini wengi wao hawajui kabisa miiko, sharti na nguzo za swala ila wanafuata mkumbo tu.Rejea Qur’an(7:205), (7:55) na (4:142).

3.      Waislamu wengi hawahifadhi swala zao.

Pamoja na kuswali kwao bado wengi hawazingatii na kutekeleza kikamilifu sharti na nguzo za swala zao inavyotakiwa.Rejea Qur’an(107:4-5) na (23:1,8).

 

4.      Wengi hawaswali kwa Unyenyekevu swala zao.

Kukosa unyenyekevu (utulivu wa mwili, fikra na uzingativu) hupelekea mwenye kuswali kutofikia lengo na matunda ya swala.RejeaQur’an(29:45),(23:1-2) na(23:10-11).

 

5.      Kutosimamisha Swala za jamaa ipasavyo.

Waislamu wengi hawaswali jamaa misikitini au hawazingatia sharti za swala ya jamaa kama kunyoosha safu ipasavyo, kugusanisha mabega, vidole, n.k.  Rejea Qur’an(23:1-2).

 

            4.3. Kutoa Zakat.

§  Umuhimu wa Zakat na Sadakat katika Uislamu.

                                   i.            Zakat ni nguzo ya tatu ya Uislamu.

Baada ya shahada mbili na kusimamisha swala nguzo muhimu sana katika uislamu ni kutoa zakat kama ilivyoainishwa katika hadithi.

                                                                                         

                                 ii.            Kutoa zakat na Sadaka ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).

Kutoa zaka na vile tulivyoruzukiwa katika mali na huduma au misaada mbali mbali ni wajibu kwa waislamu wanaovimudu.Rejea Qur’an(14:31) na (2:254).

 

                               iii.            Kutoa Zakat ndio kitambulisho cha Uislamu na Ucha-Mungu wa mtu.

Muislamu akiacha au kukataa kutoa zakat kwa makusudi ni ishara ya kuritadi na kutoka katika Uislamu.     Rejea Qur’an(9:11) na (2:2-3).

 

                               iv.            Kutoa Zakat na sadaka ni sababu ya mtu kufaulu Duniani na Akhera.

Miongoni mwa sifa za waumini na wacha-Mungu ni kutoa katika vile walivyoruzukiwa na muumba wao.Rejea Qur’an(2:2-3), (23:1-4), (22:34-45) na (2:262,274).

 

                                  v.            Kutotoa Zakat na Sadaka ni sababu ya kuangamia mtu Duniani na Akhera.

Kutotoa katika vile tulivyoruzukiwa hupelekea mtu kustahiki adhabu hapa Duniani na Akhera pia.    Rejea Qur’an(9:34-35), (92:8-10) na (3:180).

 

§  Namna lengo la zakat linavyofikiwa.

Zakat na sadaka zinalengo la kutakasa mali na nafsi ya mtoaji na mpokeaji kama ifuatavyo;

                                   i.            Zakat na sadaka inavyotakasa mali ya mtoaji.

Zakat hutolewa 2.5% ya mali na kuwapa wanaostahiki, hivyo kuitakasa mali ya mtoaji kutokana na chumo la haramu na haki za watu.

 

                                 ii.            Zakat na sadaka zinavyotakasa nafsi ya mtoaji.

Utoaji mali kwa wanaostahiki huitakasa nafsi ya mtoaji kutokana na ubakhili, kuabudu mali, kibri, n.k katika kumiliki mali na kuwa na upole, huruma, n.k.

Rejea Qur’an(61:10-12) na (9:102-103).

 

                               iii.            Zakat na sadaka inavyotakasa nafsi ya mpokeaji.

Utoaji wa zaka na sadaka kwa wanaostahiki huondoa chuki, husuda, uadui, unyonge kwa wasionacho na kuleta udugu, upendo, shukurani na ushirikiano.  Rejea Qur’an(9:60).

 

                               iv.            Zakat na sadakat huitakasa jamii ya waislamu.

Utoaji wa zakat na sadaka hujenga jamii yenye udugu wa kweli, kujenga uchumi wa halali na kuondoa chuki na uadui baina ya masikini na matajiri.   Rejea Qur’an(61:4).

 

§  Kwa nini lengo la Zakat na Sadaka halifikiwi katika jamii yetu?

Pamoja na zakat na sadaka kutolewa na baadhi ya waislamu lakini malengo yake hayafikiwi, zifuatazo ni baadhi ya sababu;

                                   i.            Wengi watoao zakat na sadakat hawajui lengo lake halisi.

Waislamu wengi wanatoa zaka na sadaka kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio utakaso.

 

                                 ii.            Waislamu wengi hawatoi zakat kabisa.

Waislamu wengi licha ya kuwa na mali na uwezo wa kutoa zakat na sadaka lakini hawatekelezi au kuhimiza wengine katika kutoa mali zao pia.  Rejea Qur’an(2:2-3).

                               iii.            Wengi watoao zakat na sadakat hawatekelezi masharti ya utoaji.

Pamoja na matajiri wachache kutoa zakat na sadaka, lakini bado hutoa kwa ria, masimbulizi,adha na kuleta uadui na fitna katika jamii.Rejea Qur’an(2:264).

 

                               iv.            Zakat na sadaka haikusanywi na kugawanywa kijamii.

Utoaji na ugawaji wa zakat na sadaka umekuwa unafanywa kila mtu kivyake, bila mpango maalumu wa kukusanya na kugawa kwa wanaostahiki.

 

                                  v.            Wengi watoao zakat na sadakat chumo lao ni la haramu.

Ingawa waislamu wengi hutoa zakat na sadaka, lakini lengo na matunda yake hayafikiwi kutokana na chumo lao kuwa haramu.

 

            4.4. Saumu (Funga).

§  Umuhimu wa swaumu (Funga) katika Uislamu.

 

                                      i.            Funga ya mwezi wa Ramadhani ni nguzo ya nne katika Uislamu.

Funga ya mwezi wa Ramadhani ni faradhi kwa waislamu wote na ni miongoni mwa nguzo za Uislamu baada ya shahada, swala na zakat.Rejea Qur’an(2:183).

 

                                    ii.            Kufunga mwezi wa Ramadhani ni utambulisho wa Uislamu wa mtu.

Mtu akiacha nguzo hii kwa makusudi ni sababu na ishara tosha ya kutoka katika Uislamu.

 

                                  iii.            Kufunga mwezi wa Ramadhani ni utambulisho wa Ucha-Mungu wa mtu.

Funga ya Ramadhani na sunnah zingine ni kielelezo cha Ucha-Mungu wa muislamu zikitekelezwa vilivyo.    Rejea Qur’an(2:183).

                                  iv.            Kutofunga mwezi wa Ramadhani makusudi hupelekea kukosa msamaha.

Muislamu asipofunga mwezi wa Ramadhani makusudi basi, hukosa msamaha, na rehma na hustahiki adhabu za Mwenyezi Mungu (s.w). 

                                     v.            Kufunga mwezi wa Ramadhani ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).

Kufunga mwezi wa Ramadhani ni faradhi (amri) kwa waislamu wote isipokuwa wenye udhuru.    Rejea Qur’an(2:183).

 

§  Lengo la Funga linavyofikiwa.

Lengo kuu la funga ni kumuandaa mja (muislamu) kuwa mcha-Mungu (2:183). Na lengo hili hufikiwa kama ifuatavyo;

                                            i.            Funga humzidishia mfungaji imani na uadilifu.

Kufunga ni ibada ya siri, anayejua ni mfungaji na Muumba wake tu, hivyo hufunga ili apate radhi na malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu peke yake.

                                          ii.            Funga humzidishia mja nidhamu na utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

Mja akiwa amefunga huwa mtiifu kwa kufuata amri na kuacha makatazo ya Mwenyezi Mungu na kuchunga vilivyo masharti na nguzo zote za funga.Rejea Qur’an(2:168) na (2:172).

                                        iii.            Funga humzoesha mja kudhibiti matashi ya nafsi na kimwili.

Funga humuepusha mja na tabia za kinyama kama kula, kunywa, kujamii bila sababu ya msingi, na kumjenga kiroho na kiutu ili kuwa na hadhi yake.Rejea Qur’an(25:43-44) na (2:30-31).

                                        iv.            Funga humuwezesha mja kuwahurumia wanaadamu wenzake.

Funga hujenga huruma na mapenzi kwa kule mfungaji kukaa na njaa na adha yake, hivyo hujifunza kuwahurumia wasiokuwa nacho na wenye matatizo. (34:12-13) na (49:13).

                                           v.            Funga humpatia mfungaji afya (siha).

Kwa mfungaji kukaa na njaa muda mrefu, huuwezesha mwili kupumzika na kuondoa malimbilkizo ya vyakula tumboni ambayo ni sumu kwake.

 

                                        vi.            Funga huwafanya Waislamu kuwa Ummah mmoja.

Hii ni kwa sababu funga imefaradhishwa kwa waislamu wa rika na jinsia zote, maskini na matajiri pia, wote hutekeleza amri hii bila ubaguzi wowote.   Rejea Qur’an(49:13).

 

§  Faida za Funga.

-           Huleta huruma, upendo na mapenzi baina ya wanajamii.

-           Huleta utii na nidhamu kwa mfungaji kwa Mola wake na wanaadamu pia.

-           Huimarisha afya ya mfungaji.

 

§  Kwa nini Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji wengi?

Pamoja na waislamu wengi kujizatiti katika kufunga mwezi wa Ramadhani na funga zingine za sunnah, lakini wengi wao hafikii lengo la funga kwa sababu zifuatazo;

                                                        i.            Wengi wafungao hawajui lengo la funga.

Wafungaji wengi hufunga kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio kuwa wacha-Mungu kama lilivyo lengo la funga.   Rejea Qur’an(2:183).

 

                                                      ii.            Wafungaji wengi chumo lao ni la haramu.

Waislamu wengi wafungao chakula chao, futari yao na daku zao zinatokana na chumo la haramu ambalo ni sababu ya kutopata matunda ya funga zao.

 

                                                    iii.            Kutofahamika lengo la maisha na uhusiano na lengo la funga.

Waislamu wengi hutekeleza ibada maalumu kama swala, funga, n.k na kuona kuwa ndio lengo kuu la maisha yao na kuacha nyanja zingine za maisha yao. Rejea Qur’an(51:56).

 

                                                    iv.            Wengi wafungao hawazingatii miiko na sharti za funga zao.

Waislamu wengi wafungao huishia kushinda njaa na kiu bila kupata faida ya funga zao kwa kutojizuilia na mambo maovu, machafu, laghawi, upuuzi, n.k.

 

                                                       v.            Wengi wafungao hawatekelezi nguzo na sunnah za funga ipasavyo.

Pamoja na waislamu wengi kufunga, lakini wengi wao hawaswali kabisa swala za faradh na sunnah na kubakia kufuata mkumbo kwa kushinda na njaa.

 

4.5. Hijjah.

§  Umuhimu na Nafasi ya Hijjah katika Uislamu.

                                            i.            Hijjah ni nguzo ya tano ya Uislamu.

Baada ya shahada, swala, zakat na funga, nguzo muhimu na ya mwisho ya Uislamu ni Hijjah.       Rejea Qur’an(3:97).

 

                                          ii.            Hijjah ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).

Kama ilivyofaradhi kwa nguzo zingine, Hijjah ni ibada ya lazima kwa waislamu wenye uwezo wa kimali na afya.     Rejea Qur’an(3:97).

 

                                        iii.            Kutoenda Hija makusudi ni kustahiki adhabu za Mwenyezi Mungu.

Kwa kila muislamu mwenye uwezo, akipuuza kutekeleza ibada ya Hijah basi anastahiki adhabu hapa duniani na Akhera pia.    Rejea Qur’an(3:97).

 

                                        iv.            Kutekeleza ibada ya Hija hupelekea kupata msamaha Duniani na Akhera.

Kwa kila mwenye kutekeleza ibada ya Hijjah ipasavyo, basi husamehewa madhambi yake yaliyotangulia.

 

§  Lengo la Hijjah.

Kuwa askari Mcha-Mungu aliyekuwa tayari kutumia mali na nafsi yake katika kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kutawala maisha ya jamii.   Rejea Qur’an(48:18) na (3:96-97).

 

§  Matendo ya ibada ya Hijjah na Mafunzo yatokanayo.

Kabla na wakati wa kutekeleza ibada ya Hijjah, kuna mafunzo na hatua za kuzingatia kama ifuatavyo;

 

                                            i.            Maandalizi na Safari ya Hijjah.

Ni lazima muislamu kabla ya kwenda Hijjah afanye maandalizi ikiwa ni pamoja na kuzidisha ucha-Mungu, kuandaa gharama, mahitaji, n.k.   Rejea Qur’an(2:197)

 

                                          ii.            Ihram.

Ni hali ya kuwa katika vazi rasmi na miiko kwa mwanaume mwenye Kuhiji au kufanya Umrah.

Funzo (49:13):

-  Vazi la Ihram linatufunza usawa baina ya wanaadamu wote.

 

                                        iii.            Talbiya.

Ni kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kusema yafuatayo, “Labbayka Allahumma Labbayka. Labbayka laashariika laka labbayka. Innal-hamda Wanni’imata laka wal-mulka, laashariika laka”

Mafunzo (22:27) na (48:18):

-          Talbiya inatufunza kumuitikia Mwenyezi Mungu (s.w) kufuata maamrisho na kuacha makatazo yake.

-     Talbiya inatufunza umoja na usawa baina ya waislamu wote.

 

                                        iv.            Tawaf.

Ni kitendo cha kuizunguka Ka’aba mara saba kuanzia jiwe jeusi kwa mwelekeo wa kinyume na saa kwa kulibusu au kuligusa au kuashiria.

Mafunzo:

-          Kuchukua ahadi ya utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

-          Kumtaja na kumtukuza Mwenyezi Mungu (s.w) kwa wingi.

-          Inatufunza umoja, udugu na usawa baina ya wanaadamu wote.

 

                                          v.            Sai.

Ni kitendo cha kutembea mara saba baina vilima viwili, Saffaa na Marwaa, kwa kuanzia Saffaa na kumalizia Marwaa.

Mafunzo:

-          Inatufunza utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

-          Inatufunza ushujaa na uhodari katika kupigania Uislamu.

-          Inatufunza kuwa tayari kuhangaika kwa ajili ya kupigania Uislam

 

                                        vi.            Kupiga Kambi Mina, Mwezi 8 Dhul-Hijah.

Ni kitongoji kilichopo baina ya Mji wa Makkah na bonde la Arafah. Mahujaji hulala hapo na kuondoka kesho yake kuelekea Arafa asubuhi.

Mafunzo:

-          Huwafunza mahujaji kuwa askari waliotayari kuacha kila chaokwa ajili ya kupigania Uislamu.

-          Huwafunza mahujaji kuwa askari wanatiifu kwa Muumba wao.

 

                                      vii.            Kusimama Arafah, Mwezi 9 Dhul-Hija.

Arafa ni bonde lililo baina ya vilima vitatu. Mahujaji husimama humo tangu Swala ya Adhuhuri hadi Magharibi na kuomba dua mbali mbali.

Mafunzo:

-          Huwakumbusha mahujaji mkutano mkuu wa siku ya Kiama.

-          Hutufunza kuwa hakuna aliyebora ila amchae Mungu zaidi.

-          Kisimamo cha Arafa kinatufunza usawa baina ya wanaadamu.

 

                                    viii.            Kupiga Kambi Mzidalfah.

Mzidalfa ni kitongoji kilicho baina ya Mina na Arafa. Mahujaji huswali Magharib na Isha hapo na kuelekea Mina mara tu baada ya swala Alfajir.

                                     Mafunzo:

-          Huwafunza mahujaj kuwa askari waliojiandaa kupambana na maadui wa Mwenyezi Mungu (s.w).

-          Kuomba dua hutufunza kuwa ushindi ni kwa nusura ya Mungu tu.

                                        ix.            Kutupa Mawe Mina katika Minara Mitatu, Mwezi 10, Dhul-Hija.

Ni kitendo kinachofanyika kuanzia Mwezi 10-13, Dhul-Hija kwa kutupa vijiwe saba kila Mnara.

Mafunzo:

-   Zoezi hili huwafunza mahujaj ujasiri wa kupambana na maadui zao.

-   Huwafunza mahujaj pia mbinu na silaha katika kupigana na maadui.

 

                                          x.            Kuchinja mnyama Mwezi 10, Dhul-Hija.

Katika siku hii Hajj atanyo nywele, kuchinja mnyama, kutupa mawe kwenye Minara mitatu na kutufu Tawaful-Ifaadha (tawafu ya nguzo).

Mafunzo:

-   Zoezi hili linawafunza mahujaj utiifu kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

-   Tunajifunza kuwa tayari kuua au kuuawa kwa ajili ya Mungu.

-   Inatufunza kuwa na subira na kujitoa muhanga katika kunusuru dini  Rejea Qur’an(22:37) na (37:111).

 

                                        xi.            Siku za Tashriiq Mwezi 11-13, Dhul-Hija.

Ni kilele cha ibada ya Hija, ambapo mahujaj hupumzika kambini na kutathmini vitendo vyote walivyovifanya.

Mafunzo:

-   Huwafunza mahujaj kumkumbuka Mungu baada ya kazi ngumu.

-   Huwafunza askari kuwa na mazingatio na yale waliojifunza kwayo.

 

                                      xii.            Tawaf ya Kuaga (Tawaful-Widaa).

Ni Tawafu ya kuaga baada ya ibada ya Hija kukamilika na kujiandaa kurejea nyumbani kwa mahujaji.

Mafunzo:

-          Huwafunza mahujaj kuwa viongozi (makhalifa) katika ardhi.

-          Kuwa askari waliochukua mafunzo tayari kwa kuyatekeleza.

-          Kuchukua ahadi ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

 

§  Kwa nini wengi wanaohiji hawafikii lengo la Hijah zao?

Pamoja na mkusanyiko wa mamilioni wa mahujaj katika Mji wa Makka kila mwaka lakini matunda ya Hija hayafikiwi. Zifuatazo ni baadhi ya sababu;

                                                  i.      Kuhiji kwa chumo la haramu.

Waislamu wengu hufunga safari ya kwenda hija kwa fedha za pato la haramu ambazo ni kikwazo cha kupata matunda ya hija zao.

                                                ii.      Kutochunga miiko, nguzo na sharti za Hijah.

Pamoja na kufunga safari ya Hijah au Umrah, mahujaj wengi hawachungi miiko, nguzo na masharti ya Hijah au Umrah ipasavyo.  Rejea Qur’an(2:197).

                                              iii.      Kutokuwa na elimu na ujuzi sahihi juu ya ibada ya Hijah.

Mahujaji wengi hufunga safari ya kwenda Hija au Umrah ili hali hawana ujuzi wowote wa ibada watakazozitekeleza ila kufuata mkumbo tu.

                                              iv.      Kutojulikana kwa lengo halisi la Hijah au Umrah.

Waislamu wengi hufunga safari ya Hijah au Umrah kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio kuwa askari wa kupigania dini.  Rejea Qur’an(51:56).

                                                 v.      Kufunga safari ya Hijah kwa Malengo mengine.

Waislamu wengi hufunga safari kwa ajili ya biashara, utalii au kutafuta umaarufu wa kujiita majina ya Al-Hajj ambayo ni nje na lengo la Hijah.

5.0. HAKI NA UADILIFU KATIKA UISLAMU.

     5.1. Dhana ya Haki na Uadilifu katika Uislamu.

§  Maana ya Haki kwa Mtazamo wa Uislamu.

Ni muunganiko wa sheria na maadili kwa lengo na madhumuni ya kuilea jamii katika amani, furaha, udugu wa kweli na mahusiano mema kati ya wanaadamu.

§  Misingi ya Haki na Uadilifu katika Uislamu.

Maisha ya furaha na amani ya kweli hupatikana kwa kusimama misingi ya haki na Uadilifu katika jamii kama ifuatavyo;

                                            i.            Tawhiid.

Haki na Uadilifu wa kweli hupatikana kwa kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo katika maamrisho na makatazo yake.

 

                                          ii.            Utume.

Katika kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) ni kufuata misingi ya miongozo ya mitume wake wote kupitia vitabu vyao.

                                        iii.            Siku ya Mwisho.

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha yetu ni kuzingatia kuwa kila kitendo kitahukumiwa na kulipwa kwa haki siku ya Kiyama.

 

§  Aina au migawanyo mbali mbali ya Haki katika Uislamu.

1.      Haki za Allah.

2.      Haki za Nafsi.

3.      Haki za Viumbe na Mazingira.

4.      Haki za Binadamu kwa ujumla.

5.      Haki za Raia katika Dola ya Kiislamu.

6.      Haki za Maadui katika Vita (mateka).

 

1.      Haki za Mwenyezi Mungu (s.w).

Katika Uislamu haki za Mwenyezi Mungu ziko makundi mawili;

                                            i.            Haki ya Uungu.

Ni kumsifu na kumtii kwa sifa zake kama za uumbaji, umilikaji na ulezi wa viumbe vyote na ukamilifu wake tofauti na viumbe alivyoviumba.Rejea Qur’an(45:23), (25:68), (9:31) na (31:13).

                                          ii.            Haki ya Kuabudiwa.

Ni Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa na viumbe vyake muda wote, na ndio lengo kuu la kuumbwa mwanaadamu.Rejea Qur’an(51:56), (5:44), (11:25-26) na (29:16-17).

2.      Haki za Nafsi.

Haki za nafsi imekokotezwa kuanzia binafsi, familia, wazazi, n.k kama ifuatavyo;

(a)   Mtu Binafsi.

Haki za msingi ni chakula, makazi, malezi, elimu, mavazi, matibabu na kufanyia kazi vipaji na neema alizonazo inavyostahiki ikiwemo;

·         Haki ya Macho.

Ni kutazama yaliyoamrishwa na kuyaepusha na yaliyoharamishwa.

 Rejea Qur’an(17:36), (41:20), (24:30-31) na (20:131).

·         Haki ya Masikio.

Ni kusikiliza yaliyoamrishwa na kutosikiliza yaliyoharamishwa pia. Rejea Qur’an(8:22) na (6:25).

·         Haki ya Midomo na Ulimi.

Ni kula, kunywa na kuzungumza yaliyohalalishwa na sio yaliyoharamu.

Rejea Qur’an(16:114), (17:26-29), (17:53), (41:33) na (31:6).

·         Haki ya Mikono na Miguu.

Ni kushika na kuendea vyote vilivyoamrishwa na kuacha vilivyokatazwa.Rejea Qur’an(25:72) na (31:18).

                     (b)  Haki za Familia.

Ni kusimamia malezi, elimu, uadilifu na wajibu wa kila mmoja katika familia    kwa muongozo wa Qur’anna Sunnah ili kuleta kufikia lengo la kuumbwa. Rejea Qur’an(52:21).

                    (c)  Haki za Watoto.

Watoto wana haki ya kupata malezi na makuzi bora kulingana na mahitaji yao kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’anna Sunnah katika sehemu zifuatazo;

·         Haki ya Uhai.

Uhai wa mtoto ni haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kupitia malezi na makuzi ya wazazi.

·         Haki ya Nasaba.

                              Mtoto kupata nasaba ni haki kisheria ili kuwa mwanafamilia halali.  Rejea Qur’an(33:4).

·         Haki ya Makuzi na Malezi bora.

Makuzi na malezi bora ya mtoto ni kupata haki zake za msingi na elimu inayomuwezesha kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo.  Rejea Qur’an(66:6).

                    (d)  Haki za Wazazi.

Ni kuwahurumia, kuwaheshimu, kuwafanyia wema, kuwahudumia na      kuwalea ipasavyo.  Rejea Qur’an(31:14), (17:23-24), (4:36), (6:151), (19:14) na (19:32).

                    (e)  Haki za Jamaa na Majirani.

                              Ni kutunza uhusiano na kusaidiana pale inapohitajika kwa kuzingatia mipaka.  Rejea Qur’an         

                             (2:215).

                     (f)  Haki za Mayatima, Wajane na Masikini.

                              Ni kuwahifadhi na kuwasaidia wanapokuwa na shida na mahitaji ya kimaisha.

                              Rejea Qur’an(2:220), (4:2), (4:10), (2:262) na (2:267).

                    (g)  Haki za Udugu wa Kiimani na za Watu wengine.

                              Udugu wa kiimani ni haki na bora zaidi kuliko udugu wa damu au nasaba.

                              Rejea Qur’an(49:10), (49:13), (7:172-173), (4:7) na (5:8).

3.      Haki za Viumbe na Mazingira.

Uislamu umeweka kipaumbele katika kuhifadhi mazingira na kutunza viumbe hai na visivyo hai kupitia sera mbali mbali zikiwemo;

·         Haki ya Hifadhi ya Mazingira na misitu.

                              Rejea Qur’an(6:38), (27:60), (16:10-13), (50:7-9), (56:63-64) na (39:62).

·         Mazingira ni amana katika kulinda uhai wetu na wa viumbe wengine.

                              Rejea Qur’an(7:10) na (16:112).

·         Sera na Mafundisho ya Mtume (s.a.w) juu ya hifadhi ya mazingira katika kuleta ustawi wa jamii.

·         Sera ya mapinduzi ya kitabia katika kutunza na kuhifadhi mazingira yote yanayotuzunguka.

·         Sera ya usafi na uhifadhi wa mazingira ili kuleta ustawi wa viumbe hai.Reje Qur’an(6:141) na (25:2).

 

4.      Haki za Binaadamu kwa Ujumla (Basic Human Rights).

Uislamu umezingatia, kulinda na kusimamia haki za msingi za kibinaadamu bila kujali tofauti zao. Haki hizo ni pamoja na;

·         Haki za kuishi (maisha).   Rejea Qur’an(5:32), (6:151) na (17:33).

·         Haki ya Usalama wa Maisha        Rejea Qur’an(5:32).

·         Haki ya kulinda na kuheshimu hadhi na usafi wa mwanamke. Qur’an(17:32) na (24:2).

·         Haki ya kupata mahitaji ya lazima ya maisha.  Rejea Qur’an(70:24-25).

·         Haki ya Uadilifu na Usawa katika Hukumu (Righ to justice).Rejea Qur’an(5:8), (49:13) na (4:135).

·         Haki ya Uhuru (kila mtu kuwa huru).

Uislamu umezingatia kila mtu kuwa huru kifikra na kutomilikiwa kama bidhaa ya baishara.

 

5.      Haki za Raia katika Dola ya Kiislamu.

·         Haki za msingi za raia waislamu na wasiokuwa waislamu katika Dola ya Kiislamu ni pamoja na;

·         Haki ya kuendesha maisha binafsi bila kuingiliwa na mtu yeyote.

·         Haki na uhuru wa kutoa maoni na kuamrisha mema na kukataza mabaya.

                                    Rejea Qur’an(3:104), (9:71), (9:67).

·         Haki na Uhuru katika kufuata na kuabudu dini yeyote aipendayo mtu.

                              Rejea Qur’an(2:256), (6:108), (29:46) na (16:125).

·         Haki ya Kuwashtaki Viongozi wa juu wa Dola bila upendeleo na ubaguzi wowote.

·         Haki ya kumiliki mali au rasilimali zozote za halali na zisizoleta madhara kwa raia na Dola             

      kwa ujumla.   

·         Rejea Qur’an(2:262), (2:267) na (18:32-43).

6.      Haki za Maadui Katika Vita (mateka wa Kivita).

Uislamu unajali, kusimamia na kulinda haki ya kila mtu hata kwa maadui waliokamatwa katika vita (mateka) walifanyiwa haki na uadilifu kama ifuatavyo;  

·         Kuhurumiwa na kutofanyiwa ukatili wowote maadamu wamedhibitiwa.

·         Kuwapa mahitaji yao ya lazima ya kibinaadamu na kimaisha pia.

·         Kulinda uhai na usalama wa maisha yao mpaka mwisho wa uhasama.

·         Mateka wa kivita walikuwa na haki ya kujikomboa kwa njia zifuatazo;

o   Kulipa kiasi fulani cha pesa au mali yeyote inayokubalika.

o   Kubadilishana na mateka Waislamu waliokamatwa na maadui.

o   Kulipa fidia kwa kufanya jambo fulani lenye manufaa kwa jamii ya waislamu.    Rejea Qur’an(47:4).

·         Masuria na mateka wanawake walikuwa na haki ya kulindwa na kuhifadhiwa kwa kupewa

      wanaume waliokwenda vitani na kuishi nao katika maisha ya ndoa ili kupata mahitaji yao ya

      msingi.

·         Haki ya kumiliki mali au uchumi ulio wa halali na usio leta madhara yeyote katika Dola ya

      Kiislamu.

 

5.2. Msimamo wa Uislamu juu ya Utumwa.

  • Hali ya Utumwa kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w).

-    Biashara ya utumwa ilidumu na kuenea sana enzi za ujahili takribani nchi na

            mabara mbali mbali hasa nchi za Magharibi, Uarabuni, Bara la Asia na kwingineko Duniani.

     -  Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.

     -  Watumwa walimilikiwa kwa kuuzwa na kununuliwa kama bidhaa za biashara au kwa matumizi          

         mengineyo pia.

    -  Watumwa walikuwa wakitumika kama sehemu ya starehe na kiburudisho kwa wakubwa zao.

    -  Mateso, unyama na ukatili ilikuwa desturi ya kufanyiwa watumwa na mabwana zao katika kutimiza                 

       matashi yao.

    -  Watumwa walikuwa hawana uhuru wa kufanya na kufuata mila, desturi au dini waitakayo na waipendayo

        wao wenyewe bila ruhusa ya wakubwa wao.

   - Watumwa walikuwa wakitumikishwa kama wanyama au hata zaidi ya wanyama kwa kufanyishwa kazi          

     ngumu zilizozidi uwezo wao.

-  Kila jaribio la ubaya lilifanywa kupitia watumwa, mfano makali ya kisu, mkuki,

    mshale, n.k yalijaribiwa kwa watumwa.

-  Watumwa ndio ilikuwa nyenzo pekee ya kufanyia kazi, kubebea na kusafirishia

    mizigo mikubwa kwa masafa ya mbali.

-  Hadhi na nafasi kati ya mabwa na watumwa ilikuwa na utofauti mkubwa mno,

   kiasi kwamba bwana anaweza kumdhalilisha mtumwa kwa namna apendavyo.

-  Huduma na misaada ya kiutu kwa watumwa ilikuwa hafifu mno, kiasi kwamba

   mtumwa akiugua au kukosa uwezo wa kuzalisha mali alikuwa hana faida tena

   kwa bwana.

§  Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w).

Uislamu baada ya kuenea na kuongoza sehemu mbali mbali, ilikuwa ndio mwanzo wa kukomesha biashara ya utumwa na kumkomboa mwanaadamu kiutu, (kiroho), kifikra na kisaikolojia kupitia njia na sera mbali mbali kama ifuatayo:

-          Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.

-  Uislamu ulijenga uhusiano wa udugu na upendo baina ya watu bila kujali hadhi, nafasi, rangi,

taifa la mtu.

- Uislamu ulisisitiza kuwa ubora wa mtu unatokana na ucha-Mungu wake na pia mtumwa au mtu

huru anastahiki kuwa kiongozi na kutiiwa ipasavyo    Rejea Qur’an(49:13) na (4:25).

-  Utumwa katika Uislamu ulikuwa jambo la kupita na sio taasisi ya kudumu inayojenga matabaka ndani ya jamii.

-Uislamu uliweka mikakati ya kulinda haki, utu na hadhi ya watumwa kwa kuwafanyia wema na ihsani kama wanaadamu wengine.Rejea Qur’an(4:36) na (49:13).

-   Watumwa walikuwa na haki ya kuamini na kufuata mila au dini waipendayo bila kushurutishwa.    Rejea Qur’an(2:256).

-   Watumwa walikuwa wanapata huduma za kijamii kama mavazi na malazi sawa na mabwana au wanaadamu wengine.

-     Mtumwa alikuwa akikosea alisamehewa badala ya kuadhibiwa, Mtume (s.a.w) alisema mtumwa asamehewe hata mara sabini kwa siku.

-   Mtumwa alistahiki kuwa kiongozi na kutiiwa ipasavyo maadamu ni muislamu na Mcha-Mungu. Mtume (s.a.w) amesema “msikilizeni na mtiini kiongozi hata akiwa ni mtumwa wa kutoka uhabeshi, maadam anafuata njia ya haki

-     Uislamu unalinda hadhi ya mtumwa kwa kutomuita “Ewe mtumwa wangu” badala yake anaitwa “Ewe kijana wangu”.

-     Watumwa walikuwa na haki ya kujikomboa na huru kwa njia mbali mbali zikiwemo:

o   Kulipa kiasi fulani cha pesa au mali yeyote inayokubalika.

o   Kubadilishana na mateka Waislamu waliokamatwa na maadui.

o   Kulipa fidia kwa kufanya jambo fulani lenye manufaa kwa jamii ya   waislamu.     Rejea Qur’an(47:4).

 

-  Mtume (s.a.w) na Maswahaba waliwaachia watumwa huru na kuwakomboa wengine kisha kuwaacha huru kama ifuatavyo:

o   Mtume (s.a.w) mwenyewe aliwaacha huru watumwa 63.

o   Bi Aisha (r.a) mkewe Mtume (s.a.w) aliwaacha huru watumwa 67.

o   Ibn Abbas aliwaachia huru watumwa 70.

o   Abdallah bin Umar aliwaacha huru watumwa 1,000.

o   Abdul-Rahman bin Auf alinunua watumwa 30,000 na kuwaacha huru.

Mpaka kufikia mwisho wa uongozi wa Makhalifah wa nne Waongofu, suala la Utumwa lilibakia kuwa historia katika ulimwengu wa Kiislamu.

6.0. QUR’AN

          6.1. Sura za Makkah na Madinah.

·         Mgawanyiko wa Qur’an.

-  Qur’anyote ina jumla ya sura 114 Sura zilizoshuka Makkah ni 86 zilizoshuka kwa miaka 13 cha Utume Na za Madinah ni 28 zilizoshuka kwa miaka 10.

 

§  Tofauti kati ya Sura za Makkah na Madinah

Sura za Makkah

Sura za Madinah

1. Walengwa.

Walengwa walikuwa waumini waliosimu mwanzo wa Utume.

Zililenga Maadui wa Dola ya Kiislamu Madinah wakiwemo; Wanafiq, Washirikina, Wayahudi na Wakristo.

2. Ujumbe.

Sehemu kubwa ya ujumbe ni kujenga imani juu ya Mwenyezi Mungu (s.w), Malaika, Vitabu, Mitume, Siku ya Mwisho na Qudra yake.

 

Ujumbe ulilenga ujenzi wa Dola na jamii ya Kiislamu Madinah kupitia sheria na hukumu mbali mbali.

3. Muundo wa sura.

Sura nyingi ni fupi na zina aya fupi fupi zenye lengo moja.

Sura nyingi ni ndefu na zina aya ndefu zenye ufafanuzi zenye lengo la utekelezaji wa sheria.

4. Mbinu

Zimetumia lugha fupi ya mchomo kwa walengwa kwa kutumia viapo, historia ya watu waliopita, kuwahofisha na kuwakatisha tamaa maadui wa Uislamu na kuwatia moyo na kuwaliwaza waumini katika kutekeleza ujumbe wa Qur’an.

Zimetumia lugha ya sheria na ufafanuzi katika ujenzi wa Dola ya Kiislamu Madinah, kwa kutumia historia ya Mitume ili kuwaliwaza waumini kupigania Dini na kuwakatisha tamaa maadui wao wakiwemo; makafiri, washirikina, wanafiq na Wakristo. 

 

    6.2. Tafsiri na Mafunzo ya Sura Zilizochaguliwa.

§  Suratul-Fiyl (105): Imeteremshwa Makkah, Ina Aya Tano.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

1.      Jee, huoni jinsi Mola wako alivyowafanya watu wa ndovu (tembo)?

2.      Jee, hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?

3.      Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi.

4.      Wakawapiga kwa vijiwe vya udongo wa motoni.

5.      Akawafanya kama majani yaliyoliwa (na kutemwa).

                  Mafunzo kwa Ufupi.

1.      Mwenyezi Mungu (s.w) ni Muweza wa kila kitu.

2.      Viumbe vyote viko katika Milki ya Mwenyezi Mungu (s.w) na ni Majeshi yake yaliyotayari kumtumikia ipasavyo.

3.      Nusura na Msaada wa Mwenyezi Mungu (s.w) hupatikana muda wowote watu watakapomuamini na kumtegemea ipasavyo.

4.      Kuangamizwa kwa Abraha na jeshi lake na Jeshi asilolijua wala kulitegemea ni dalili ya Kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).

§  Suratul-Humaza (104): Imeteremshwa Makkah, Ina Aya Tisa.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

1.      Adhabu kali itamthubutikia kila mwenye kuramba kisogo, asengenyaye, msengenyaji.

2.      Ambaye amekusanya mali na kuihesabu (tu bila ya kuitumia katika njia za kheri).

3.      Anadhania kuwa mali yake itambakisha milele.

4.      Hasha! Bila shaka atavurumishwa katika (moto unaoitwa) Huttama.

5.      Na ni jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni nini (huo moto unaoitwa) Huttama?

6.      (Huo ni) moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa (kwa ukali bara bara).

7.      Ambao unapanda (mpaka) nyoyoni.

8.      Hakika watafungiwa ndani ya moto huo.

9.      Kwa manguzo marefu (ili wasiweze kutoka).

 

Mafunzo kwa Ufupi ya suratul Humaza

1.      Kusengenya ni katika makosa makubwa kabisa.

2.      Ni makosa makubwa kukusanya mali bila kuitumia katika njia za kheri.

3.      Matumizi mabaya ya ulimi na neema zingine hupelekea kwenye maangamizi na adhabu.

4.       Matumizi mabaya ya ulimi kama fitna, uongo, usengenyi, n.k. huleta chuki, husda na mtafaruku katika jamii.

 

§  Suratul-A’sr (103): Imeteremshwa Makkah, Ina Aya Tatu.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

1.      Naapa kwa zama (zako Ewe Nabii Muhammad!).

2.      Kuwa wanaadamu yuko katika hasara.

3.      Isipokuwa wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri na wakausiana (kufuata) haki na wakausiana (kushikamana) na subira.

Mafunzo kwa Ufupi.

1.      Mwenyezi Mungu huapia kitu au kiumbe chochote kinachofahamika ili kutoa uthibitisho kwa kile anachoapia.

2.      Muumini haruhusiwi kuapa kwa kiumbe chochote isipokuwa kwa jina la Mwenyezi Mungu peke yake.

3.      Wakati (muda) ni rasilimali muhimu sana inayotakiwa kutumiwa kwa uangalifu mkubwa.

4.      Imani ya kweli huthibitishwa katika vitendo vizuri.

5.      Uislamu sio dini ya ubinafsi, hivyo ni lazima watu wausiane katika kufanya wema na kufuata haki.

6.      Subra ni nyenzo muhimu sana na ya pekee katika kuweza kuusimamisha Uislamu

§  Suratul- Takaathur (102): Imeteremshwa Makkah, Ina Aya Nane.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

1.      Kumekughafilisheni (katika) kutafuta wingi (wa mali na jaha na watoto na kujifakharisha kwayo).

2.      Hata mmeingia makaburini (mmekufa kabla ya kufanya kheri yeyote).

3.      Sivyo hivyo! Karibuni hivi mtajua (kuwa sivyo hivyo).

4.      Kisha (nasema) sivyo hivyo karibuni hivi mtajua (kuwa sivyo hivyo).

5.      Sivyo hivyo! Lau kama mnajua ujuzi wa yakini (kuwa sivyo hivyo msingefanya hivyo).

6.      Hakika mtauona moto wa Jahiym.

7.      Kisha (nasema) mtauona (moto) kwa yakini.

8.      Kisha kwa hakika mtaulizwa siku hiyo juu ya neema mlizopewa (mlizitumiaje).

 

                    Mafunzo kwa Ufupi.

1.      Pupa katika kutafuta anasa za dunia ndizo hupelekea mtu kumuasi Mwenyezi Mungu (s.w).

2.      Kuchuma mali na kuhangaikia watoto sio jambo baya, bali lisitusahaulishe katika kumtumikia Mwenyezi Mungu (s.w).

3.      Kuwepo siku ya mwisho ni jambo lisilo na shaka ili kila mtu akaulzwe juu ya jinsi alivyotumia neema alizopewa.

4.      Kutumia vibaya neema na vipawa tulivyonavyo hupelekea kumuasi Mola wake na hivyo kustahiki adhabu.

5.      Neema na vipawa tulivyonavyo ni dhamana kwetu na tutaulizwa siku ya Kiama.

 

 6.3. Kukusanywa na Kuhifadhiwa kwa Qur’an.

§  Qur’anina ahadi ya kuhifadhiwa na kulindwa na Mwenyezi Mungu (s.w) tofauti na vitabu vingine kama aya zifuatazo zinavyobainisha;

      “Hakika Sisi ndio tulioteremsha mawaidha haya (Qur’an) na hakika Sisi ndio tutakayoyalinda”  (15:9).

      “Hakitakifikia batili mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye Hikima ahimidiwaye” (41:42).

 

§  Njia na Hatua zilizotumika katika kuihifadhi na kuilinda Qur’an.

Mtume (s.a.w) mwenyewe aliweka misingi madhubuti ya kuihifadhi na kuhakikisha kuwa Qur’anhaipotei kupitia njia zifuatazo;

 

1.      Mtume (s.a.w) alihifadhishwa na kufanyishwa marejeo ya Qur’anyote na Malaika Jibril (a.s) mara kwa mara, hasa mwezi wa Ramadhani. Rejea Qur’an(73:1-4), (2:185).

2.      Mtume (s.a.w) aliahidiwa kuwa atasomeshwa Qur’anna Mwenyezi Mungu (s.w) na hata sahau kamwe.   Rejea Qur’an(75:16-19) na (87:6-7).

3.      Mtume (s.a.w) aliwahifadhisha Maswahaba na Waislamu Qur’anvifuani mwao wakati ilipokuwa inashuka.

Zaidi bin Thaabit amesema: “…..kila nilipomaliza kuandika (Wahayi), Mtume (s.a.w) aliniamuru nisome nilichoandika na nilikuwa ninamsomea. Kama  palikuwa na kosa alilisahihisha kisha aliwapa watu (kunakili na kuhifadhi vifuani mwao)”.

4.      Maswahaba waliihifadhi na kuisoma Qur’anmara kwa mara hasa katika ibada za swala na zinginezo.      Rejea Qur’an(73:1-5).

5.      Mtume (s.a.w) aliwasomea waandishi wa Qur’an(wapatao 42) na kuandika kama walivyosomewa na kisha Mtume (s.a.w) aliwataka wasome ili ahakiki walichoandika.

Uthman bin Affan (r.a) amesimulia: “Wakati wowote Mtume wa Allah (s.a.w) alipoteremshiwa wahyi humuita mmoja wa watu waliochaguliwa kuandika.” (Ameipokea Tirmidh)”.

 

6.      Mtume (s.a.w) aliwaagiza na kuwasimamia waandishi wa Qur’anwapangilie sura na aya kama zilivyo katika msahafu akiongozwa na Malaika Jibril (a.s).

Uthman bin Affan (r.a) ameeleza: “Ilikuwa kawaida ya Mtume wa Allah kila iliposhuka aya za sura mbali mbali (za Qur’an) au kila aya iliposhuka alimuita mmoja wapo wa waandishi wa Qur’anna kumwambia, “andika aya hizi katika sura kadhaa baada ya aya kadhaa.”

 

§  Umihimu wa kunakiliwa upya Qur’anwakati wa Uthman bin Affan (r.a).

Khalifa Uthman bin Affan (r.a) aliteuwa waandishi 4 kunakili misahafu 7 kutoka kwenye msahafu ulioandikwa wakati wa Mtume (s.a.w) kwa sababu zifuatazo;

 

-     Kutokana na kupanuka Dola ya Kiislamu na kusambaa maswahaba na walimu wa Qur’anmaeneo mbali mbali.

 

-     Kuwa na hitajio kubwa la kufundishwa ujumbe wa Qur’ansehemu mbali mbali hasa za ugenini.

 

-     Watu wengi waliingia katika Uislamu wakiwa wageni wa lugha ya Qur’an(Kiarabu) na kushindwa kuisoma na kupata ujumbe wa Qur’an.

 

-     Kuepusha kutofautiana kwa matamshi ya usomaji wa Qur’anya asili katika ufikishaji wa ujumbe wa Qur’an.

 

-     Kuepusha kupatikana mwanya wa maadui wa Uislamu katika upotoshaji na upoteaji wa ujumbe wa asili wa Qur’an.

 

             6.4. Madai na Hoja za Makafiri dhidi ya Qur’an.

                        Qur’anyenyewe inajieleza kuwa ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake,

                        “Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake” (2:2).               

 

Makafiri wa zamani na wa zama hizi wametilia shaka Qur’ankwa kutoa madai yafuatayo;

                                                        i.            Mayahudi wameikataa Qur’ankwa lengo la kuficha haki na batili (kuchanganya haki na batili). Qur’an(2:42), (40:74), (2:105) na (2:23).

                                                      ii.            Dai kuwa Qur’anni uzushi, uongo na visa vya watu wa kale. Qur’an(53:13), (65:15), (6:25), (38:7) na (8:31-32).

                                                    iii.            Dai kuwa Mtume ni mwendawazimu.  Qur’an(16:6), (13:47), (23:70), (68:5).

                                                    iv.            Dai kuwa Yuko anayemfundisha.   Qur’an(10:103), (44:14) na (25:2).

                                                      v.            Dai kuwa Qur’anni uchawi na maneno ya shetani.   Qur’an(34:43), (26:210).

                                                    vi.            Dai kuwa Mtume amerogwa.   Qur’an(17:43)

                                                  vii.            Dai kuwa Qur’anni mashairi ya Muhammad.   Qur’an(21:5), (52:33).

                                                viii.            Dai kwa nini hajapewa miujiza kama aliyopewa nabii Musa.   Qur’an(28:48)

                                                    ix.            Dai kwa nini Qur’anhaikuteremshwa yote kwa wakati mmoja.Qur’an(25:32).

                                                      x.            Kuifanyia Qur’anmzaha, chuki, kujivuna na kujiona.

Qur’an(41:52), (47:9), (86:13-14), (21:216-217), (45:9), (9:64).

                                                    xi.            Dai kuwa Muhammad si Mtume.   Qur’an(13:43).

                                                  xii.            Dai kwa nini Muhammad hakuteremshiwa Malaika.  Qur’an(17:95).

                                                xiii.            Dai kuwa mtume gani anayekula na kwenda sokoni.   Qur’an(55:7).

                                                xiv.            Dai kuwa kwa nini ametumwa binadamu.   Qur’an(34:43), (17:94).

                                                  xv.            Dai kuwa Mtume apande mbinguni na ateremke na Kitabu ili wakisome. Qur’an(17:93), (74:53).

 

7.0. SUNNAH NA HADITH.

     7.1. Hoja juu ya Kukubalika Hadith.

§  Hadith ni chanzo na chem chem ya pili kuwa muongozo wa maisha ya waumini baada ya Qur’an.

“Anachokupeni Mtume chukuweni na anachokukatazeni nacho kiacheni.”  (59:7).

“Anayemtii Mtume ameshamtii Mwenyezi Mungu.” (4:80)   Rejea pia Qur’an(52:3-4).

 

§   Zifuatazo ni baadhi ya hoja za wapinzani wa Hadith.

                                      i.      Hadith hazikufuata mpango kama ulivyo mpangilio wa Qur’anwakati wa kushuka, kupangwa, kuhifadhiwa na kuandikwa.

Udhaifu wa dai hili;

-  Kutoandikwa kwa Hadith kama ilivyoandikwa Qur’ansio hoja na sababu ya kutokubalika Hadith.

-  Mtume mwenyewe aliwakataza Maswahaba kuandika Hadith wakati wa uhai wake.

 

                                    ii.      Baada ya kufa Mtume (s.a.w), waislamu waligawanyika makundi tofauti yanayopingana, na hata kuweza kubuni maneno na kudai kuwa ni Hadith za Mtume (s.a.w). Je utajuaje Hadith zilizosahihi?

Udhaifu wa Hoja hii;

-  Kuna Wanachuoni wenye msimamo madhubuti waliobobea katika elimu ya Hadith na hawakujihusisha na migogoro yeyote iliyozuka

-  Vigezo vya kisayansi kama Isnad, Riwaya na Matin vilitumika katika kuchambua  usahihi na udhaifu wa Hadith.

 

                                  iii.      Hadith zilikusanywa na kuandikwa muda mrefu baada ya kufa Mtume (s.a.w) na Maswahaba. Je kuna ushahidi gani unaothibitisha kuwa maneno yaliyosemwa ni ya mtume (s.a.w)?

Udhaifu wa Hoja hii;

-  Sunnah ya Mtume (s.a.w) ni maelezo juu ya maisha yake ambayo maswahaba walirithishana baada ya kutawafu (kufa) Mtume.

-   Ukusanyaji na uandishi wa Hadith ulifanyika kwa utaalamu wa kisayansi katika kubaini ukweli wa Hadith.

 

       7.2. Mafunzo ya Hadith Zilizochaguliwa.

                                               

§  Hadith ya Kwanza; Kuamrisha mema na Kukataza Maovu.

 

Kutoka kwa Abi Saidil-Khudhur (r.a) amesema: Nimemsikia mjumbe wa Mwenyezi Mungu anasema;

“Mwenye kuuona uovu miongoni mwenu na auondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi (na aondoshe) kwa ulimi wake iwapo hawezi (na aondoshe) kwa moyo wake (achukie) na hiyo ndiyo imani dhaifu.”   (Ameipokea Muslim).

            Hatua za kuondosha uovu:

-          Hatua ya kwanza na bora ni kuondosha kwa mikono.

-          Hatua ya pili kwa ubora ni kuondosha kwa kusema.

-          Na hatua ya mwisho na dhaifu ni kuchukia moyoni.

 

Mafunzo ya Hadith kwa Ufupi:

1.      Ni wajibu kuondosha maovu kwa kisaidizi chochote kile kiwacho kulingana na mazingira.

2.      Jukumu la kuamrisha mema na kukataza maovu linaanzia kwa mtu mmoja mmoja na ummah kwa ujumla

3.      Kutochukia uovu na kuridhika nao ni dalili ya kukosa imani moyoni.

                                                                                                                                                                                                   

§  Hadith ya Pili: Sifa za Muumini wa kweli.

Kutoka kwa Ibn Umar (r.a) amesema: Kasema mjumbe wa Mwenyezi Mungu;

“Muislamu wa kweli ni yule wanaosalimika Waislamu kutokana na (maudhi) ya ulimi wake na mkono wake. Na muumini wa kweli ni yule wanaomuaminisha watu juu ya damu zao na mali zao.”      (Muttafaqun Alayhi)

Mafunzo ya Hadith kwa Ufupi:

1.      Haifai kuwaudhi, kuwafitinisha, n.k. waislamu, wanaadamu wengine pamoja viumbe kwa ujumla.

2.      Miongoni mwa maudhi ya ulimi ni kusengenya, kukejeli, kufitinisha, kupigana, kudhulumu na kuitanana majina mabaya.

3.      Uislamu ni dini ya mapenzi, huruma, kusaidiana na kushirikiana.

4.      Muumini wa kweli ni muaminifu kwa kila anachosema na kutenda pia.

 

§  Hadith ya Tatu: Ukarimu na Kusaidiana.

Kutoka kwa Abi Saidil-Khudhur (r.a) kasema: ilitokezea tumo safarini pamoja na Mtume (s.a.w); akaja mtu mmoja juu ya kipando chake, akawa anaangaza kulia na kushoto, Mtume (s.a.w) akasema;

“Mwenye kipando cha ziada na ampe msaada asiye na kipando, na mwenye chakula kilichozidi (matumizi yake) na ampe msaada mwenye kukihitaji (asiyenacho)”

 

Akataja aina mbali mbali za mali mpaka tukaona (tukajua) kwamba hatuna haki ya kuweka ziada (baada ya matumizi yetu).      (Ameipokea Muslim)

 

Mafunzo ya Hadith kwa Ufupi:

1.      Ni wajibu wa kila muislamu aliyenacho kumtilia hima kila anayehitaji msaada wa kibinaadamu.

2.      Ugawaji mbaya wa rasilimali na utajiri ndio sababu ya kuwepo matabaka ndani ya jamii.

3.      Uislamu umekataza kuhodhi bidhaa muhimu kwani kinyume cha sheria.

4.      Uislamu umetilia mkazo maisha bora kwa kila raia na kukataza kufanya israfu.

 

8.0 DOLA YA KIISLAMU MADINAH

     8.1. Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah.

-    Kabla ya kufika Madinah, Mtume (s.a.w) akiwa mji wa Quba aliamuru msikiti ujengwe uliokuwa Ukiitwa ‘Masjid Quba.’   Rejea Qur’an(9:108).

-    Mtume alifika Madinah (Yathrib), Oktoba 622 A.D.

-  Kwa heshima ya Mtume (s.a.w) Madinah ikapewa jina la Madinatun-Nabii (mji wa Mtume) na Al-Madinah Al-Munawwarah (mji ung’aao).

 

§    Hatua na Mambo (Taasisi za Kisiasa) za msingi alizotumia Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah.

1.      Kujenga Msikiti.

-  Msikiti ulikuwa ndio Ikulu, mahakama, kituocha jeshi, ukumbi wa bunge (shura), n.k. Qur’an(3:95), (2:150).

-  Ulikuwa kituo muhimu cha kiharakati katika kusimamisha na kuendeleza Uislamu. Rejea Qur’an(22:40), (2:114), (72:18) na (9:19).

 

2.      Kujenga Ummah wa Kiislamu.

-  Mtume (s.a.w) aliwapatanisha kabila la Aus na Khazraj Madinah waliokuwa na uadui wa muda mrefu baina yao. Qur’an(3:103).

-  Mtume (s.a.w) pia aliwaunganisha udugu imara kati ya Muhajirina wa  

-    Makkah na Answaar wa Madinah na kuwa ummah mmoja. Qur’an(8:75).

-  Pia aliimarisha uchumi kwa kuunganisha ummah wa Kiislamu na kuwa kitu  kimoja. Qur’an(59:8-9).

 

3.      Kuweka Mkataba wa Madinah (Madinah Charter).

-  Mtume (s.a.w) alijieleza katika mkataba huo kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ndiye kiongozi mkuu wa Dola ya Kiislamu.

-  Mkataba uliainisha vipengele vya amani na wajibu wa kila kundi kati ya makabila ya Mayahudi na Waarabu washirikina wa Madinah na Dola ya Kiislamu Madinah.

-  Uliainisha nafasi, majukumu na wajibu wa waumini katika Dola.

-  Mkataba uliainisha uhuru wa kila mtu kuabudu kwa mujibu wa imani na dini zao.

                                                                                                                                               

4.      Kuweka Mikataba ya amani na Makabila ya Mayahudi na mengine yaliyokuwa pembezoni mwa Dola ya Kiislamu Madinah.

-  Makabila na koo tatu za Kiyahudi zenye nguvu zilizokuwa pembezoni mwa mji wa  Madinah yalikuwa;

·         Banu Quraizah

·         Banu Qainuqa na

·         Banu Nadhir

5.      Kuunda Shura na Sekretarieti.

-  Mtume (s.a.w) aliteua washauri wake wakuu katika kuendesha Dola ambao Walikuwa Abu Bakr (r.a), Umar bin Khattab (r.a), Uthman bin Affan (r.a), Ally bin Abu Twalib (r.a) na   Hamza bin Abdul-Muttalib (r.a).

-  Aliteua waandishi maalumu wa kuandika na kutunza mikataba, takwimu, kumbukumbu na nyaraka zote za Dola ya Kiislamu Madinah.

 

6.      Kuandaa Ummah wa Kiislamu Kijeshi na Kiusalama.

-  Mtume (s.a.w) aliwaanda na kuwahimiza waislamu kuwa wakakamavu na hodari katika shabaha, mieleka na kutumia silaha.

-  Kila Muislam alikuwa mpiganaji na mpelelezi dhidi ya maadui wa waislamu na Dola ya Kiislamu.  Rejea Qur’an(4:71).

-  Aliunda na kuweka vikosi vya doria na ulinzi kuzunguka mipaka ya Dola ya Kiislamu Madinah. Qur’an(8:26).

 

7.      Kuimarisha Uchumi.

-  Mtume (s.a.w) aliwahimiza waislam kufanya kazi kwa bidii ili kujiimarisha Kiuchumi na kuendeleza Dola.

-  Utoaji wa Zaka, Sadaka na mapato mengine yalihimizwa na kukusanywa Kijamii na kuboresha huduma za jamii.    Rejea Qur’an(22:41).

                                                                                               

§  Mafunzo yatokanayo na Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah.

Kutokana na mambo ya msingi aliyoyafanya Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah tunajifunza yafuatayo;

1.      Hatunabudi kuanzisha na kuendesha vituo vya harakati, msikiti ukiwa ndio kitovu cha msingi.

2.      Mshikamano, kuhurumiana na kupendana kwa vitendo baina ya waislamu ndio nyenzo pekee katika kuhuisha na kuendeleza harakati za Kiislamu.

3.      Hatunabudi kuishi vizuri, kuwahesimu na kuwatendea haki, wasiokuwa waislamu hasa wale wasiopiga vita waislamu na Uislamu wazi wazi.

4.      Ni wajibu kwa kila muislamu kuwa mkakamavu, jasiri na kujifunza mafunzo ya kijeshi na kuwa tayari kulinda na kuupigania Uislamu katika jamii.

5.      Hatunabudi kuwajua vema maadui wa Uislamu na Waislamu, mbinu na silaha zao na kuchukua tahadhari dhidi yao.

6.      Ni wajibu kuimarisha uchumi wetu kwani ndio nyenzo muhimu na ya msingi katika kuendesha harakati za Kiislamu.

7.      Uongozi bora, makini na uwajibikaji wa kila mmoja kulingana nafasi yake ndio kiungo muhimu katika kuendesha harakati za Kiislamu.

 

8.2. Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Madinah.

§  Mfumo wa Mapato na Uchumi katika Dola (Serikali) ya Kiislamu Madinah.

Dola (Serikali) ya Kiislamu Madinah ilipata mapato yake kupitia njia zifuatazo;

 

1.      Zaka na Sadaka ndio ilikuwa njia kuu ya kukusanya mapato ya serikali (Dola) ya Kiislamu iliyowahusu waislamu wote wenye uwezo.

2.      Jizya – Ni kodi waliokuwa wanalipa wasiokuwa waislamu wanaume tu wenye uwezo wa kuwa askari kwa ajili ya ulinzi wa Dola.

3.      Al-Kharaj – Ni kodi waliolipa wasiokuwa waislamu, walio na mashamba katika Dola ya Kiislamu.

4.      Al-fay – Ni mapato yanayotokana na mashamba ya Serikali (Dola) ya Kiislamu Madinah.

5.      Al-Ghanimah (Ngawira) – Ni mapato yanayotokana na mali ilitekwa katika vita, iliyolipwa 1/5 ya mali yote ilyotekwa.

6.      Ushr – Ni kodi (ushuru) iliyotolewa na waislamu wenye ardhi katika Serikali (Dola) ya Kiislamu kwa kiwango cha 10% kwa maji ya asili (mvua) na 5% kwa maji ya kumwagilia.

7.      Zaraib – Ilikuwa ni kodi zilizotozwa na serikali (Dola) ya Kiislamu kwa muda kwa ajili ya maslahi ya nchi.

 

§  Msonge wa Uongozi na Siasa katika serikali (Dola) ya Kiislamu Madinah.

Tofauti na serikali zingine, serikali ya Kiislamu ilijengwa katika misingi mikuu mitatu; Tawhiid, Utume na Ukhalifa (nafasi ya mwanaadamu hapa ulimwenguni). Rejea Qur’an(30:20), (3:189), (12:40), (7:54), (4:80), (4:65), (24:55), (2:30).

Mgawanyo na msonge wa uongozi wa Dola ya Kiislamu ulikuwa kama ifuatavyo;

-     Qur’an– ilikuwa ndio Katiba kuu (Constitution) ya kuongozea Dola iliyotafsiriwa kivitendo (Sunnah) na Mtume (s.a.w) mwenyewe. 

-     Mtume (s.a.w.) – alikuwa ndio kiongozi na amiri jeshi mkuu (commander in chief) wa Dola ya Kiislamu aliyesimamia na kuendesha kazi zote za Dola ambapo Msikiti ulikuwa ndio Ikulu ya Dola (State House).

-     Shura (Cabinet) – Mtume (s.a.w) aliteua washauri wake wakuu wakaribu, weledi na wazoefu (Baraza la Mawaziri) katika shughuli zote za kuongoza Dola ambao ni Abu Bakr (r.a), Umar bin Khattab (r.a), Uthman bin Affan (r.a), Ally bin Abu Twalib (r.a) na Hamza bin Abdul-Muttalib (r.a) na wengineo.

-     Sekretarieti (Secretarial) – Mtume (s.a.w) aliteua jopo la waandishi na watunza kumbukumbu na nyaraka zote za serikali.

-     Wali au Gavana – Walikuwa ni wakuu wa majimbo (mikoa) ambao waliteuliwa na Mtume (s.a.w) ili kuhakikisha sheria na haki zinatekelezwa ipasavyo katika majimbo yao.

-     Amil – Walikuwa ni wakusanyaji wa Zaka na Sadaka walioteuliwa na Mtume (s.a.w) kila jimbo la Dola ya Kiislamu.

-     Kadhi – Mtume (s.a.w) alikuwa ndiye Jaji mkuu wa Dola ya Kiislamu na aliteua Kadhi (Jaji) kila jimbo (mkoa) aliyesimamia haki na hukumu zote kwa mujibu wa Qur’anna Hadith.

§  Mfumo wa Ulinzi na Usalama katika Dola ya Kiislamu Madinah.

Dola (serikali) ya Kiislamu Madinah iliposimama na kuanza kazi za kuongoza jamii iliandamwa na maadui wa kila aina. Mtume (s.a.w) aliweka mikakati na mbinu madhubuti za kuilinda na kuihami serikali yake ikiwa ni pamoja na;

                                                  i.      Misafara ya Kujihami (Patrol) na Upelelezi.

Mtume (s.a.w) aliweka watu maalum kwa ajili ya kulinda mipaka ya Dola na kupeleleza harakati za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu.Rejea Qur’an(4:71).

                                                ii.      Kuweka Mikataba ya amani.

Mtume (s.a.w) aliweka mikataba ya amani na makabila ambayo hayakusilimu yaliyopembezoni mwa Dola ya Kiislamu kama, Banu Dumra, Mudlaj, n.k.   Rejea Qur’an(9:13-15).

                                              iii.      Kupigana vita.

Njia hii ililazimika kutumika baada ya kuzidi uonevu, dhuluma na choko choko za wazi dhidi ya Waislamu na Uislamu.Rejea Qur’an(2:193), (9:111) na (9:29)

                                              iv.      Sera ya wazi juu ya wanafiki.

Mtume (s.a.w) alichukua tahadhari na hatua dhidi ya wanafiki waliojidhihirisha wazi kutengana na ummah wa waislamu kwa kuwatenga.Rejea Qur’an(9:73), (9:84) na (9:80).

                                                 v.      Sera ya Uislamu juu ya amani.

Mtume (s.a.w) alitekeleza na kuelekeza mafundisho ya Uislamu juu ya kutunza na kulinda amani kama fursa na dhamana katika kueneza Uislamu.   Rejea Qur’an(8:61), (16:90), (2:84), (8:5-8).

                                              vi.      Uhusiano wa Kiplomasia na nchi za nje.

Mtume (s.a.w) aliweka sera ya wazi juu ya uandikashaji na utekelezaji wa mikataba mbali mbali na maadui wa Uislamu kama Aqaba, Hudaybiyah, n.k.   Rejea Qur’an(5:8), (42:40-42), (60:8).

 

§  Madhumuni ya Dola ya Kiislamu.

1.      Kujenga maisha ya mwanaadamu yaliyo katika misingi ya (Tawhiid) Ucha-Mungu na matendo mema.

2.      Kuondosha uovu, dhuluma,ukandamizaji,maasi,ukatili, tabaka, unyonyaji, uonevu, n.k katika jamii. Qur’an(57:25).

3.      Kutumia mamlaka katika kusimamia na kuendeleza maadili katika maisha ya jamii. Qur’an(22:25).

4.      Kusimamia na kulinda haki na uadilifu kwa wanaadamu wote na viumbe wengine.

 

8.3. Upinzani dhidi ya Dola ya Kiislamu Madinah.

§  Maadui wakubwa wa Dola ya Kiislamu Madinah.

Kwa kipindi cha miaka 10 ya uongozi wa Mtume (s.a.w) maadui walioibuka kupambana na Dola ya Kiislamu walikuwa;

o   Makafiri wa Kabila la Kiquraish.

o   Wanafiki.

o   Mayahudi

o   Warumi (Wakristo).

o   Makabila mengine ya Kiarabu

§  Mbinu na njia walizotumia maadui wa Uislamu dhidi ya Waislamu na Dola ya Kiislamu Madinah.

Rejea Kitabu cha 3, EDK – Shule za Sekondari; Uk. 250 - 352.

 

o   Makafiri wa Kiquraish.

-  Walivamia mji wa Madinah na kupora mifugo na kuipeleka Makkah.

-  Walimwandikia barua kwa kiongozi wa wanafiki Abdullah bin Ubayyi kumtaka wamfukuze Mtume (s.a.w) kutoka mji wa Madinah.

-  Kuwatishia vita makabila yaliyokuwa yakiishi kati ya Makkah na Madinah yawe dhidi ya Uislamu na wasijekusilimu.

-  Walichoma moto mashamba ya mitende ya waislamu Madinah.

-  Walimchoma mkuki Zainabu bint Muhammad (s.a.w) wakati akielekea Madinah.

 

o   Wanafiki.

-  Walikuwa wanatoa nyudhuru za uongo kuepuka jukumu la kupigana jihadi.

-  Walimzulia uzinifu mke wa Mtume (s.a.w) Aisha (r.a) kuwa amezini na sahaba Safwan (r.a) wakati wa kurudi msafara wa Banu Mustaliq.

-  Walijenga msikiti wao kama kichaka cha kupiga vita Uislamu na kutaka kumuua Mtume (s.a.w).

-  Walishirikiana na maadui wengine wa Uislamu ili kuupiga vita Uislamu.

-  Walijitenga wanafiki 300 katika vita vya Uhudi na kuwaacha waislamu 700 Waliopambana na maadui wa Kiquraish 3,000 waliojizatiti kivita.

-  Walichochea ugomvi baina ya Muhajirina na Answar na kutishia kumfukuza Mtume (s.a.w) Madinah wakiongozwa na Abdullah bin Ubayyi katika msafara wa vita vya Banu Mustaliq.

 

o Mayahudi.

                        - Walishirikiana na wanafiki katika kuwatia wasi wasi waislamu walipobadilishiwa Qibla kutoka Jerusalemu na kuelekea Al-Kaaba, Makkah.

                        -     Walitangaza kuwa Mtume (s.a.w) ni mtume wa uongo.

                        -     Waliifanyia Qur’anstihizai (mzaha).   Rejea Qur’an(2:245), (3:181).

-     Wamjaribu Mtume (s.a.w) kwa kumuuliza maswali ya kubabaisha yasiyo na majibu ya dhahiri, kama vile:

·         Usingizi wako ukoje.

·         Ni vitu gani Israil (Nabii Yaaqub) alijiharamishia mwenyewe.

·         Ni malaika yupi anakuletea wahayi, n.k.

 -   Kuwavunja moyo na kuwadhalilisha waislamu.

-  Walishirikiana na Wanafiki kwa njama za kutaka kumuua Mtume (s.a.w) na kuuhilikisha Uislamu.

-  Walivunja na kusaliti mikataba ya amani waliowekeana na Mtume (s.a.w).        

-  Walichochea fitina baina ya Answar kwa kuwakumbushia ugomvi wao wa zamani baina ya Aus na Khazraj.  Rejea Qur’an(3:100-101).        

 

o   Warumi (Wakristo).

-     Gavana, Shurahbil bin Amr Ghassaany wa Dola ya Kirumi alimuua mjumbe wa Mtume (s.a.w), Haarith Bin Umair Al-Az katika mji wa Muttah.     

·         Mtume (s.a.w) alituma jeshi la askari 3,000 kupambana na jeshi la Kirumi lenye askari 100,000.

 

·         Mtume (s.a.w) alichagua makamanda watatu, ambao ni Zaid bin Harith (r.a), Ja’afar bin Abi Twalib (r.a) na Abdullah bin Rawahah (r.a) na kuwaagiza kuwa akiuawa moja anayefuatia achukue nafasi na wakiuawa wote basi wamchague miongoni mwao aongoze jeshi.

 

·         Makamanda wote 3 waliuawa na hatimaye walimchagua Kamanda Khalid bin Walid (r.a) aliyeoongoza jeshi kishujaa na kupelekea kupata ushindi.

 

·         Kutokana na ushujaa walioonyesha waislamu katika vita vya Muttah, Warumi walipata woga na kulikimbia jeshi la waislamu katika msafara wa Tabuuk.

 

·         Kuwashinda Warumi kulipelekea Dola ya Kiislamu kuwa Super Power ya Ulimwengu wakati wa Mtume (s.a.w) na ndio kutimia lengo la kuletwa kwake.   Rejea Qur’an(48:28).

 

o   Makabila mengine ya Waarabu.

-     Mtume (s.a.w) alilishughulikia na kulitia adabu kila kabila la Kiarabu lililojaribu kuleta choko choko dhidi ya Dola ya Kiislamu.

-     Makabila ya Taif ya Bani Thaqif na Bani Hawazin yaliyokuwa na nguvu kijeshi, Mtume (s.a.w) aliyasambaratisha katika vita vya Hunain akiwa na askari 12,000,  baada ya Fat-h Makkah mwaka wa 8 A.H.

·         Katika vita vya Hunain, Mwenyezi Mungu (s.w) aliwaacha Waislamu wapate fundisho kwanza, kwa kupata kipigo kutoka kwa maadui.

·         Mwenyezi Mungu (s.w), aliwaonesha waislamu kuwa, ushindi wao haupatikani kwa wingi na ubora wa silaha zao tu, bali kwa msaada wake.

·         Baada ya fundisho hilo, waislamu walipata ushindi wa kishindo baada ya Mwenyezi Mungu (s.w) kushushia Malaika.

·         Waislamu walipata ushindi na kuchukua ngawira mbali mbali zikiwemo;

-          Ngamia 24,000

-          Kondoo 40,000

-          Aqyyah (fedha taslim) 4,000/=

-          Mateka 6,000

“Bila shaka Mwenyezi Mungu amekunusuruni katika mapigano mengi, na siku ya Hunayni (pia); ambapo wingi wenu ulikupandisheni kichwa, lakini haukukufaeni chochote, na ardhi ikawa dhiki juu yenu; ingawa ilikuwa yenye wasaa, kisha mkageuka mkarudi nyuma (mnakimbia). Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume Wake na juu ya walioamini. Na akateremsha majeshi (ya Malaika) ambayo hamkuyaona, na akawaadhibu wale waliokufuru; na hayo ndiyo malipo ya makafiri.” (9:25-26).

 

§  Vita vya Badri.

-     Vilikuwa ndio vita vya kwanza vya jihad vilivyopiganwa siku ya Ijumaa mwezi 17 Ramadhani, mwaka wa 2 A.H (624 A.D) katika bonde la Badri. 

 

-     Chanzo cha vita ni kuwa mtume (s.a.w) alikusudia kuuzuia msafara wa Maquraish wa Makkah uliotokea Syria (Sham) uliosheheni bidhaa zenye thamani ya dinar 50,000 kwa ajili ya maandalizi ya kuupiga vita Uislamu na Waislamu.

 

-     Mtume (s.a.w) alikuwa na askari 313, ngamia 70 na farasi 2 tu na Makafiri wa Kiquraish wakiwa askari 1000 waliojizatiti kivita, ngamia 700 na farasi 300.

 

-     Waislamu walipata ushindi kwa waliuawa Maqurish 70 wengi wao wakiwa vigogo wa Makkah na waislamu 14 tu waliuawa. 

      Rejea Qur’an(3:123-124), (8:9-11), (54:45), (8:65), (8:17) na (8:48).

Mafunzo kutokana na Vita vya Badri.

1.      Ushindi wa waislamu katika vita unatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na sio kutokana na ubora wa silaha na wingi wa askari.Rejea Qur’an(3:123-124), (8:42-45).

 

2.      Tunajifunza pia namna ya kuwafanyia mateka wa kivita ikiwa ni pamoja na;

-  Kuwapatia haki na huduma zote msingi za kimaisha, kibinaadamu na kiutu.

-  Kuwalea na kuwafanyia wema na uadilifu kama wanafamilia wengine.

-  Kwa mateka wanaoweza kuleta madhara kwa waislamu na Uislamu, ni bora

    kuuawa badala ya kuachwa huru kwa kujikomboa.   Rejea Qur’an(8:67-69).

 

3.      Mwenyezi Mungu (s.w) aliwaadhibu makafiri na kuwanusuru waislamu katika vita vya Badri na hawakuadhibu walipokuwa Makkah kwa sababu walikuwa pamoja na Mtume (s.a.w) na pia walipewa muda wa kutubia.  Rejea Qur’an(8:32-34) na (8:19).

 

4.      Tunajifunza pia, inafaa nguvu ya kivita kutumika ikibidi katika kuzuia na kuondoa uovu, udhalimu, uonevu na choko choko za maadui.  Rejea Qur’an(8:60) na (60:8-9).

 

5.      Tunajifunza pia, Uislamu bila ya juhudi za kweli kufanyika na kumwagika damu na kujitoa muhanga ipasavyo, hautasimama katika jamii.

 

6.      Choko choko na mbinu za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu ni zenye kuendelea na hazitaisha kamwe hadi siku ya Qiyama.

 

§  Vita vya Uhudi.

-     Sababu ya kutokea vita vya Uhudi ni Maquraish kutaka kulipiza kisasi dhidi ya waislamu baada ya kushindwa katika vita vya Badri.

 

-     Maquraish waliandaa msafara wa biashara wenye thamani ya Dirham 300,000 kuelekea Iraq kama maandalizi ya kulipiza kisasi vita vya Badri.

 

-     Kikosi cha waislamu kikiongozwa na Zaid bin Harith (r.a) kiliteka msafara huo na kuchukua mali yenye thamani ya Dirham 100,000 na mateka 2.

 

-     Vita vilipiganwa siku ya Jumamosi, mwezi 15 Shawwal, mwaka wa 3 A.H (625 A.D) katika milima ya Uhudi nje ya mji wa Madinah.

 

-     Waislamu walikuwa 700 (baada ya wanafiki 300 kurudi nyuma wakiongozwa na Abdullah bin Ubayyi) na Maquraish wakiwa askari 3,000 waliojizatiti kivita, (700 wamevaa mavazi ya chuma), farasi 200 na ngamia 3,000.

 

-     Kwa waislamu kiongozi alikuwa Mtume (s.a.w) na kwa Maquraish viliongozwa na Hindu bint Utbah mkewe Abu Sufyan.

 

-     Mtume (s.a.w) aliteuwa kikosi cha watu 50 wakiongozwa na Abdullah bin Jubeir kukaa juu ya mlima ili kulinda kikosi cha maadui kikiongozwa na Khalid bin Walid.

 

-     Vita vilipoanza waislam walipata ushindi lakini baadae kugeuka kipigo baada ya waislamu 43 kuondoka mlimani na kupelekea Mtume kuvunjwa meno 2.

 

-     Waislamu 70 waliuuawa akiwemo shujaa Hamza bin Abdi Muttalib (r.a) aliyeuliwa na mtumwa Wahshi bin Harbi aliyeandaliwa na Hindu bint Utbah.

Mafunzo yatokanayo na Vita vya Uhudi.

1.      Lengo la maadui wa Uislamu na waislamu kupigana ni kuwaangamiza wao, kuharibu miji yao na mali zao pia. Hivyo ni wajibu waislamu kuwa na tahadhari muda wote kupambana na maadui wao.

 

2.      Kushauriana katika kupanga mambo ni jambo la busara sana, kama alivyoshauriana Mtume (s.a.w) juu ya sehemu ya kupiganwa vita vya Uhudi.

Rejea Qur’an(3:159) na (3:166-167).

 

3.      Tunajifunza pia ni wajibu waislamu kutumia mbinu, ujuzi, uzoefu, na jitihada za kivita pamoja na kuwa wanapata msaada wa Mwenyezi Mungu (s.w).Rejea Qur’an(8:60).

 

4.      Msaada wa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa waislamu unapatikana pale tu waislamu watakapotii amri zake na wakapigania dini vilivyo.Rejea Qur’an(3:151-152).

 

5.      Kuvunja na kutotii amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake hupelekea kutofikia mafanikio hata kama watajizatiti na kufanya jitihada ipasavyo.  Rejea Qur’an(3:152), (3:165) na (33:36).

 

6.      Tunajifunza pia, makosa ya watu wachache yasipuuzwe na kufumbiwa macho bali yarekebishwe kwani athari yake itasibu jamii nzima.Rejea Qur’an(8:25).

 

7.      Mwenyezi Mungu (s.w) anatukumbusha kuwa pepo haipatikani kwa kutamani, lele mama na ushabiki bali, kufanya jitihada ya kweli. Rejea Qur’an(3:142-150), (3:156-160) na (3:169-171). 

 

8.      Msamaha na nusura ya Mwenyezi Mungu (s.w) upo karibu kwa waislamu pindi watakapotubia na kurejea kwake na kupambana na maadui ipasavyo.Rejea Qur’an(3:152-154), (3:166-167) na (3:139-141).

 

9.      Ushindi wa waislamu katika vita unatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na sio kutokana na ubora wa silaha na wingi wa askari.   Rejea Qur’an(3:123-124), (8:42-45).

 

10.  Choko choko na mbinu za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu ni zenye kuendelea na hazitaisha kamwe hadi siku ya Qiyama.

§  Vita vya Ahzab

-     Maquraish waliungana na mayahudi, wanafiki na makabila mengine ya waarabu baada ya kuona kuwa wao peke yao hawawezi kuufuta Uislamu.

 

-     Makafiri wakiwa 10,000 waliojizatiti kivita mwaka wa 5 A.H. kwa ajili ya kuivamia Madinah na waislamu wakiwa askari 3,000 tu na dhaifu kwa njaa.

 

-     Waislamu kupitia rain a ushauri wa Salman Al-Farsy walibuni kuchimba handaki lenye upana yadi 5 na kina yadi 5 kuzunguka mji wa Madinah.

 

-     Maadui walipozingira, walishindwa kuruka handaki na wakawa wamezingira mji wa Madinah kwa muda wa mwezi 1.

 

-     Waislamu walipata dhiki kubwa ya njaa siku 3 na zaidi na huku wakiendelea kuchimba mtaro.

 

-     Waislamu walishinda kwa kupata nusura kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) baada ya kuletwa mvua na upepo mkali uliowakimbiza maadui. Rejea Qur’an(33:9-15), (33:25).

 

Mafunzo yatokanayo na vita vya Ahzab (Handaki).

1.      Kushauriana katika kupanga mambo ni jambo la busara sana, kama alivyoshauriana Mtume (s.a.w) juu ya sehemu ya kupiganwa vita vya Uhudi.

Rejea Qur’an(3:159) na (3:166-167).

2.      Tunajifunza pia ni wajibu waislamu kutumia mbinu, ujuzi, uzoefu, na jitihada za kivita pamoja na kuwa wanapata msaada wa Mwenyezi Mungu (s.w). Rejea Qur’an(8:60).

3.      Msamaha na nusura ya Mwenyezi Mungu (s.w) upo karibu kwa waislamu pindi watakapotubia na kurejea kwake na kupambana na maadui ipasavyo.

Rejea Qur’an(3:152-154), (3:166-167) na (3:139-141).

4.      Ushindi wa waislamu katika vita unatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na sio kutokana na ubora wa silaha na wingi wa askari.  Rejea Qur’an(3:123-124), (8:42-45).

5.      Choko choko na mbinu za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu ni zenye kuendelea na hazitaisha kamwe hadi siku ya Qiyama.

 

 8.4. Mkataba wa Hudaibiyah.

                    -   Ni mkataba wa amani baina ya waislamu na Maquraish wa Makkah, mwaka wa         6 A.H, Dhul-Qa’adah (Machi, 628 A.D) katika kitongoji cha Hudaybiyah karibu na

Mji wa Makkah.

       -    Mkataba ulitiwa saini na Mtume (s.a.w) kwa niaba ya waislamu na Suhail bin Amri

 Kwa niaba ya Makafiri wa Kiquraish.

 

§  Yaliyopelekea kutokea kwa Mkataba wa Hudaybiyah.

-     ilikuwa Mtume (s.a.w) kutimiza ndoto (wahay) aliyoota mwaka 6 A.H. kuwa kuna siku atafanya ‘Umrah’.

-     Mtume (s.a.w) akiwa na waislamu 1,400 walikwenda kufanya ibada ya ‘Umrah’ lakini walizuiliwa na Maquraish katika kitongoji cha Hudaibiyah wasiingie Makkah.

-     Mtume (s.a.w) alituma wajumbe 2, mmoja baada ya mwingine ili kuwaomba Maquraish wawaruhusu waingie Makkah, lakini walikataliwa.

-     Mtume (s.a.w) alituma mjumbe wa 3, ‘Uthman bin Affan’ (r.a) aliyeshikiliwa na Maquraish kwa muda, na kuja tetesi kuwa ameuawa.

-     Mtume (s.a.w) aliwakusanya waumini chini ya mti na kuchukua kiapo cha utii (Bai’at) juu ya kulipiza kisasi cha ‘Uthman bin Affan’ (r.a), lakini baadaye alirejea.

      Rejea Qur’an(48:18).

-     Maquraish kwa kuwaogopa waislamu, walimuomba Mtume (s.a.w) kuweka mkataba wa amani na Mtume (s.a.w) alikubali, na ukaitwa “Mkataba wa Hudaybiyah”.

      Rejea Qur’an(48:1).

§  Vipengele vya Mkataba wa Hudaybiyah.

1.      Waislamu warudi Madinah bila kufanya ‘Umrah’.

2.      Waislamu wanaweza kurudi mwakani (7 A.H) kufanya ‘Umrah’ lakini wakae siku tatu.

3.      Wakija Makkah wasije na silaha ila panga zikiwa ndani yah ala zao.

4.      Waislamu hawataenda nao Madinah waislamu wanaoishi Makkah na wala hawatamzuia yeyote miongoni mwao anayetaka kubakia Makkah.

5.      Kama yeyote wa Makkah atatoroka kwenda kusilimu, Waislamu hawana budi kumrudisha (wasimpokee), lakini yeyote kutoka Madinah akitoroka kwenda Makkah kuritadi, Maquraish hawatapaswa kumrudisha Madinah (watampokea).

6.      Makabila ya Waarabu yatakuwa huru kufanya Itifaki (urafiki) na upande wowote ule yanaoupendelea.

7.      Pasiwe na vita kwa kipindi cha miaka 10 baina ya waislamu na Maquraish na baina ya waitifaki (Allies) wa Waislamu na waitifaki wa Maquraish.

8.      Hapana ruhusa ya kutengua hata sharti moja katika hizi kabla ya miaka 10 kupita.

 

Mafunzo yatokanayo na Mkataba wa Hudaybiyah.

1.      Ahadi ya Mwenyezi Mungu (s.w) siku zote ni ya kweli na yenye kutimia, kama alivyotimiza ahadi kwa Mtume (s.a.w) alipoota kuwa siku 1 atakwenda ‘Umra’. Rejea Qur’an(48:27).

 

2.      Katika kusimamisha Uislamu, ni lazima pawepo na mbinu na mipango maalumu ya muda mfupi na muda mrefu ili kufikia malengo yetu katika nyanja yeyote ile.

Kama alivyofanya Mtume (s.a.w) katika mkataba wa Hudaibiyah:

-     Kufuta ‘Bismillahir Rahmaanir Rahiim’,

-     Kufuta ‘Muhammad Rasulullaah’.

-     kukubali kipengele cha 4 na 5 ijapokuwa vilikuwa vinawadhalilisha waislamu.

Rejea Qur’an(48:18), (48:29) na (48:22).

 

3.      Waumini walipata maliwazo ya Mwenyezi Mungu (s.w) baada ya kukata tamaa kutokana na uonevu wa baadhi ya vipengele vya Mkataba wa Hudaibiyah.   Rejea Qur’an(48:20-29) na (48:1-8).

 

4.      Tunajifunza pia, ni wajibu kutekeleza mikataba tuliyoandikiana hata ikiwa na Makafiri, kama alivyotekeleza Mtume (s.a.w) mkataba wa Hudaybiyah. Rejea Qur’an(48:10) na (60:10-12).

5.      Ni wajibu kufikisha ujumbe wa Qur’ankwa wasio waislamu na viongozi wao, kama alivyofanya Mtume (s.a.w) kwa kutuma mabalozi sehemu mbali mbali.

 

6.      Mazingira ya amani na utulivu ni jambo la muhimu sana katika kueneza na kuendeleza ujumbe wa Uislamu, hivyo mapatano ni bora zaidi kuliko kupigana.

7.      Waislamu tuwe wepesi katika kutumia fursa zinazopatikana na kupelekea kufikia malengo yetu ya kuusimamisha Uislamu katika jamii.

8.      Tuwe tayari kupoteza maslahi madogo madogo katika kutafuta fursa, mazingira na suluhu inayopelekea kufikia lengo kuu.

9.      Tuwe na uvumilivu na subira kwa kutotegemea matunda ya kusimamisha Uislamu kupatikana haraka na bila ya misukosuko.

10.  Nusura na ushindi kwa waislamu hupatikana baada ya waislamu kufanya juhudi ya dhati mwisho wa uwezo wao.    Rejea Qur’an(48:1).

§  Matunda (ushindi) yatokanayo na Mkataba wa Hudaybiyah.

1.      Waislamu walipata fursa ya kulingania Uislamu na watu wengi walisilimu wakiwemo majemedari kama, Khalid bin Walid, Suhail bin Amr na Amr bin Al-As na wengineo.

Rejea Qur’an(48:1).

 

2.      Kuhamia jangwani kikosi kilichosilimu na kuwa tishio kwa misafara ya Maquraish, Maquraish walimuomba Mtume (s.a.w) kuondoa kipengele kilichowakataza wanaosilimu Makka kwenda Madinah kilichokuwa kero kwa waislamu.

 

3.      Mtume na waislamu walipata fursa ya kuutangaza Uislamu ndani na nje ya Bara Arabu kama vile, Mashariki ya kati, Misr, Uhabeshi na Wafalme mbali mbali.

Rejea Qur’an(3:64).

4.      Waislamu walipata fursa ya kujiimarisha kiuchumi kwa kufanya biashara hasa za masafa ya mbali kwa amani na falme za nje ya Bara Arab.

 

5.      Waislamu waliweza kujizatiti kijeshi na kuweza kuwadhibiti maadui wa Uislamu na waislamu katika mapigano mbali mbali kama;

     -      Wayahudi (Warumi) katika vita vya Khaibar na Muttah mwaka wa 7 A.H.

     -      Ushujaa wa waislamu yalisababisha maadui kuwakimbia msafara wa Tabuuk.      

6.      Mtume (s.a.w) akiwa na waislamu 2,000 walifanikiwa kufanya Umrah mwaka wa 7 A.H (badala ya wale 1,400 waliorudishwa 6 A.H.) na kutimiza ndoto yake ya ushindi.  Rejea Qur’an(48:27).

 

7.      Fat-h Makkah – kilele cha ushindi, baada ya Maquraish na Waitifaki wao kuvunja mkataba wa Hudaybiyah baada ya muda wa miaka 2 tu, na Mtume alitumia fursa hii kuikomboa Makkah bila vita.

 

§  Fat-h Makkah (Kukombolewa Makkah).

-     Mtume (s.a.w) aliandaa askari 10,000 mwezi 10 Ramadhani, 8 A.H (Januari 1, 630 A.D) kuelekea Makkah.

-     Kukombolewa Makkah kulipelekea kusilimu Abu Sufyan na viongozi wengine wa Makka na kuwa kishawishi kusilimu watu na makabila mengi pia.

 

-     Baada ya Fat-h Makka, waislamu waliyashinda makabila ya Waarabu yenye nguvu kama; Banu Thaqif na Banu Hawazin katika vita vya Hunain.  Rejea Qur’an(17:81).

 

-     Dola ya Kiislamu chini ya uongozi wa Mtume (s.a.w) ilienea Bara Arab nzima na aliigawanya katika majimbo na kuteuwa Walii, Kadhi na Amil kama viongozi kwa kila jimbo.

 

8.5. Hija ya Kuaga na Kutawafu kwa Mtume (s.a.w).

-     Ilikuwa mwaka wa 10 A.H alikwenda kuhiji na Waislamu zaidi ya 100,000 baada ya kutimia miaka 23 ya Utume.  Rejea Qur’an(5:3).

-     Mtume (s.a.w) mwezi 9 Dhul-Hija, 10 A.H akiwa Viwanja vya Arafa, alikhutubia waislamu akiwa juu ya ngamia.

-     Mtume (s.a.w) alianza kuugua miezi miwili baada ya Hija ya Kuaga na hatimaye alifariki jioni siku ya Jumatatu mwezi 12 Rabi’al-Awwal, 11 A.H.(Juni 8, 632 A.D.) akiwa na umri wa miaka 63.

***************************************

==================================

Wabillah Tawfiiq

 

Join WhatsApp Channel